Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, May 11, 2012

Semina ya IMCI yafanyika Haydom

Mradi wa Afya ya Msingi Mbulu (Primary Health Care Mbulu-PHCM) uliochini ya Kanisa Katoliki jimbo la Mbulu kwa kushirikiana na Shirika la SOLIDARMED ya Uswisi wanaendesha semina ya magonjwa ya watoto IMCI yaani Integrated Management Childhood Illness inayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya IM iliyopo Haydom na kisha kufanya mafunzo kwa vitendo katika Hospitali ya Kilutheri ya Haydom kwenye wodi ya watoto (LENA Ward) na RCH.
Semina hiyo inayofanyika mara moja kwa mwaka, huu ukiwa mwaka wa tatu toka ianze mwaka 2010, ilianza rasmi tarehe 07 mwezi Mei na inatarajia kukamilika tarehe 18 mwezi huu. Akizungumza na Ohayoda baada ya semina jana jioni, mratibu wa semina hiyo ndugu Stanslaus Herman maarufu kama Koski alieleza kuwa, semina hii inawahusu wauguzi na madaktari kutoka katika zahanati mbalimbali za wilaya ya mbulu ili waweze kukabiliana na magonjwa haya ya watoto.
``IMCI hufanyika kwa awamu moja kila mwaka, na kila awamu huwa na washiriki wasiozidi 16 ambau hupata mafunzo kwa siku 11 na kisha baada ya semina huenda kuyafanyia kazi waliyofundisha ili kupunguza vifo vya watoto waliochini ya miaka 5`` alisema Koski
Semina hii imeandaliwa na Edward Mwisana ambaye ndiye IMCI Focal person wa wilaya na wakufunzi wa semina ni Dr. Nyamgondo Marwa kutoka hospitali ya wailaya ya Arumeru, Dr. Wilfred Sungura kutoka hospitali ya wilaya ya Monduli na Mganga mkuu wa wilaya ya Mbulu (DMO) Hassan Mataka.OMBI: Usiache kupigia kura swali letu la wiki hii lililopo upande wa juu kulia wa blog hii

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda