Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, May 31, 2012

SINTOFAHAMU:Kwa nini kuna Usiri na Urasimu hata katika kutoa taarifa ambazo hazina usiri wowote?

 Amani ya Mungu ipitayo ufahamu wote iwahifadhi enyi wasomaji wa Ohayoda popote pale mlipo!
Kama kawa kama dawa kama wasemavyo wajuvi wa mambo wa kizazi hiki cha 3G au .com kama siyo cha bongo fleva, leo ni siku moja kabla ya ile siku ambayo wafanyakazi huipenda kama siku ya kupokea mshahara, yaani leo ni siku moja kabla ya "furahiiiiiiday", kitu Alhamisi mwanawani kama ilivyo ada nakuletea SINTOFAHAMU kuhusu mambo ambayo kwa kweli huwa yanaleta ukakasi katika mioyo ya wengi na hakuna pa kutapikia na hapa ndipo mahal pake
Leo ndugu zangu tunaangazia tabia ya viongozi wa taasisi za umma na binafsi, ofisi za serikali na hata watu binafsi kupenda kubania habari au taarifa wakati hizo taarifa zipo kwa ajili ya umma kuufahamu na hakuna madhara yoyote ya kiusalama umma ukiyafahamu.
Mada ya leo imepewa msukumo mkubwa sana kutoka kwa hawa mabwana na mabibi ambao kwa kweli urasimu (bureaucracy) unawasumbua sana hasa linapokuja kwenye suala la takwmimu katika taasisi wanazoziongoza. Kila mara ninapotafuta habari fulani ambayo huwa ni ya ufahamu kwa ajili ya kuwafahamisha wasomaji wangu na nyingine kwa ajili ya afya ya akili yangu, nimekuwa nakumbana na majibu kama
"mimi si msemaji labda uongee na mkuu wangu",
Ninapomtafuta mkuu huyo ninapewa jibu kama hili
"wewe ni nani na kwa nini unataka kujua, kama unataka hizo taarifa andika barua na kisha uje".
Sasa jiulize nilikuwa nataka kujua nini? Hapo nilikuwa nimemwuliza "Naomba kujua kanisa katoliki Mbulu linauwezo wa kuingiza watu wangapi? (capacity). Hilo tu, kitu ambacho hata muumini au kila mtu anahaki ya kufahamu, na kama wewe ni kiongozi unalifahamu kwa kichwa na sioni ubaya wa kutoa taarifa kama hiyo, kuniambia niandike barua kisha nipeleke Mbulu kwa jibu ambalo unaweza kunipa hata kwa SMS ni uwendawazimu, eti mtu anakuuliza "nitajuaje kama unataka kulilipua?" kweli haya ndo mawazo ya hao wakuu? Kwani ukubwa wa kanisa ni siri? SINTOFAHAMU
Jana niliandika makala juu ya uzuri na ukubwa wa kanisa hili, kama jambo la kujivunia kuwepo huku kwetu na wadau wengi walivutiwa sana na wengine wakataka kujua zaidi hasa ukubwa wake maana wapo waliokuwa wanataka kulilinganisha na Efatha au kanisa la Kakobe, nilidhani ni jambo la kujivunia kumbe ni siri....kama kujua idadi ni siri kiasi hicho, vipi nikitaka kujua liligharimu kiasi gani na linaeneo kiasi gani si ntapitishwa mlolongo kama naomba Uraia? Hawaoni kuwa hii inaweza kuwa kivutio hata cha utalii wa kihistoria na wageni wakaja pande hizi?
Si huko tu, nilitaka kujua rate ya maambukizi ya UKIMWI katika wilaya ya Mbulu, nikawasiliana na "anayehusika" na maswala ya UKIMWI wilayani kwani ndiye mratibu wa shughuli zote za wilaya, yaani hata vituo vinavyohusika na UKIMWI hawaruhusiwi kutoa takwimu hata vya vituo vyao mpaka viende kwa mkuu huyo ambaye yeye pia hawezi akakuambia mpaka msemaji mkuu ambaye ni "Mganga Mkuu wa Wilaya".
Sijataka kujua nani ameathirika wala nani anatumia ARV, nataka kujua kasi ya maambukizi na maeneo ambayo yapo kwenye hatari kubwa zaidi, wananchi wanahaki ya kujua na mimi pia kama mwananchi ninahaki achilia mbali haki ya msingi ya kupata na kutoa habari, huko nako naambiwa mpaka barua! Khaa sasa hizo takwmu mnakaa nazo ili iweje? Mnasubiri warsha na tarehe 1 Desemba ndiyo mtoe? Sintofahamu huu mgando wa mawazo mpaka lini!
Sintofahamu kwa nini taasisi nyingi zina mifumo ya habari (Information Systems) tena wanaigharimikia fedha nyingi sana kuiweka na kuwalipa wataalamu fedha nyingi, lakini hizo taarifa hazina msaada kwao na hata kwa wananchi. Kama unabisha nenda kwenye taasisi yoyote omba takwimu kama utazipata kwa wakati, tena baada ya kuandika barua na kupitia kwa watu wengi...khaa udalali mpaka kutoa habari, inakera!
Sintofahamu labda kwa sababu za kiusalama au sijui lakini si amri ya 11 kuwa ukitaka taarifa yeyote polisi lazima msemaji mkuu awe RPC, yaani uhalifu umetokea Haydom au Kiteto na wewe upo hapo unaenda mpaka Babati kwa RPC akupe taarifa! Sijui kwa nini nchi yetu inapenda urasimu kiasi hiki! Kazi ya OCD na OCS ni nini?
Kama hizi taasisi zingetusaidia kuweka habari ambazo kimsingi siyo "CLASSIFIED" yaani hazina madhara kiusalama na si siri, wala tusingesumbuana nao ila kwa kuwa wanaona fahari kuzikumbatia tutasumbuana nao mpaka kieleweke. Inasikitisha mpaka leo taasisi kubwa sana kama Dayosisi, Hospitali na hata vyuo havina tovuti, na hata kwa zenye hizo tovuti haupati habari yoyote yenye manufaa! Kama unabisha niambie kama Halmashauri zote za wilaya, ELCT Dayosisi ya Mbulu, Jimbo Katoliki Mbulu, Vyuo vyote (vilivyopo Manyara na Singida), Haydom Lutheran Hospital n.k kama zinatovuti! Na kama zinazo wameweka habari gani humo?
Leo hii ukitaka kujua historia ya taasisi husika hauwezi kuipata kwa sababu tu wanaona fahari uwanyenyekee kwa kuandika barua na kuweka "appointments" ili uweze kuzipata. Usije ukalogwa ukataka kujua idadi ya wafanyakazi na taaluma zao, usije ukathubutu kuuliza wanalipa kodi kiasi gani wala mapato yao ni kiasi gani wakati kiuhalisia na hata sheria (statutory) inawataka watoe taarifa haza za mahesabu yao ya fedha na kuziweka hadharani.
Usiri mwingine hauna tija, hasa kwa dunia ya leo ambayo inatawaliwa na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, utabana hapa kwingine habari zitapatikana..tena afadhali utoe habari ili ipokelewe na kukupa sura nzuri kuliko kuibania kwani ikishapatikana haitaku"feva" wewe. Hakuna siri duniani, kama za usalama wa taifa zinavuja sembuse za taasisi ambazo zenyewe tu zinaendeshwa kwa majungu na umbea?
Aidha ntakuwa si muungwana kama nisipowapongeza viongozi wa ngazi za chini hasa vijijini ambao kwao "protokali" si ishu sana, hawaoni tabu kukupa takwimu na taarifa hasa maeneo wanayoongoza lakini kosea ukaenda ngazi za juu, urasimu hadi kero jibu ni "andika barua".
Sintofahanu usiri huu na urasimu huu utaendelea mpaka lini lakini ninaimani kuwa hautadumu sana kwani kwa spidi ya teknolojia ilivyo havitadumu. Ni bora kubadilika mapema na kuanza kukubaliana na hali halisi kuwa kupata habari na kutoa habari ni haki ya msingi ya kila mtu. Mkuu wa kaya mwenyewe kule magogoni hafichi habari tena anawaita waandishi wa habari sasa wewe ndugu yangu na mimi unajifanya mkali kuliko mwenyenyumba nashindwa kukuelewa!
Ushauri wa bwerereeeeee kwa wahusika, wekeni mifumo mizuri ya kutoa na kupokea habari kwa umma ili kujijengea taswira nzuri siyo tu kwa umma bali pia kwa wafanyakazi na hata wanaotaka kuwekeza kwenu! Nimesema kutoa na kupokea habari, nikifika hapa natoa wito maalumu kwa Taasisi zote ziwe na utaratibu wa kukusanya maoni ya wateja na hata wafanyakazi wao maana taasisi nyingi zinaamini mambo yapo shwari kumbe yashavurugika wakati viongozi wapo fofofoooo! Nadhani hapa wahusika mmeshanielewa sitaki kwenda kwenye mifano hai!No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda