Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, May 15, 2012

Papaa On Tuesday....Anayetaka Usawa Mwisho Wake Uchawi


Kama kawaida siku ya Jumanne naungana na blogger Samuel Sasali kupitia blog yake ya http://samsasali.blogspot.com/ kukuletea makala ya Papaa On Tuesday anapozungumzia masuala mbalimbali ya maisha. Leo Papaa anasema ``Anayetaka Usawa mwisho wake Uchawi``.......
Sam Sasali, Kichwa cha Ukweli sana 

Na Samuel Sasali a.k.a Papaa Sebene
Katika Kila Kabila hapa nchini kwetu Tanzania kuna misemo ama maneno yaliyokuwa yakitumika katika Jamii hizo, nakumbuka siku za nyuma niliwahi ongea kuhusu ndege anayepatika kule kijijini kwetu mwenye jina la Ripyoko, kama hukusoma watu wenye tabia sa Ripyoko gonga hapa http://samsasali.blogspot.com/2012/02/papaa-on-tuesdayripyoko-ana-uzuri-wake.html.

Katika neno la leo nimechukua maneno kutoka katika mila za kabila za Watu wa Ukerewe wenye msemo "Anayetaka Usawa Mwisho Wake Uchawi". Maneno haya yalitumiwa na wazee wa Kikerewe kuwa husia vijana wao na kuonyana wao kwa wao kuhusu watu kuwa na Tamaa katika maisha. Kila Kitu ukitaka kuwa sawa na wengine ikitokea kwamba huna uwezo basi unafika mahali utumie njia nyingine kupata ama kumuondoa yule aliyenacho. Ikitaka Usawa kwenye kila kitu na huku huwezo huna basi katalogy ya zamani ni Uchawi unamalizia ili kuwa nacho.

Kwenye Kizazi chetu cha leo njia za kupata mambo, fedha na ufahari ziko nyingi sana. Kuna watu wametamani kuishi kama wengine, sababu watu wana magari nao wametamani kuwa sawa nao kwa sababu hii kuna wengine wameuza utu wao wameuza miili yao kupata fedha kuna walioingiliwa kinyume cha maumbile ili wapate kile wanachotaka kuwa nacho ili waonekane nao wanacho. Kuna waliolala na Wanaume ama Wanawake ili wapate simu za Mikononi. Kuna walioweka taaluma zao chini wakavuliwa nguo ili wapate kazi walizopata leo.

Kuna watu kadha wa kadha kwa kutaka kuonekana na wenyewe hawajambo kwenye maisha ili wawe sawa na mashosti zao ama Marafiki zao wamejikuta wametumia kila njia ili kupata kile wanachotaka kuwa nacho. Tamaa ya maisha ya hali ya juu imesababisha wengi wa vijana wenzetu na ndugu zetu kutumia njia za kila namna ili nao wawe nacho. Kuna Waume za watu wamewahonga akina dada maduka ya nguo na salon, kuna wake za watu wamelala na Serengeti Boys ili wawape kazi wakaka, Kuna Watu wazima na heshima zao Wametoa rushwa ili nao wapate wanachotaka kukipata. Kuna walioua watu, kuna waliopora waume za watu, kuna wanaotunzwa na wanawake mijimama ili tu wawe na maisha kama wengine. Kutaka sana Usawa Mwisho wake Uchawi.
Huwezi kuwa na kila Kitu. Kwanini usijitahidi kuchakalika na maisha. Kwanini uwe mtumwa wa mapenzi, huna raha na mumeo, huna raha na mkeo ingawa maisha yako yana kila kitu, unapewa kila kitu unapata kila kitu kasoro amani ndani ya maisha yako. Inakusaidia nini kuupata Ulimwengu wote Kisha ukakosa Uzima wa milele??.

Wengine wameingia kwenye Ushoga sababu za kujikidhi kimaisha, wengine wameingia kwenye biashara za kujiuza sababu ya kutaka nao wawe nacho. Wanafunzi wanatafuta wanaume wa Kulala nao na Kuwahonga ili awe anabadilisha chakula kila siku, ili awe anavaa nguo za gharama kila weekend. Wengine wanajiuza kwenye mitandao ili wapate BlackBerry. Maisha ni Mbegu unachopanda ndicho utakachovuna. Mshahara wa dhambi ni mauti, huwezi kupata mshahara kama hujafanya kazi. Wapo wanaopandishwa vyeo ili wawe "Mabosi" kwa njia za short cut, Wapo hadi wanaotafura Soko la Ujasiriamali wa vitu vyake kwa kujiuza, yaani anajiuza ili kupata tender kwenye Kampuni fulani, sio vijana sio wana ndoa maisha ni safari ndefu, kwa sababu hii kuna wanandoa wamewaambukiza wenzi wao HIV, kwa sababu hii kuna vijana wameukwaa UKIMWI sababu ya kutafuta kuwa kama fulani.
Inakusaidia nini kuwa kama mimi, Inakusaidia nini kuwa kama fulani, inakusaidia nini unapokuwa unashindana na fulani kuwa wewe umefanikiwa sana kuliko mwingine. Mambo haya yamepelekea wengine kuoa ama kuolewa na watu wasio wapenda kutoka kwenye mioyo yao lakini sababu ya uwezo wa fedha wamejikuta wamedondokea huko, watu hawa wamejikuta hawawezi kuachana watu hawa ili tu waendelee kuchuna wenzao. Hawana furaha ingawa ukikutana nao ni full bling bling, magari makubwa, full amaduka ya vipodozi kwa hali hii wapo wengi wanasaliti ndoa zao.

Mashindano ya namna hii hayana mwisho we unaponunua hiki wenzio anakufunika na wewe unatafuta namna ya kumfunika, nae anakufunika, mwisho wa siku utatamani afe. Rafiki yangu Chela aliwahi sema "Kuna Wachawi Wengi Sana Hawashiki Tunguli, Ila Matendo yao ni Uchawi tosha". Ishi vile Uwezevyo usiishi kama vile watu watakavyo, Wahenga walisema Kuchamba Kwingi Mwisho huondoa NNyaaa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda