Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, May 4, 2012

Tafakari ya Baba Xtina: Kwa Baraza la mawaziri hili; tusiwe na matarajio makubwa au kidogo!

Baba Xtina, Uholanzi

Kwa Baraza la mawaziri hili; tusiwe na matarajio makubwa au kidogo!
Mheshimiwa Rais kafanya kile ambacho wengi walitarajia na wachache hawakutarajia. Kamwacha Ngellejah (labda baada ya kelele dhidi yake kuongezeka) lakini why Naibu wake Malima hajaachwa?
Uteuzi wa Kagasheki ni SAFI na tu aungwe mkono maana KAGASHEKI ni mtu wazungu wanasema DECENT naibu wake kuna mashaka!
Ujenzi Magufuli kaongezewa nguvu ya Injinia Lwenge maana alikuwa na Lawyer ambaye hakumsaidia sana!!!
Sheria kumrudisha Chikawe ni Weledi maana Chikawe ni Mwanasheria Kombani hajui sheria zaidi ya Adminstrative law!
Mabadiliko ya Ghasia na Mkuchika inaitwa change from 4-4-2 to 5-2-3 maana Ghasia anafiti TAMISEMI swali Mkuchika anafit Utumishi? Kwa seniority sawa kuna katibu mkuu Makini Utumishi anaweza kumsaidia
Lukuvi kubakizwa wizara ile sawa kabisa lakini ingefaa sana kama angepelekwa TAMISEMI he is a man of his own!
Mgimwa ni mchumi na mtaalam wa mambo ya fedha!! Ni uteuzi unaokidhi matakwa ya taaluma!!!! Ni mwanataaluma mzoefu hivyo anajua Theory na Practice manaibu sina cha kuwasemea maana ndo nimewasikia leo!
Mambo ya ndani sawa; lakini kuhama hama kwa Waziri Nchimbi ni kama anaandaliwa kuwa Rais maana kwa kipindi cha miaka 7 ametumikia wizara zaidi ya nne! Zingatia Ulinzi na Mambo ya ndani
Ajira na vijana hakuna tija huko maana yeyote angefaa, burudani Sayansi na Technolojia NAIBU Makamba, kwa vile anayafaham mambo ya technolojia basi tutarajie mambo makubwa!
Uteuzi wa waziri Professa Muhogo Nishati na madini kulitabiriwa na kutarajiwa; Kwa vile ni Professor basi tuamini anaweza kuwa mtendaji kuliko kuwa mwanasiasa ambayo ni sawa kwa Prof Mnyaa, na Prof. Kawambwa!
uchukuzi imekuwa wizara na Mwakyembe kama anahamishwa wizara mama kwenda wizara dada! kwa taaluma yake ya sheria tunategemea miujiza!!!
Sofia Simba na wengine sina maoni! lakini suala la jumla ni kuwa mawaziri wabadilishe utendaji kutoka wa SIASA hadi wa KIMENEJIMENTI!
MUNGU IBARIKI TANZANIA

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda