Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, May 22, 2012

Papaa On Tuesday……Kukua Sio Miaka Ila Maamuzi.


Kama kawaida siku ya Jumanne naungana na blogger Samuel Sasali kupitia blog yake ya http://samsasali.blogspot.com/ kukuletea makala ya Papaa On Tuesday anapozungumzia masuala mbalimbali ya maisha. Leo Papaa anasema ``KUKUA SIYO MIAKA ILA NI MAAMUZI``
Ninawasalimu kupitia jina la Bwana Wetu Yesu Kristo. Ninakila sababu ya Kumshukuru Mungu weekend hii nilikuwa na muda Mzuri na Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Ardhi, Jumapili nikawa kwenye Kanisa moja huko Mbezi Luis, Weekend hii Jumamosi nitakuwa kwenye “Worship Experience Competition” na Jumamosi hiyo hiyo nitakuwa Mabibo Fellowship na Jumapili kama kawaida nitakuwa kwenye Performance na “Move”.Kwenye Biblia kuna habari ya mtu aliyeamua kufanya Maamuzi mbele za Watu, zipo stori nyingi lakini bwana mmoja kwenye Biblia akatangaza mbele za Watu. "Chagueni hivi leo, Mtakaye Mtumikia" huwezi kusema haya mameno kama watu unawaelewa fika, aliwaambia haya maneno sababu hawa watu wanashindwa kufanya mamuzi, akawapa mtihani rahisi. Lakini yeye kuoneonesha Ukomavu wa kimaamuzi akatangaza hadharani "Mimi na Nyumba Yangu Tutamtumikia Bwana". Saa ngapi amekaa na familia kijadiliana nayo??lakini akatangaza hadharani haya ndo maamuzi ya "nyumba yangu". Alikuwa so straight haina kuuma uma maneno.

Kwa maisha yetu ya kila siku nimewahi jiuliza hivi ni lini unajijua unakuwa mkubwa??kila siku kuna mtu anasheherekea “birthday” yake. Yaani kwa maana nyingine ni kwamba kila siku kuna mtu anakuwa mkubwa lakini wengi wetu zinaongezeka tu miaka lakini matendo yale yale. Lini uliwahi umeshakuwa mkubwa??
Kuna watu tumewahi waona wanamiaka ya kutosha tu lakini wamekuwa wakifanya mambo ya kitoto, na kuna watoto tumewahi waona ama wasikia wakiamua mambo ya kiutu uzima sana.
Lazima kizazi hiki kijifunze kufanya maamuzi, hata kama ni magumu kiasi gani lakini umeamua, kuto kufanya maamuzi na kwenyewe ni maamuzi lakini yanakugharimu zaidi.

Katika Kufanya maamuzi kuna watu wa aina nyingi lakini tunaweza kuyaweka katika makundi makubwa matatu.

Kundi la Kwanza ni lile lililojaaliwa kuweza kufanya maamuzi kwenye maisha yao. Wanachokipanga ndicho wanachokifanya. Wao huwa hawahesabu kufanya maamuzi kuna gharama sana kuliko kuto kufanya. Haijalishi maamuzi hayo yatamgharimu kiasi gani lakini ili awe na amani lazima aamue. Wako So straight. Kama kuna kitu hataki hana haja ya kuremba anakuambia Sitaki A, B, C. Kama kuna mkaka ama mdada anamfuatilia hana muda wa kukopesha, hata kama itaharibu urafiki wao lakini mapemaaaa anakuwa wazi kwako kuwa huo upande mimi sipo kabisa, ukiwambia twende dinner sijui kwenye send off anakuambia kabisa sina muda huo. Group hili huwa hawa entertain kitu wasichokitaka. Kama hataki muwazi kama anataka ni muwazi pia. Kama mmekubaliana kuwa akikukopesha ukasema  utalipa tarehe 8 nakuambia utalipa tarehe 8, Ukisema Kikao kitaisha saa 9 kama hujamaliza basi. Wako So Open na maamuzi yao. Kama Hawezi kukuchangia hakuambiii nitaangalia, no anakuambia SINA HELA, ama SITAKI. Ingawa maamuzi yao hupelekea watu wengi kuwatenge kama sio kuwaogopa lakini huwa ninawependa watu hawa sababu KWELI yake ni Kweli na Haina Hila ndani yake. Unaweza kuta mtu ana umri Mkubwa tu lakini hawezi kusimamia hata maneno yake mwenyewe. Hawezi kutunza Promise aliyoiweka yeye mwenyewe. Kuna watu wamekuwa mizigo kwa wengine kutokana na maamuzi yao ya Kitoto Watu Serious hawawezi fanya kazi na watu wasio jitambua tambua. Kama Umesikia kuna watu wanamsema vibaya kwanini usimtafute huyo mtu mkaongea. Kuna marafiki zangu wengi sana wamewahi kunitafuta sababu wanasikia A, B,C tukakaa chini na kuyamaliza utoto huleta athari kubwa sana kwenye makuzi ya kila siku.

Kundi la Pili la Watu ambao wao huchelewa kufanya maamuzi, ni kweli wanafanya maamuzi lakini maamuzi yao either hugharimu maisha yao ama maisha yaw engine. Kuna wengine wanafanya hivi sababu wanakuwa hawana uhakika, kuna wengine wanafanya hivi sababu wanafaidika na kuto kufanya maamuzi, na kuna wengine wanachelewa kufanya maamuzi sababu ya Upendo na kuna wengine wanachelewa kufanya sababu yak u entertain kile kilichopo sababu kinakuwa hakijamfunga sababu kwa kinywa anakuwa hajatamaka ingawa matendo yanaonesha kama yuko katika hilo. Unaweza kuta kuna mkaka anampenda sana mdada na mdada pengine anampenda mkaka lakini mkaka na muda mwingi pengine wako pamoja utadhani wana uhusiano lakini ajabu Mkaka hajawahi kutamka neno kuwa anampenda mdada. Mwisho wa siki mdada anakuwa haelewi kinachoendelea mwisho unakuta mdada anaolewa na mtu mwingine na Mkaka anadai ameumizwa au ameachwa, hivi huyu ameumizwa ama amejiumiza??Kuchelewa kufanya maamuzi wakati mwingine huchelewesha mambo mengi sana ya maendeleo. Mara ngapi umewahi kukosa deal sababu ya kuchelewa kufanya maamuzi. Kuna wengine wamewahi kukosa kazi sababu saa aliyokuja kuamua it was too late. Kama unaweza amua leo usingoje kesho. Kama jambo unachelewa kuliamua basi liwe na sababu maalum lakini sio tabia ya kuchelewa kuamua. Nimewahi ona mdada ambaye alipendwa sana na mkaka, mkaka was full committed utadhani kafanyiwa maombi ya zindiko, hakuna ambacho mdada alitaka hata kwa utani jamaa asifanye, jamaa alijinyima kwa ajili yam dada, kumbe mdada alikuwa anashindwa kuamua kwa sababu zake binafsi, mwisho wa siku Mkaka akaona hapo hakuna cha kuendelea kusubiri na kutafuta mwenzi mwingine, wakati mkaka ameamua kugeukia mambo yake ndipo huyu mdada akawa yuko tayari, Yule kaka aliamua kuendelea na maamuzi yake ya kupenda atakakopendwa nay eye sio hii ya kucheleweshana. Kwa kuchelewa kuamua kwa sababu moja ama nyingine Relationships nyingi sana za Kibongo zimekuwa na mautata mengiiii sana. Wengine wamechelewa kuoa ama kuolewa sababu walipotakiwa kufanya maamuzi walichelewa kufanya maamuzi.

Kundi lingine la watu ni lile ambalo wao hawawezi kufanya maamuzi, ingawa kushindwa kufanya uamuzi na wenyewe ni uamuzi lakini hawa wanaogopa kuwaumiza wengine pale wanapohisi wakifanya maamuzi watawaumiza wengine. Utakuta hawa situ wanachelewa ila hawawezi kuamua hata kama wanateseka wanataka kuonekana wako pouwa huku wanaumwa. Kuchelewa kufanga maamuzi ama kushindwa kufanya maamuzi kumesababibisha wengine kuteseka kwenye maisha yao. Utasikia mtu anasema “Mi Siwezi Mwambia”, “We Mwache tu, lakini siwezi Mkatalia”. Mtu huyu akikutana na watu wa kundi la kwanza wanashangaa inakuaje unashindwa kuamua??Maisha ndivyo ya livyo wengi wamekuwa kwenye kifungo watu wa kundi hili sababu kubwa hawawezi kufanya maamuzi. Wanavumilia kuteseka lakini kwa vinywa vyao hawawezi. Kuna wengine wamefanyiwa hadi visa lakini wamo tu.

Umri unasonga kuna  mambo kwenye maisha ni vema tukajifunza kufanya maamuzi, nimewahi kuandika kuhusu kufanya maamuzi magumu, kama hukusoma gonga hapo.
Mungu akusaidie kuona wewe uko kwenye kundi gani la kwenye maisha.

Papaa
0713 494110.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda