Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, May 30, 2012

Shujaa wetu: Franz Wesinger-Mhandisi aliyejenga kanisa Katoliki Mbulu

  • Ujenzi ulianza bila fedha wala vifaa
  • Baada ya ujenzi yabaki kontena 12 zikiwa na vifaa, majukwaa, magari n.k

Duh kumbe leo ni Jumatano? Muda unavyokimbia utadhani siku ina saa 22 siku hizi...kwanza kabisa napenda kuwaomba radhi wapenzi wasomaji wa ohayoda kwa kuchelewa kuileta mada yetu ya kila siku ya jumatano ya Shujaa Wetu ambapo tunapaa fursa ya kutambua mchango wa mtu au watu mbalimbali ambao wamefanya jambo lolote lenye manufaa kwa jamii au hata kuiletea jamii yetu sifa au pengine mafanikio yao binafsi ambayo ya nafaa kuigwa na jamii nzima.
Je wamfahamu mtu aliyejenga kanisa kubwa kuliko yote Tanzania na la pili kwa ukubwa Afrika Mashariki?
Huyu si mwingine bali ni Mhandisi Franz Wesinger aliyezaliwa mwaka 1928 huko Bavaria Ujerumani.
Mwaka 2003, akiwa na miaka 75 mhandisi Franz Wesinger ambaye pia ni msanifu wa majengo alirudi Tanzania kwa ajili ya kupanga ujenzi wa kanisa jipya la Katoliki Arusha na ni katika kipindi hicho ambacho mapadre wawili wa kanisa Katoliki jimbo la Mbulu walikumbwa na kashfa ya ufisadi kama baada ya kufuja jumla ya Shilingi za Kitanzania Milioni 340 kwa bei ya 1000 kubadili dola moja wakati huo  (dola 340,000). Mapadre hao, msaidizi wa askofu (Vicar General) John Nada na father Melkiadus Qameyu wa parokia ya Dareda walituhumiwa kupoteza kiasi hicho cha fedha baada ya kutapeliwa na mganga wa kienyeji aliyefahamika kwa jina la Mohamed mrisho kuwa angeziongeza mara mbili....mafaza wakaingia mkenge...
Turudi kwa Franz Wesinger, huyu bwana alifanya mahojiano na gazeti la Arusha Times mwaka 2003 na haya ni sehemu ya maelezo yake kuhusu ujenzi wa Kanisa hilo
"Katika miaka 15 iliyopita, Jimbo la Mbulu limepiga hatua kubwa sana. Jitihada za awali za marehemu Askofu Hhando zimezaa matunda kwani walianza kidogo au kusema ukweli halisia walianza bila fedha lakini waliweka imani yao kwa Mungu huku wakitumia msaada kidogo kutoka kwa wamihionari kutoka Ulaya na ujenzi ulianza. Amini usiamini, walianza ujenzi wakitumia sepetu lililovunjika na toroli la mbao. Kanuni kuu ilikuwa kubana matumizi na kuhudumu (huduma) pamoja kukawa kichocheo kikubwa katika jimbo zima kumtumikia Mungu" alisema Franz
"Hata baada ya ujenzi na kanisa kuwekwa wakfu zilibaki kontena 12 zikiwa zimejaa vifaa vya ujenzi, mashine, magenerata, jukwaa kubwa, magari mawili na lifti (cranes) bila kutumika"
"Kuna tofauti kati kuhudumu kwa imani na kutumaini kupata faida pasipo kufanya kazi" aliongeza Franz akizungumzia ufisadi uliotokea Mwaka moja baada ya ujenzi wa kanisa hilo kukamilika.
"Hata wana wa Israeli walimsahau Mungu na kuabudu ndama wa dhahabu baada ya Mungu kuwatoa utumwani mwa Wamisri na kuwapitisha katika bahari ya Shamu"
"Waisraeli walikombolewa lakini walitaka kupata faida pasipo kufanya kazi, hauwezi kumtumikia Mungu kwa ulanguzi"
Franz Wesinger alieleza kuwa anajisikia fahari kubwa sana moja ya sehemu maskini zaidi Tanzania ina Kanisa kubwa zaidi na zuri zaidi nchini na kuona fahari kuwa imejenga hilo kanisa lenyewe kwa msaada pekee wa Mungu"
Chini ya usimamizi wa Franz Wesinger ujenzi wa kanisa hili ambalo leo ni fahari kubwa kwetu ulikamilika kwa ufanisi wa hali ya juu na kutimiza ndoto ya aliyekuwa Askofu wa Jimbo Kuu la Mbulu Marehemu Hhando. Franz Wesinger anatoa funzo la uaminifu na kuacha "legacy" kwa vizazi vijavyo. Sina uhakika kama bado yupo hai lakini Franz Wesinger alifanya kazi kubwa sana tofauti na "wahandisi" wetu ambao ninauhakika kisingebaki kitu baada ya ujenzi na katu kazi ya ujenzi wa kanisa hilo usingekamilika.
Kwa ufahamu tu: Franz Wesinger ndiye aliyejenga pia Kanisa kuu Katoliki la Arusha 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda