Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, May 23, 2012

Step Up ya Papaa Sam Sasali yatinga hadi huku Kwetu

Leo katika makala yake ya kila siku ya jumatano blogger Samuel Sasali kupitia blog yake ya www.samsasali.blogspot.com alifanya mahojiano kwa njia ya simu kutoka Dar es Salaam, akitaka kujua mambo mbalimbali ninayoyafanya huku nilipo. Ohayoda inakuletea jinsi majadiliano hayo yalivyokuwa (au bofya http://samsasali.blogspot.com/2012/05/step-upamani-paul-gaserijogoo-la-mjini.html)

Step Up....Amani Paul Gaseri..Jogoo La Mjini Lililowika Kijijini "Mzee Wa Kambi Popote"

Amani Paul Gaseri.
Kama ulikuwa hujua basi leo wacha nikujuze, Mtu aliyebuni Jina la "Friends On Friday" anaitwa Amani Paul Gaseri, Head Of Technical Department ya Fof Tanzania.

Wakati tulipokutana Kamati ya Maandalizi kubuni Jina la Event yetu, Kila Mtu alikuja na idea yake, wengine wakasema "Business Networking" wengine "Evening Of Happiness" "Usiku Wa Kujiachia" kila mtu na mawazo yake ndipo Amani Paul akasema nadhani tuite "Friends On Friday" Kwa sababu ni Ijumaa inayokutanisha Marafiki, Marafiki zako wanakuwa marafiki zangu, marafiki zangu wanakuwa marafiki zako, kila mtu kwa style hiyo basi tunajikuta tuna Ijumaa Ya Marafiki, Friends On Friday. Kuanzia hapo Jina limekuwa kupita maelezo. Huyu Si Mwingine ila ni Kichwa Cha Ubunifu. Tangu nilipokutana na Amani akiwa UDSM na kuwa nae karibu kwa kazi mbali mbali za Blog niligundua ni hazina kubwa sana katika Taifa la Tanzania. Hatukusita Kumuita kuingia kwenye Kamati ya FoF.
Amani Paul Gaseri Wa Kwanza Kulia akiwa na Team ya Friends On Friday Committee.

Kwa Muda Mrefu Amani amekuwa nje ya Jiji la Dar-es-Salaam tangu alipoaga kuwa anaenda Kijijini mara moja, ghafla amekuwa akifanya kazi kutokea kijijini lakini mambo yanakwenda. Ghafla Amani akaongea na Ze Blogger wazo la Kuwa na Blog, ambayo haikuwa na Mjadala, muda si Muda OHAYODA ikawa hewani.
Amani Paul akitoa mawazo yake Katika Mkutano Mkuu wa Friends On Friday nje ya Jiji la DSM.

Blog ikafanya mawasiliano na Mzee wa Kambi Popote, Amani Paul Gaseri Jogoo la Mjini lililoamua kwenda Kuweki Kijijini Kwao. Na haya ndiyo yakikuwa mahojiano ya Papaa Ze Blogger na Amani Paul Mzee wa Kambi Popote.

Griiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, Ngriiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, Ngriiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii (Muito wa Simu)

Papaa Ze Blogger: Kaka habari Ya Kijijini.

Amani Gaseri: Salama Papaa Za Huko?

Papaa Ze Blogger: Huku Kwema  tu sijui ninyi huko wazee wa Kilimo Kwanza Na Ufugaji?

Amani Gaseri: Mungu Mwema mdogo mdogo siku hazigandi.

Papaa Ze Blogger: Kaka kuna mambo mawili matatu natak kuipasha Jamii kuhusu ulipo sasa na unafanya nini,  Je Kuna Tatizo??

Amani Gaseri: Hakuna Tatizo, twende Kazi.
                                   Amani Paul Wa Kwanza Kushoto akiwa na Team Ya FoF

Papaa Ze Blogger: Napenda kufahamu Majina yako Kamili

Amani Gaseri: Ninaitwa Amani Yesaya Paul Gaseri japo watu mjini wengi hunifahamu kwa jina la Amani Paul, huku nyumbani wengi hunifahamu kama Amani Gaseri ndiyo maana nikabadili jina facebook kuongeza Gaseri ili iwe rahisi kwa watu wa huku kunifahamu

Papaa Ze Blogger: Ooooh twaweza pata Historia yako ya Kielimu??

Amani Gaseri: Nilianza shule ya msingi mwaka 1992 katika shule ya Msingi ENDAHARGHADATK ambako nilisoma hadi darasa la nne nikahamia shule ya msingi MARETADU JUU (zote zipo katika wilaya ya Mbulu) ambako nilimaliza darasa la saba mwaka 1998.

Mwaka 1999 nilijiunga na shule ya Sekondari ya Ilboru iliyopo Arusha ambako nilisoma kidato cha kwanza hadi cha sita nilipohitimu mwaka 2005 na kisha kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia mwaka 2005 hadi 2008 ambako nilipata shahada ya kwanza katika Biashara na Uongozi nikibobea zaidi katika masoko (Bachelor of Commerce in Marketing Management).

Papaa Ze Blogger: Kaka We Kichwa Cha Ukweli, then baada ya Kuhitimu Chuo Kikuu nadhani ukatafuta kazi kama kawaida ya Vijana Wa Kitanzania.

Amani Gaseri: Baada ya kuhitimu nilifanya uamuzi mgumu sana na nikikumbuka huwa nawaza I think I was crazy kuamua kujiajiri moja kwa moja nilipotoka chuo bila kutafuta ajira. Ilikuwa ngumu sana kueleweka hasa kwa familia yangu ukizingatia familia zetu za kiafrika lakini namshukuru Mungu baba yangu alinielewa baadaye na mama mpaka leo hii hanielewi kwani anataka niajiriwe tena ikiwezekana serikalini ili niwe na ``Job security``Niliungana na rafiki zangu Gideon Mugalula na Prosper Mwakitalima tukaanzisha kampuni inayoitwa THE BRIDGE LTD inayotoa huduma za IT hasa katika kutengeneza mifumo ya kompyuta (Software development), iliyoanza from scratch bila kuwa na capital, mtaji mkubwa ukiwa ideas na ujuzi tulionao. I am proud of The Bridge, it was a miracle na hata leo nikiangalia The Bridge ilikotoka na ilipo huwa namshukuru Mungu.Baadaye niliamua kujitoa The Bridge na kufanya kazi ninayoipenda zaidi tangu nikiwa mdogo ya kuwa mwanaHabari (si mwandishi wa habari) ambako ninatengeneza documentary films hasa katika maswala ya utamaduni na historia za jamii mbalimbali
                                         Amani Paul Gaseri akiwa Kijijini hivi Karibuni

 Papaa Ze Blogger: Kwa Kweli ni Changamoto hapo hivi ni Kwanini Ukaamua kwenda huko kwenu na Kutofautiana na Vijana wengi Wanaokimbia Mijini

Amani Gaseri: Huwa nafanya tathmini ya malengo niliyojiwekea kila mara, na baada ya kuishi mjini miaka 4 baada ya kumaliza chuo nilibaini kuwa kuna opportunity kubwa sanakijijini kuliko kubanana mjini. Maisha kijijini hayapo tight kama mjini na kuna stress chachesana. Papaa unajua mjini unapata stress kabla hata haujakutana na stress halisi ya kazi, foleni yenyewe ni stress tosha, kupata nyumba na kero za wenyenyumba na wapangaji wenzako ni stress zaidi, kila siku unawaza kulipa kodi ya nyumba. Lakini kijijini kwanza wasomi ni wachache na kwa kuwa miradi mingi hasa ya utamaduni ipo vijijini siku hizi, inakuwa rahisi kuexploit opportunities zote.Vile vile familia yangu ina assets kama mashamba ambayo yapo idle hakuna wa kuyaexploit, nikaona vi vyema nikarudi kijijini japo nitumie fursa zilizopo huku kuliko kuganga njaa mjini wakati kuna fursa kijijini.
                              Amani Paul akiwa Na huyu jamaa nadhani wa Huko Mbulu.

Papaa Ze Blogger: Wewe kaka Umeamua kujilipua kwa kiasi cha Kijasiriamali, Kwanini Uliamua Kuanzisha Blog tena yenye Mlengo Tofauti na Blog nyingi za Vijana?

Amani Gaseri: Papaa mimi ni mwanaHabari na pia ni mtaalamu wa masoko, ninajua hadhira yangu inahitaji nini na ndio maana nikaanzisha blog maalum kwa ajili ya watu wa huku kijijini. Kwanza kuna habari nyingi sana huku vijijini na pili karibu watu wote waliopo mjini wametokea vijijini lakini hawapati habari zinazohusu huko walikotoka. Hivyo niliona hiyo kama opportunity kubwa kwangu. Blog ni mwanzo tu kaka, lakini lengo ni kuwa na gazeti special la habari za huku, maalum kwa ajili ya mikoa ya manyara na Singida.

Papaa Ze Blogger: Safi Sana..Kuna Mafanikio Yoyote mpaka sasa umeyapata kupitia Blog kwa kuandika story za kwenu

Amani Gaseri: Mafanikio ni makubwa sana papaa, blog hii inawiki tatu tu tangu ianze lakini sasa inawasomaji wanaofikia 5000 na kila siku inazidi kukua, hapo sijaifanyia matangazo yoyote yale lakini wadau wamekuwa wakisambaza ujumbe. Kuna watu kabla hata ya kufungua facebook asubuhi anaanza na ohayoda.

Ninaamini baada ya muda mfupi nitaanza kupata fedha kupitia blog kutokana na matangazo na pia google adsense nao watanikubali muda si mrefu.

Pili taasisi za huku vijijini zikiwemo Halmashauri za wilaya, hospitali na shule mbalimbali wanatambua umuhimu w blog na wameonesha nia ya kutangaza matangazo mbalimbali kupitia blog yangu na wamekuwa wakinipa habari bila tatizo lolote.
Lakini kama nilivyosema nia ni kuwa na gazeti ambalo litaitwa Ohayoda kama blog ilivyo, blog imefanya kazi kama ya Yohana Mbatizaji. Wadau wengi huku Mbulu, Babati, Karatu, Haydom na maeneo ya jirani wanaijua ohayoda na wanasubiri kwa hamu gazeti lianze.

Papaa Ze Blogger: Ukitazama Blog yako Jina lake ni OHAYODA, OHAYODA, OHAYODA je kuna maana yoyote ya kwenye jina?

Amani Gaseri; Jina Blog lina maana, OHAYODA maana yake ya Jumla ni "Yowe" ama "Mbiu", Ukisema OHAYODA, OHAYODA, OHAYODA huku kwetu ni Yowe linapiga kwa Kupokezana, Ni Mbiu inayopigwa kwa kupokezana kutoka kwa Mtu mmoja kwenda kwa Mwingine. Blog hii ni Mbiu ambayo naipiga huku Kwetu Ili Kuvuta At tension ya watu kuwa hata huku Kwetu kuna Utajiri Mkubwa, Mimi Amani nimeanza Kupiga Mbiu hii Kuna Mwingine nae atanipokea kupiga mbiu hii pengine kuna Vijana wengine kama mimi Wataitikia Mbiu hii ya kwenda Kuendeleza Rasilimali zilizopo Vijijini.

So uki click hapa unakuwa unasoma Blog yangu...http://ohayoda.blogspot.com/
Baada ya Kutengeneza Documentary mojawapo ya mambo ya huko kwao Amani aliichukua kazi hiyo na kuipeleka kwa Wazee Wa Kijiji ili Kupata Baraka za Wazee hao. Hapo Laptop imewekwa Juu Ya Jiwe ili watu waone. Si Mchezo Kambi Popote.

Papaa Ze Blogger: Kama ni Creativity hapa Kwako Imelala, niambie jambo moja  Jamii yako inayokuzunguka wanazungumziaje Kazi ya Yako ya blog hasa huko kwenu?

Amani Gaseri: Huwezi kuamini nimepigiwa simu na watu wakubwa wakiwemo wabunge wakisifia sana kazi nayoifanya, nimepata emails na sms nyingi sana wengi wanaikubali sana na kuniunga mkono na wengine wameamua kujitolea kuandika habari na makala mbalimbali, huku kijijini hasa Haydom jamii inajivunia kuwa nab blog yao inayotoa taarifa zinazowahusu tofauti na huko nyuma ambako kila chombo cha habari unachosoma, kusikia au kutazama hakuna habari inayowahusu.Katika kutambua umuhimu wa blog, imekuwa rahisi kupata habari na picha kwa urahisi nyingi wakiniletea wenyewe.

Papaa Ze Blogger: Unawaambiaje Vijana ambao kwao kuna utajiri mwingi sana lakini wapo Mijini na hawana kazi

Amani Gaseri: Kama wanataka mali watayapata shambani. Hahahaaa natania… Tunatofautiana jinsi tunavyoperceive opportunities, lakini ukweli ni kwamba vijijini kuna opportunities ambazo zipo zinasubiri kutumiwa ila hakuna mtumiaji. Kuna fursa kwenye kilimo na hata biashara. Papaa huku kuna watu hawajasoma kivile lakini wametumia nafasi zilizopo, unakuta kwenye taasisi kubwa tu ambayo kwa mjini mhasibu lazima awe graduate na mwenye CPA lakini kwa huku hata mwenye diploma au advance diploma yupo juu sana. Kuna wafanyabiashara wengi sana wanaohitaji ushauri wa biashara na hakuna huduma zozote za kitaaluma lakini vijana wengi wamejikalia mjini huku wakilia hakuna ajira.

Papaa Ze Blogger: Umeamua kurudi Kijijini kuendeleza maisha ama upo kwa muda?

Amani Gaseri: Nimekwepo mjini kwa miaka minne na ile ya chuo jumla miaka 7, huko ninanetwork kubwa sana ila kwa sasa natanua mtandao wangu hadi kijijini, nitakuwa na projects za kijijini na za mjini zaendelea kama kawaida.

 Papaa Ze Blogger: Nini mipango yako ya baadae kupitia Media maana kwa sasa umeanza na Blog what next?

Amani Gaseri: Kama nilivyoeleza hapo awali, mimi ni mwanaHabari na sasa malengo yangu ya muda mrefu ni kuwa na gazeti. Tayari mchakato ushaanza mpaka Julai litakwepo katika mitaa ya Haydom, Mbulu, Karatu, Babati, Katesh, Basotu, Kiomboi, Dareda, Galapo, Dongobesh, Ilongero na Singida.

Papaa Ze Blogger: Any Comment??

Amani Gesari:Papaa sina comment ila nitoe shukrani za dhati kwa Prosper Mwakitalima, my Business Partner na comrade wangu wa ukweli, huwa najifunza mengi toka kwake na huwa ninapotaka kupata ushauri ambao ni ``objective`` yaani siyo emotional he is always the right person, straight, open and clear.He is a true professional, friend and a brother!
Nikushukuru wewe binafsi kwa kunipa nafasi kupitia blog yako, kwa zaidi ya mwaka nilikuwa najifunza mengi kutoka kwako japo wewe ulikuwa haujui ila kwa kiasi kikubwa umeniinfluence sana kuanza na blog.

Papaa napenda kuwashukuru sana Friends on Friday committee, it is a privilege to be part of such a great team. Mama D Irene, Claire, Chris, Jimmy, Anthony and Protace nawshukuru wote.
                                       Amani akiwa ndani a FoF Mtupio Wa Njano

 Kazi Ambazo Papaa Ze Blogger amewahi fanya na Amani akiwa kama Camera Man ni hizi hapa.
Hii Ilikuwa Interview ya Papaa Ze Blogger na Christina Shusho, Amani akiwa Camera Man....At Atriums Hotel.

Hii Ilikuwa mwaka 2010 Wakati Wa Retreat Ya Marafiki Huru Forum at Kawe Beach

3 comments:

 1. ...kaka hii ni zaidi ya "insipiration"...nakubali fikra zako

  ReplyDelete
 2. Mzee Hongera kwa kufanya maamuzi Magumu... na mimi nafikiria hii kitu ya Kuishi Kijijini nihamishie biashara zangu mjini true tumebanana zaidi i kuenjoy maisha tu japo tunatakiwa tusaidie na wenginge vijijini

  ReplyDelete
 3. Papaa Hongera sana Bana.
  I think umeamua kuonesha Mfano kwa wale Tallentors waliozaliwa Vijijini kwetu wakahamia Mjini kwenda Kuwika.
  On My View Its Better to Stay Kijijini na Kufanya kweli. Kwani hata waliokimbilia kuwikia Mjini wanatumia UBONGO tu.
  Tupo Pamoja kwa saaaaanaaaa
  Joshua Bajuta
  EBENEZER STUDIOS-Katesh Manyara
  Bajutageway@gmai.com
  Hot line +255 787 24 24 35, +255 765 44 55 20

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda