Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, May 29, 2012

Papaa On Tuesday....Kila Likuepukalo Lina Heri Nawe

Nimatumaini yangu ya kuwa tu wazima na tunaendelea vema na shughuli za ujenzi wa Taifa letu la Tanzania. Ninatoa pole za dhati kwa ndugu zetu wa Zanzibar katika kipindi hiki chenye hali tete ya amani, tunaamini Mungu ni Mwaminifu sana kwenye Maisha ya Kila siku. Kama uko tayari kuungana na blog hii kuwa support watu wa Zanzibar Please click here ...http://samsasali.blogspot.com/2012/05/harambee-kwa-ajili-ya-ku-support-ujenzi.html

Kati ya mambo ambayo kwenye maisha limekuwa ni changamoto kila iitwapo leo basi "Kupoteza", "Kukosa", "to loose" ni kitu ambacho kwa kweli kimekuwa changamoto. Katika Kizazi hiki ambacho hakina subira na uwezo wa kujitafutia wenyewe, mtu akikosa anaona kama maisha yamefika mwisho.

Kama kuna deal mtu anafukuzia raha yake apate, akikosa mwingine mpaka anaumwa, kuna mwingine anampenda mtu mpaka basi lakini ajabu baada ya muda watu wanamwagana, juzi kati nimesikia mpaka kuna mdada amekuwa chizi kabisa sababu kuna mkaka amemwacha na huyo mdada anampenda sana huyo mkaka kuliko pengine anavyompenda Yesu. Kuna wengine katika maisha wamekuwa wakifukuzia kazi na wengine mpaka interview wanafanya na wana kila sababu ya wao kupata lakini ajabu wanachukuliwa kama wasio stahili  watu wanabaki kujiuliza kulikoni mambo haya???maswali ni mengi kuliko majibu jambo moja nimejifunza kwenye maisha Kama Kuna jambo linakuepuka kwa sasa lina heri hata kama lina maumivu kiasi gani kwa wakati huo.


Uliza watu wengi kati ya walioolewa kwa maana halisi ya kuolewa na ndoa ya furaha kama hao wenzi wao ndo wapenzi wao wa kwanza, kuna wengine walikuwa na ma relationship yao wakaachwa wakalia, wengine wakakonda wengine wakajifungia vyumbani kuepuka aibu ya dunia, lakini leo hii Wako na ndoa zenye furaha na watu wengine kabisa, kuna wengine waliolewa kabisaaaaa ndoa kwa maana halisi mwisho wa siku wengine wakaachana leo hii wako na ndoa zingine Wamesahau mateso yao yote ya hapo awali, kila Likueoukalo lina heri ndani yake.
Kati ya Maswali ambayo Mungu nadhani anapokea kila siku kwenye meza yake (kama anayo) ni swali la WHY You allowed this to happen to me???Why Me??Why Why???hivi umewahi kulia kilio hiki mbele za Mungu???kuna watu waliponea chupu chupu kujiua kwenye maisha yao baada ya kukosa Majibu ya Mungu na Wanadamu, kwa kudra za Mwenyezi Mungu yakatokea ya kutokea Wakawa wazima Wakavumilia Leo hii Ukiwakumbusha Walichotaka kukifanya Wanacheka na kujiuliza "Sijui Nilikuwa na akili gani".

Kuna watu wanatafuta furaha uliyo nayo wana zaidi ya miezi hawajawahi ipata, kuna wake na waume za watu Wanatamani wangekuwa na amani na furaha ambayo ndoa yako inayo lakini hawajapata, kuna wanawake wanatamani Waume zao Wangekuwa wametulia kama wewe, na Wasikivu kama Wa Kwako lakini hawana, kuna Wanawake Wamewakatia tamaa waume zao lakini wanashindwa kuacha ndoa zao sababu ya Watoto, Kuna Watu kwenye ndoa zao wanapigwa vibao kila siku lakini wewe unapigwa ma-busu, kuna watu wanatamani wangekuwa na kazi uliyonayo wewe, lakini wengine wamefukuzwa, Kuna Watu wanatamani wangeendesha gari unaloendesha lakini Mungu amekupa nafasi, wenzetu Zanzibar wanakosa hata nafasi ya kujimwaga mwaga kama Kanisani kwenu lakini hawana hiyo nafasi. Kuna mambo mengi sana Mungu anakupusha nayo yana heri ndani yake.


Kama kuna kitu umekosa kwenye maisha usilie stage ya kukufuru, kama umefukuzwa kazi usijilaumu kiasi cha Kumkosa Muumba, Kama Umeachwa na Mpenzi wako Usifikirie kujiua, Kama umetapeliwa ukajiona wewe ni mjinga wa wajinga usikate tamaa, Kama umepewa talaka usijione wewe ndio zigo la dunia, Kama umetafuta kazi na umefanya application zaidi ya 200 Usijione wewe una nuksi, Kila Jambo Likuepukalo Jua lina heri ndani yake ni kweli mengine yanatuacha na hisia kali, mengine yantuacha na maumivu mengi, na mengine yanatuletea maswali kuliko majibu kuwa kwanini inatokea kwako tuu, uhai ni zaidi ya ulichokosa, wewe sio wa kwanza kukosa kwenye maisha,kuna waliokosa kuliko wewe na wakajaribu tena.

Huwa hatujui ni nini Mungu anatuepusha navyo kwenye maisha ila "Siku Moja Tutaelewa" niliandika article hii siku chache zilizopita nikisema katika mambo mengi yanayotokea kwenye maisha huwezi jua kwanini yanatokea ila "siku Moja Tutaelewa"...Click here...http://samsasali.blogspot.com/2012/04/papaa-on-tuesdaysiku-moja-tutaelewa.html.


Neno la Mungu linasema Mawazo Ya Mungu yako Juu sana, sasa inawezekana Mungu anakuepusha na mambo usiyoyajua hapo baadae ukikosa usikate tamaa simama kaza buti safari bado inaendelea ukilia sana hakuta kusaidia, tangu umeanza kulia umepata nini zaidi ya "Pole", Maisha ni Kuamua, unaweza kuamua kuwa na furaha ama kuwa na huzuni, unaweza kuamua kucheka unaweza kuamua kulia. Ila Kila unapokuwa kwenye maswali mengi ya Why Why Why imekutokea basi jifunze kuwa Kila Lilalotuepuka Lina Heri, na Kila Linalotupata Lina Funzo ndani yake.

Papaa
0713 494110

1 comment:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda