Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, May 7, 2012

Sumaye: Miaka 10 ya Uwaziri Mkuu na 20 ya Ubunge, Je atakumbukwa kwa yepi hasa nyumbani?

Sumaye akiteta na Sitta
``Nilikuwa sijui kwa nini Tanzania ni maskini`` Kauli ya Sumaye baada ya kutoka kusoma shahada ya Uzamili chuo kikuu cha Havard, Marekani
Nilikuwa nasoma darasa la nne mwaka 1995 katika shule ya Msingi Maretadu Juu wakati Frederick Tluway Sumaye alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nakumbuka wananchi wengi waliusifia uteuzi huo wakiamini kuwa ataitumia nafasi aliyopewa japo kuleta maendeleo siyo tu katika jimbo lake la Hanang, bali pia kwa wilaya zinazopakana mayo.
Mwaka moja baadaye, Sumaye akafanya ziara rasmi katika Wilaya ya Mbulu, nakumbuka tulifanya maandalizi mkubwa ya gwaride la chipukizi, kwaya, usafi na viongozi mbalimbali wa kitaifa walikuwa si haba na alihutubia wananchi wa Maretadu japo mengi aliyoyasema siyakumbuki eidha kwa kuwa hayakuwa na tija au sikuyatilia maanani zaidi ya kutaka kumuona Waziri Mkuu kwa macho yangu ya damu na nyama zaidi ya kumsikia kwenye radio (wakati huo nilikuwa sijui hata TV ni kitu gani)!
Sumaye ambaye pia alikuwa Mbunge wa Hanang toka mwaka 1985 (nikiwa na umri chini ya mwaka moja) hadi mwaka 2005 (nikiwa Chuo Kikuu) baada ya kushindwa king`ang`anyiro cha kuwania kiti cha urais kwa tiketi ya CCM pengine bila kupenda au imani kuwa angeshinda Urais alimwachia Mary Nagu agombee Ubunge jimbomi Hanang. Katika kipindi chote, sijawahi kuona mabadiliko yoyote ya msingi aliyoyafanya, pengine atasema ujenzi wa Zahanati ya Tumaini-Katesh na kuwa barabara ya lami inayojengwa hivi sasa kuunganisha Arusha na Singida vilikuwa kwenye mpango wake! Miaka 10 ya mipango? 

Miaka 20 ya Ubunge, 10 ya Uwaziri Mkuu....Sumaye ameliacha jimbo la Hanang kuwa moja ya majimbo maskini zaidi nchini na hayo yalidhihirishwa na aliyekuwa makamu wa rais ambaye sasa ni rais wa Zanzibar Dr. Shein. Ni aibu iliyoje, japo anadai nyumbani kwake ni Endasak, lakini muda wote aliishi Dar (na Kibaha?), na kama isingekuwa mashamba ya ngano ya NAFCO na Hospitali ya Haydom, wananchi wengi wa wilaya ya Hanang hasa Basotu wasingepata huduma zozote za jamii.
Ni aibu iliyoje, angalia waliokuwa mawaziri wakuu wastaafu walivyoboresha huduma za jamii kwao hasa barabara, Msuya barabara zimeenda hadi milimani, Lowasa nani asiyejua Monduli? Hadi Pinda pamoja na madhaifu yake lakini amepeleka barabara na huduma muhimu kwao Mpanda. Hadi amezidiwa na kina Mramba ambao lami imefika hadi vijijini Rombo lakini yeye kama waziri mkuu ameshindwa kutoa ushawishi serikalini akumbuke alikotoka!
Yumkini alikuwa hajui anachotakiwa kufanya mpaka alipoenda marekani kusoma tena shahada ya pili, pengine hatuna sababu ya kumlaumu kwani si kosa lake, au ni ubinafis na kuyafumbia macho matatizo ya wananchi wake.
mengi yanasemwa kuhusu uhusika wake katika kuyaua mashamba ya ngano ya NAFCO ambayo baada ya kufa bado kuna mgogoro baina ya wawekezaji, wakulima na wafugaji. Akiwa kama mstaafu amekaa pembeni, mbali na waathirika hao huku hatma ya mgogoro huo ikiwa njia panda.

Pengine si Sumaye peke yake, ni kasumba ya viongozi wetu wanaotoka huku ambao hawatumii dhamana zao kuwanufaisha wananchi wa waliowafikisha huko walipo. Marmo miaka 25 ya ubunge na awamu kadhaa za uwaziri lakini hakumbukwi kwa chochote zaidi ya kauli zake za dharauu kuwa ``nitashinda kwa ridhaa ya wajinga wengi na kuwaongoza wasomi wachache`` na kauli nyinginezo nyingi.
Mary Nagu amekuwa waziri kwa muda mwingi lakini nini amefanya cha kukumbukwa? Msindai je? Barabara ni mbovu, huduma za jamii ni duni na viongozi wetu hawaonekani huku kwetu. Pengine yawafaa kusoma alama za nyakati na kujifunza kwa yaliyomkuta Patrick Qorro miaka ile Karatu. Mpaka leo karatu imekuwa mfano wa kuigwa kote nchini, Marmo alipata aibu kutoka kwa walewale aliowaita wajinga na wananchi wa Iramba nao wakamwondoa Msindai Igana izumbe baada ya kuchoshwa na usultani wa miongo mingi:

Sumaye pengine ana ndoto za kugombea urais mwaka 2015, lakini ajue watakaokuwa wa kwanza kumpinga ni watu anaodai ni wa nyumbani kwake japo kiuhalisia ni mgeni huku. Siyo kwa kwamba nabii hakubaliki kwao lakini kwa kuwa hana vigezo. HAJAWA MWAMINIFU KWA KIDOGO, HAWEZI KWA MAKUBWA!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda