Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, May 8, 2012

Papaa On Tuesday: Is not Linking But it Links

Kila Jumanne Ohayoda itakuwa ikiungana na blogu rafiki ya samsasali.blogspot.com katika makala yake maarufu ya kila siku ya jumanne ``Papaa on Tuesday``.
Twende kazi.....

Is not linking....but it linksKwa kudra za Mwenyezi Mungu ni matumaini yangu ya kuwa wote tu wazima na Mungu bado ni mwema kwetu, nafahamu wengine wanapita katika "rough roads' za maisha lakini ninaamini "Hata Hilo Nalo Litapita" hakuna hali ya kudumu katika maisha.

Samuel Sasali ``Papaa Sebene``
Pili ninapenda kuwashukuru wapenzi wa Blog waliojitokeza kuja kwenye Mkesha Mkubwa wa Aflewo hapa Dar-es-Salaam ijumaa iliyopita. Nilikutana na watu ambao walijitambulisha kuwa ni wapenzi wa Blog. Mungu ni mwema sana.

Papaa On Tuesday ya Sept, 2010 niliandikia Papaa On Tuesday hii ambayo nimeihuisha kuwa inayoendana na mazingira yetu ya mwaka 2012.

Nianze kwa kusema kuna matukio mengi sana yaonayoendelea katika maisha yetu kwa kuyafanya ama kufanyishwa au kufanyisha tukidhani hayana uhusiano na sisi kwenye maisha yetu ya baadae ukweli ni kwamba yanauhusiano mkubwa sana kwa jicho la karibu as if they are not linking, the fact ni kwamba yana link.

Tumeona kwenye Kampeni za Igunga na Arumeru zilizopita tuliona Past inavyoletwa mbele ya maisha ya watu, tazama Dr. Slaa suala la ndoa na Upadri ambavyo limeshikiwa bango he thought is not linking but its links, tumeona matendo ya Mawaziri yalivyowagharimu na kuwaondoa katika nafasi zao kwa uteuzi mpya wa Rais

Kuna mambo mengi sana tunadhani yanatokea kwenye maisha yetu by chance na tukaamua kuyapotezea lakini the fact is kuna link kubwa ya matukio ya maisha yetu ya nyuma ya sasa na wakati ujao. Wote tunatambua story ya Yusuph na ndugu zake matukio yoteeeee ukiyatazama ni kama hayana link na future yake lakini ndo scenario nzima mpaka anakuja kuwa waziri mkuu from gerezani as if is not linking but it links mtu wangu. Kaa dakika mbili think of yourself where you came from watu uliokuwa nao na kusoma nao, angalia ulikopita huwezi jua kama kuna link na future yako but I tell you there is a link.

Njia za Mungu ni ndefu sana, nilikutana na rafiki yangu Weda Ringo Loyola High School Wakati huo mimi nafundisha vipindi Vya dini yeye akiwa Mwanafunzi, kuanzia wakati huo tukawa marafiki ni wakati huo ndipo aliponipa wazo la Blog na kulishikia bango. Kama sio Kwenda Loyola na Kukutana na Weda pengine leo Papaa On Tuesday isingekuwepo. Huwezi Jua haya mambo huwa yanaanzia wapi na Kuishia wapi, mengi tunaonaga ni kama Coincidence lakini yana link kwa namna moja ama nyingine kwenye maisha yetu ya Kila siku. Kuna watu utakutana nao ama kuna hali watakupeleka either utarudi nyuma ama utaenda mbele ama utabaki hapo hapo ulipo.

Waza ulivyokutana na Mumeo ama Mkeo ama Mchumba wako, Waza namna ulivyofahamiana na fulani, tafakari namna ulivyopata kazi ya sasa kutoka ile ya Awali, kuna mambo yanakuwa kama bahati mbaya lakini kumbe yana mwelekeo wa maisha. Nilikutana na Mc Pili Pili Facebook, kwa namna ya ajabu lakini kumbe kuna kusudi, mambo mengi tunaona "Is Not Linking, But It Links"

Ask yourself mara ngapi mambo mengi yanatokea kwako ndo unakuja realize kuna connection, huwezi Jua Mungu anataka wewe ufike wapi but there must be a link mambo mengi yanayoendelea sasa with our future. Waza mwenyewe namna ulivyojiunga na kanisa ulilosali, waza namna ulivyopata kazi, waza namna ulivyompata mume au mkeo, waza namna ulivyopata nyumba unayokaa, kuna link kubwa sana, ninachotaka kukuthibitishia it doesn’t matter what are you passing through, the best is yet to come, ukitazama ulivyo sasa na ulikotoka as if there is no link but ipo, maisha ni ups and down getting and loosing, our future is already designed. Kuna watu wanakuja kwenye maisha yetu wanatuuuuuuuumizaaaaaaaaaaaaa, but good enough they are just part of our future. Usitazame kidole kinachoonesha mwezi utazame mwezi wenyewe.

Nimejifunza kujisikia vibaya pia ni sehemu ya maisha, usijisikie vibaya kujisikia vibaya, there other times I just feel lonely and alone, lakini kuna neno huwa nalitumiaga na rafiki yangu  mwenye jina la Protace tangu tukiwa mwaka wa kwanza chuoni, "Hili nalo Litapita" nakumbuka kulikuwa na hard times kwenye maisha yetu ya chuo, tulikuwa mpaka kuna majira ya kukusanya na kupotezea, nakumbuka rafiki yangu huyu Protace alilazwaaaa hahahah Jamani Mapenzi balaaaaa yaani unapenda mpaka unalazwa dhuuu, na tulipobaki wawili tu tukiwa tunaongea tunakuliza kwanini hili limetokea, then tukasema “Hili Nalo Litapita”. Some other times Mungu anawaondoa people we loved them very much yaani kama nilivyompendaga naniiiiiii, na tunaona ulimwengu umekuwa Upside Down na kama ulimwengu wote umekwisha, unawazaaaaaaa hupati majibu, ukweli ni kwamba its just a Season and Its a Matter Of Time, huwezi kupotezea siku zote, there is a time you will get what you want.

Nimalize kwa kusema historia inaweza kuandikwa kwa dakika moja na isifutike milele na unaweza dhani is not linking but it links someday somewhere. Huwezi kuwa na hali zote siku zote, huwezi kuwa na furaha siku zote, usijisikie vibaya kujisikia vibaya, kupata na kukosa vyote kwenye maisha vipo, huwezi kupata milele kuna siku utapoteza, huwezi kuwa nafuraha kuna siku watu watakuboa, huwezi kufurahishwa na Kila Mtu siku zote, lakini hakuna anayeweza kudumu kwenye hali moja siku zote, kila linalotokea katika maisha “Jua Nalo Litapita”

If two people always agree on everything, then one of those people is probably not needed…..Is not linking But It Links.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda