Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, May 7, 2012

Tukumbuke nyumbani: Tusisubiri hadi uchaguzi na wakati wa ndoa!

Wanakijiji wa kijiji cha Endaharghadatk wametoa wito kwa watu mbalimbali hasa wasomi waliosoma kijijini hapo na wengine wanaopenda maendelea kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo kijijini hapo. Wakizungumza na Ohayoda kwa nyakati tofauti, Mwenyekiti wa kijiji hicho ndugu Martini Ako na diwani wa kata ya Haydom ndugu Nasaeli Sulle wamewaomba wasomi kukumbuka nyumbani na kuchangia maendeleo walikotoka.
``Wanakijiji wanajitahidi kujitolea kwenye shughuli za maendeleo, bado tunaendelea na ujenzi wa madarasa, maabara, mabweni ya wasichana na nyumba za walimu za shule ya Sekondari ya Kijiji (Mama Kari Secondary School), tunaujenzi wa zahanati na pia ujenzi wa ofisi ya kijiji`` alise,a Martin Ako
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa, wanakijiji wamekuwa wakibeba mzigo mkubwa kuhakikisha watoto wanapata elimu bora lakini juhudi za wanakijiji zinakatishwa tamaa na hao wasomi kwani wakimaliza masomo yao mchango wao hauonekani kwani wengi hupotelea mijini na kuacha mzigo mzito kwa wananchi ambao hali zao bado ni duni kimaisha
``Tunajitolea nguvu kazi katika shughuli zote za ujenzi, tunafyatua matofali, kugonga kokoto, kusomba mawe na mchanga kwa kuwa vyote vipo kwenye uwezo wetu na hizo rasilimali zipo kijijini, lakini tunakwama hasa panapohitajika matumizi ya fedha kwani uwezo wa wananchi ni mdogo`` aliongeza mwenyekiti huyo
``Tunaomba wasomi waliosoma hapa watusaidie, wananchi watafurahi na wataelewa umuhimu wa elimu, si tu kusubiria wakati wa uchaguzi au wakitaka kuoa au kuolewa wanarudi nyumbani`` alimalizia

Naye diwani Nasaeli Sulle alitoa wito kwa wasomi hasa wanaotoka Haydom kutambua kuwa dhamana ya maendeleo ya Haydom ipo mikoni mwao na kuwaomba wasomi na watu wengine wapenda maendeleo kuunga mkono juhudi za serikali na wananchi katika kuleta maendeleo badala ya kupotelea mijini.

Wakati huo huo, Arthur Awet mkazi wa kijiji cha Rotia wilayi Karatu anayefanya kazi jijini Dar es Salaam, alielezea kusikitishwa na jinsi wasomi wasivyopenda kujitokeza kuchangia maendeleo walikotoka
``Kuna siku nikishirikiana na Paroko wa home tukawataarifu watu waje kwa ajili ya mjadala wa maendeleo ya jamii kule nyumbani ila tuliambulia watu 2 jumla tukawa 4, ny, uhamasishaji zaidi wahitajik`` alisema Arthur


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda