Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, May 23, 2012

Shujaa Wetu: Walimu wote wa darasa la kwanza

Ni Jumatano nyingine na siku zazidi kuyoyoma kama mshahara! Lady Jay Dee aliimba siku hazigandi na kweli zinakimbia utadhani mgonjwa wa kipindupindu anavyoendesha! Kama kawa kama dawa, leo twatupia macho yetu kuwatambua wale watu mbalimbali katika jamii yetu, walio hai na wafu ambao kwa namna moja au nyingine wamefanya kitu cha kukumbukwa katika jamii yetu, yaani wameacha "foot prints" katika mioyo yetu na ni vyema tuutambue mchango wao ili uwe hamasa kwetu kufanya mazuri kama wao.
Nakumbuka wakati naenda kujiandikisha kuanza shule ya msingi mwaka 1991 nilikutana na watoto wenzangu enzi hizo, leo nikiangalia wengi wetu tulipo na tulivyo na nikilinganisha na enzi hizo najiuliza maswali mengi, moja kubwa huwa ni "Je tunawakumbuka walimu wetu hasa wale wa darasa la kwanza waliotufundisha kusoma na kuandika?

Wengi wetu hatukusoma kwenye shule za "chekechea" na tuliosoma shule za msingi tofauti na waliosoma shule za "St. School Bus" na walimu hawa wa darasa la kwanza walikuwa na shughuli pevu ya kututoa ujinga. Inahitaji moyo kumfundisha mtu ambaye hajui kitu kabisa, mwingine hajui hata lugha unayoitumia kufundishia, unaanza kwanza kumwelekeza Kiiraqw au kinyiramba ndo tafsiri kwa kiswahili kisha aanze kuelewa. Hata kama nalipwa mshahara kiasi gani siwezi kuifanya...tuwaachie wenye huo wito kwa kweli
Embu kumbuka enzi hizo unafika shule? Unafuta makamasi mashavuni? Wengine hata matumizi ya choo hawakuwa wanayaweza badala yake walikuwa wanajisaidia kwenye nguo lakini inahitaji kuwa na moyo mgumu kama paka kuweza kuvumilia yote na hatimaye kutoa wataalamu ambao wengi wetu leo tunaringa lakini hatukumbuki tumetoka wapi. 
aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!
iiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!
oooooooooooooooooooo
uuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!
Hawa walimu kwanza walitufundisha tuipende shule, kupitia nyimbo na upendo mkubwa waliokuwa wanatuonesha, hata adhabu za fimbo enzi zile kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili zilikuwa adimu sana ili tu uweze kupenda shule. Walimu hawa walicheza na kuimba na watoto, hapa namkumbuka mwalimu Denis Amsi, Mwalimu Agnes Karengi, Mwalimu Magdalena Koppa, Mwalimu Samweli Sarya, Mama Trophim, Mwalimu Gewe na walimu woooooooote ambao walifanya kazi ya walimu wengine wa madarasa ya juu iwe rahisi sana kwani hawa walikuwa wanapokea wanafunzi wanaojua kusoma na kuandika. Lakini kama ilivyoada ya binadamu, sifa zote wanachukua walimu wa darasa la saba na hata hao wanafunzi huwa hawakumbuki waliowawezesha wao kujua kusoma na kuandika.
Borghild Evjen Olsen akifundisha kuandika na ususi 
Hapa namkumbuka pia Borghild Evjen Olsen, mke wa Dr. Olav Olsen wakati wanafika hapa Haydom miaka ya mwanzo ya 1950 na kuanza kufundisha watu siyo kusoma na kuandika tu, bali hata kuvaa nguo. 
Lakini Mungu si Akona/ay bwana, hawa walimu huwa hawazeeki, wapo vile vile! Unabisha? Nenda kamwangalie mama Karengi au nenda mpaka Maretadu juu umkute mama Trophim, au nenda Endagaw utamkuta mwalimu Christina Joseph toka Kilamatembo hadi Endagaew, toka nipo shule ya msingi wapo vile vile! Tunawakuta na kuwaacha wao wanapeta!
Big up kwa walimu woooote wa darasa la kwanza, hasa mama yangu japo nilijifunza mwenyewe kusoma na kuandika kabla sijaanza shule kutokana na kukulia mazingira ya shuleni, lakini mchango wake kamwa hautasahalika hasa kwa wote waliosoma shule ya msingi Endaharghdatk!
"Hesabu ni nzuri sana weee X2 
Mwalimu nifundishe, siwezi kusahau ee mwalimu ee mwalimu nifundisheeeeeeeee"

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda