Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, May 30, 2012

Shughuli ya upigaji picha kwa ajili ya Datoga Documentary Film

Baada ya kukamilisha kutengeneza filamu inayowatambulisha Wairaqw, shughuli ya kutengeneza filamu itakayowatambulisha Wadatoga ilianza. Leo tulikuwa ``location`` kuchukua baadhi ya scene kwa ajili ya filamu hiyo itakayokamilika mwishoni mwa mwezi Juni na kuwa mitaani pamoja na ile ya Wairaqw. Scene ya leo inahusu mazishi ya watu maarufu wa kabila la Wadatoga yanayofahamika kama Bung`eda ambapo huchukua mpaka muda wa mwaka mzima. Bung`eda hii itahitimishwa mnamo tarehe 17 Juni na huu ukiwa ndio mwezi wa mwisho wa shughuli hiyo maandalizi ya sherehe ya bung`eda yalikuwa yamepamba moto na wageni kutoka sehemu mbalimbali walikuwa wameanza kuwasili na shughuli za ujenzi zipo katika hatua ya mwisho. Ohayoda itakuletea katika makala maalum kuhusu Bung`eda.
 Jua likanza kuchomoza, hapa ni ziwa Basotu na nyuma ni mlima Hanang
 Kwa imani ya wadatoga, ghuta Salahod ambapo mapacha wawili (salahod) wa Asseta (Mungu wa Kidatoga) walitokea hapa ziwa Basotu na pia wanaishi katika vilele viwili vya mlima Hanang
 Kina mama wakiimba nyimbo za kuamsha ``mizimu`` asubuhi
 Ilibidi tupozi kupiga nao picha pamoja na wenyeji baada ya zoezi la kuchukua hio nyimbo za kuamsha hao ``waliolala``
 Pascal naye alijichanganya
 Gunners inamashabiki hadi huku, hawa machalii ni manazi wakubwa wa Arsenal Kwa hapo nyuma hilo ndilo kaburi ama Bung`eda, ambapo marehemu anazikwa kwa kukalishwa na kujengewa kama inavyoonekana
 Pascal akiwa katika shughuli

 Hapo nyuma ni nyumba zinazojengwa kwa ajili ya kuwapokea wageni watakaokuja kwenye sherehe ya Bung`eda


 Mlima Hanang wenye urefu wa meta 3418 ndio mlima wa 3 kwa urefu nchini, je wadau tunalifahamu hilo? Hapa ndipo wadatoga wanaamini Salahoda Asseta wanapoishi (Mapacha wa Mungu)
 Ndege wa kuvutia katika ziwa Basotu
 Ziwa Gidamunyoda ambalo ni la kreta (Crater lake) limetenganishwa na barabara na Ziwa Basotu lakini ajabu ni kuwa maji yake ni ya chumvi wakati ya ziwa Basotu ni baridi (fresh)

 Ziwa Basotu, Hanang
Mlima Hanang kwa mbali 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda