Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, May 22, 2012

Zaidi ya 800 waomba Kujiunga na Chuo cha Uuguzi Haydom

  • 450 wafanya mtihani kati ya waombaji 800
  • Mtihani wachelewa kuanza, ufinyu wa nafasi chuoni wahamisha mtihani Kanisani
  • 45 kudahiliwa kati ya 450Zaidi ya watahiniwa 450 kati ya walioomba 800 wanafanya mtihani wa kujiunga na chuo cha uuguzi cha Haydom (Haydom School of Nursing). Kutokana na hali hiyo, imebidi masomo ya kawaida kusimama chuoni hapo kwa ajili ya kupisha shughuli hiyo, lakini pamoja hayo nafasi haikutosha na ikabidi mtihani huo ukafanyikie katika Kanisa la Haydom (KKKT) kwani chuo hicho kina uwezo wa kuchukua wanafunzi wasiozidi 200.
Uwingi wa watahiniwa hao unatokana na ukweli kwamba chuo hiki kimekuwa moja ya vyuo bora zaidi vya uuguzi nchini na kujipatia sifa ndani na nje ya Tanzania na kimekuwa na rekodi nzuri ya kutoa wauguzi bora.
Mkuu wa Chuo hicho ndugu Barthlomayo Paulo Madangi aliwaeleza watahiniwa hao zaidi ya 800 na wengine 30 wanaofanya mitihani ya ``Up grading`` kuwa watakaochaguliwa ni wale wenye vigezo vya kujiunga na chuo hicho na watakaofaulu.
``Hakuna atakayeingia kwa mlango wa nyuma`` aliwaeleza wakati akiwakaribisha na kuwapa maelekezo ya mitihani ```na wala msifikirie kama kuna atakayeingia kwa mlango wa nyuma, ni wale tu wenye vigezo na watakaofaulu ndio tutakaowachagua``
Ohayoda iliweza kumhoji mtahiniwa moja aliyejitambulisha kwa jina la Erick Abraham kutoka Arusha ambaye alisema kuwa japo watahiniwa ni wengi anajiamini kuwa atafaulu.
``Nilipata habari kuhusu hiki chuo mtandaoni, ninajiamini nitafaulu na kupata nafasi`` alisema Erick
Haydom School of Nursing kina uwezo wa kudahili wanafunzi 45 tu kwa mwaka na 20 wa ``upgrading``.
Ohayoda inawatakia watahiniwa wote mtihani mwema.

Mkuu wa Chuo Barthlomayo Paulo Madangi (kushoto) akiwa na msaidizi wake Cecilia Nakei ofisini kwakeWasimamizi wa mtihani wakiwa ``busy`` kuhakiki watahiniwa kabla ya mitihaniKila kona ya chuo hiki watu kibao haijawhi kutokea, embu cheki hapa chini, 45 tu ndio watakaopata udahili kazi ipo kama una moyo mdogo wala hautapoteza muda hasa.

Mkuu wa Chuo akitoa maelezo kwa watahiniwa


Madangi na Crescent Ombay 

watahiniwa wakiwa makini kusikiliza maelezoKila kona watu wapo ``busy`` hasa Mkuu wa Chuo ndugu B. Madangi

Ofisi ya mapokezi ya HSN ilikuwa imependezaje?

Foleni ya kuingia kwenye chumba cha mtihani japo walikuja kuhamishwa


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda