Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, May 9, 2012

SHAMQE LEKU: Toka 1998 shule ya Msingi Maretadu Juu

Leo katika pitapita zangu, nilisikia mtu ananiita, sikuweza kumtambua haraka mpaka alipojitambulisha. Huyu bwana anaitwa Shamqe Leku nilisoma naye shule ya Msingi Maretadu Juu. Miaka 14 imepita toka tumeonana lakini imenikumbusha mambo mengi sana. Jamaa alinishangaza kwa kitu kimoja ambacho leo ndio nimekijua, ``alikuwa ameoa toka tukiwa darasa la tano!!`` duh!
Hivi sasa ana watoto watatu wa kiume, Amos (16) amemaliza darasa la saba, Rogate 13 na Alex 9. Namkubali sana huyu mshikaji kwa sababu uzazi wa mpango kauzingatia.
``Kuna raha ya kuzaa mapema Amani`` aliniambia ``wananisaida kazi nyumbani na sasa ninamiaka 30 nshamaliza kazi ya kuzaa`` alisema huku akiona fahari akiwa na watoto wake.
Duh! Shamqe amenifanya nifikirie vizuri uamuzi wangu wa bado nipo nipo sana!


Nikiwa na Shamqe na wanawe!

Shamqe akiwa na machalii wake watatu, dah gepu hili ni soo

Kutoka kushoto ni Alex, Amos na Rogate

Swahiba Shamqe Leku

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda