Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, May 4, 2012

Ujambazi sasa tishio Haydom

Jana usiku majira ya saa mbili kumeripotiwa tukio la ujambazi nje kidogo ya mji wa Haydom ambapo mwendesha pikipiki moja alipigwa mapanga kichwani na watu wasiofahamika katika eneo la Qorong`ayda karibu na kwa Simon Matre. Majeruhi huyo ambaye bado Ohayoda haijafahamu jina lake amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Kilutheri ya Haydom (HLH) akiwa na hali mbaya.


Tukio hili limetokea wakati bado kukiwa na sintofaham kuhusu utekaji wa magari hivi karibuni na kuibua hali ya wasiwasi kwa wakazi Haydom na vitongoji vyake kwani wimbi la ujambazi linazidi huku kukiwa hakiwa hakuna juhudi zozote kutoka jeshi la polisi kulishughulikia tatizo hili. Akizungumzia hali hiyo, mkazi wa Haydom ambaye anafanya kazi katika Hospitali ya Haydom, Bi. Janeth John alisema kuwa wanachi hawana imani na polisi kwani wimbi la ujambazi linazidi toka utekaji wa magari na sasa mashambulizi ya kudhuru watu, polisi haijatoa tamko lolote.
Aidha wananchi hao wamedai kuwa polisi walipopigiwa simu walidai kuwa gari halina mafuta na badala yake kuwageuzia kibao waathirika kwa kuwahoji kwa nini wanatembea usiku! "Tunakoelekea ni kubaya sana, saa mbili usiku na polisi badala ya kutoa msaada wanatoa majibu ya kejeli" alieleza mkazi moja aliyetambulika kwa jina moja la Elibariki. Alizidi kuhoji kazi ya polisi ni nini kama hawapambani na uhalifu ilhali wakiwanyanyasa waendesha pikipiki kwa kuwakamata hata pasipo na makosa yanayoeleweka huku wakiwaacha wahalifu.

Katika hatua nyingine baada ya tukio la jana eneo la Qorong`ayda ambalo hivi karibuni gari la wagonjwa lilitekwa maeoneo hayohayo, wazee kutoka maeneo ya Bisigeta, Maghang, Qorong`ayda na maeneo ya jirani wamekutana leo asubuhi na kutoa laana kwa wote wanaohusika na matukio haya ya ujambazi.

Ikumbukwe kuwa jana Ohayoda ilirepoti kuhusu tukio la utekaji magari hususani gari lakubebea wagonjwa la HLH na wazee wakadhamiria kuendesha shughuli ya utoaji laana siku ya jumamosi tarehe 06 may 2012 na sasa shughuli hiyo imefanyika leo.
Je nini kitafuata baada ya matukio haya? Wananchi hawana imani na jeshi la polisi na kunawasiwasi kuwa wananchi watafikia hatua ya kujichukulia sheria mikononi kama ilivyotokea miaka ya 1990 ambapo majambazi mawili yaliyokuwa yakisumbua sana watu Haydom yalipopigwa na wanachi wenye hasira na kuchomwa moto baada ya matukio ya uporaji, uvamizi wa Hospitali na kuiba mashine ya kusukuma maji. Tukio kama hilo pia lilitokea Dongobesh ambapo wananchi walijichukulia sheria mikononi baada ya kuvamia wahalifu waliokuwa chini ya ulinzi wa polisi na kuwaua baada ya kupoteza imani na jeshi hili.
Juhudi za Ohayoda za kuwasiliana na mkuu wa polisi kituo cha Haydom hazikufanikiwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda