Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, May 16, 2012

Shujaa Wetu: Flatei Gregory Massay wa Tumaini Group-Mbulu

 • Alianzisha Kikundi akiwa na miaka 14
 • Alianza kucheza sarakasi akiwa na miaka 6
 • Kimetoa ajira kwa vijana 35
Kama ilivyoada, kila siku ya Jumatano, Ohayoda inatoa fursa kwa jamii kutambua mchango wa mtu au kikundi cha watu katika jamii yetu. Mchango huo unaweza kuwa mafanikio yake binafsi ambayo yameiletea jamii yetu heshima au amefanya jambo lolote la kishujaa ambalo linastahili kuigwa na jamii nzima.
Human pyramid in from of the norwegian parliament, Oslo
Tumaini Group katika moja ya Tour Ulaya
Leo Ohayoda inaangazia macho mchango wa Flatei Gregory Massay wa Mbulu, ambaye kwa sasa ni Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbulu, siyo kwamba yeye ni shujaa kwa kuwa katibu mwenezi wa chama hicho tawala bali kwa mambo aliyoyafanya kabla hata hajaingia kwenye ulingo wa siasa akiwa na kikundi chake cha sana kiitwacho ``Tumaini Group`` chenye makazi yake mjini Mbulu.
Flatei ni moja kati ya watu wachache wenye vipaji vya hali ya juu kuwahi kutokea katika wilaya ya Mbulu na hata mkoa wa Manyara kwa ujumla, akidhihirisha vipaji tofauti katika sanaa, ubunifu na hata uongozi uliothabiti, toka kuongoza kikundi alichokianzisha akiwa na umri wa miaka 14 hadi kuwa katibu mwenezi wa chama. 
Juma on his belly with his feet on his head.
From Barabaig! in Olavshallen, Trondheim.
Photo: Carl-Erik Eriksson


Flatei Gregory Massay au Flatei si jina geni kama linavyofahamika na wengi katika wilaya ya Mbulu na wilaya za jirani. Umaarufu wake unatokana na kuanzisha kikundi cha sanaa kinachoitwa Tumaini Group mwaka 1986 akiwa na umri wa miaka 14 tu. Flatei aliyeanza kucheza sarakasi akiwa na miaka 6 ilifika wakati alikuwa akimdanganya mama yake ili ampe ruhusu akecheze sarakasi mjini Arusha takribani kilometa 250 kutoka Mbulu.
Toka kuanzishwa kwake, Tumaini Group imekuwa ikifanya siyo tu shughuli za sanaa bali pia kama kikundi cha kuelimisha jamii na kuwapa watoto hasa wanaotoka katika familia maskini fursa ya kunufaika kutokana na vipaji vyao na pia kutoa burudani kwa jamii.
Kikundi cha Tumaini mpaka sasa kinaundwa na wasanii wapatao 35 wenye umri kuanzia miaka 6 hadi 39 ambao wamekuwa wakitoa burudani katika sehemu mbalimbali wilayani Mbulu na hata sehemu nyingine ndani na nje ya nchi yetu ambako kote walikopita wameweza kuteka na kukonga mioyo ya mashabiki wao.
Boys stretching.

From physical exercise with children in Tumaini Group
Photo: Elin Hassel Iversen
Ingawa Tanzania ni mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani na kwa kuwa wasanii wengi wa Tumaini Group hutoka katika familia maskini, Tumaini Group linawapa vijana hao fursa ya mafunzo ya sanaa mara tano kwa juma, mafunzo ambayo huwaweka kuwa na uwezo wa hali ya juu kutoa burudani na kuelimisha mashabiki wao.
Uongozi madhubuti wa Flatei na Lucian Theobald Ngaire umekiwezesha kikundi hiki kudumu kwa muda mrefu na kuweza kuhimili changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa weledi wa hali ya juu. Chini ya uongozi wao, kila msanii hufunzwa majukumu tofauti katika kikundi ili kuwapa uwezo wa kuchukua nafasi yoyote ile hata pale aliyepewa jukumu hilo anapokosekana.
Flatey trains acrobatics
Flatei practice actobatic throws
Photo: Audun Eriksen

Kikundi hiki kimekuwa na mafanikio ya hali ya juu kwani kimeshinda tuzo mbalimbali ndani na nje ya nchi yetu. Kila mahali wanapofika hukutana na mashabiki wanao``pagawa`` na ``show`` wanazofanya. Iwe sarakasi, uigizaji au ngoma za asili, Tumaini Group wameweza kukonga nyoyo za mashabiki wao vilivyo.
Kikundi hicho kinaamini kuwa uboreshaji wa shughuli za sanaa na ubunifu ni msingi wa kutoa huduma bora za sanaa na zenye kuendana na nyakati na mazingira husika.
Flatei na Tumaini Group pamoja na mafanikio makubwa waliyonayo wameamua kujikita Mbulu ili kuwapa wananchi wa Mbulu na maeneo ya jirani burudani na pia kuwaelimisha. Pengine kikundi hiki kingeweza kupata mafanikio makubwa kwa kujikita maeneo ya mijini zaidi kama Arusha na Dar es Salaam kama vinavyofanya vikundi vingine vya sanaa na wasnii mbalimbali lakini wame``sacrifice`` mafanikio binafsi na kuiweka jamii yao mbele, jamii ambayo imewatoa wao na kutoa kama ``shukrani`` kwa jamii. Mara nyingi huwa nafikiria kuhusu kikundi hiki na namna ambavyo hakipati sifa inayostahili, nadhani ni wakati muafaka kuuenzi mchango wa kikundi hiki na hasa wa Flatei Gregory Massay kwa heshima kubwa aliyotuletea, kuanzisha kikundi akiwa na miaka 14 na kudumu mpaka leo ni mafanikio tosha. Tusisubiri hadi mtu afe ndipo tuthamini mchango wake, kwa hili Flatei, Lucian na kikundi kizima cha Tumaini wanastahili pongezi na heshima.
Ohayoda linapenda kukupongeza kwa juhudi zako na kukupa heshima ya kuwa Shujaa wetu wa wiki ya pili toka kuanzishwa kwa makala hii maridhawa. Hongera sana Flatei na Tumaini Group

Kwa habari zaidi kuhusu Tumaini Group tembelea
www.tumainigroup.comPhoto: Audun Eriksen

1 comment:

 1. Hongera sana Flatei .. nashukuru kusikia ya kwamba bado unaendelea kufundisha sarakasi.. inapendeza kuwa na watu kama wewe kwenye jamii yetu.

  Nakumbuka kipindi kile miaka ya 1996 na kuendelea ulikuwa pale kwa DOMINIKI HAYDOM KUFUNDISHA SARAKASI na kuonyesha michezo ya sarakasi.. dahhh umetoka mbali sana..

  nashukuru Ohayoda blogspot kwa kukupaisha unastahili kwa kweli...
  Kila lakheri na unachofanya maishani.. Mwenyenzi Mungu akulinde na kukuongezea baraka zake kwa wingi... Keep up great work. :)

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda