Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, May 15, 2012

Mkenya amtafuta mama Yake Haydom

TITAL SHADRACK NDUMUNA 


Kijana Tital Shadrack Ndumuna (Pichani) hapo juu, raia wa Kenya anamtafuta mama yake Gladys Hhando Gara aliyeondoka nyumbani kwao huko Baringo Kenya mwaka 2001 akiwa na miaka mitano amefika Haydom baada ya kupata habari kuwa mama yake ni mwenyeji wa maeneo ya Haydom.

Tital ambaye amemaliza kidato cha nne huko mwaka jana huko nchini Kenya, aliamua kumtafuta mama yake baada ya kuuliza kwa majirani zake na kumweleza kuwa mama yake anatokea Tanzania sehemu inaitwa haydom ndipo alipoamua kuja kumtafuta katika kipindi hiki anachosubiri matokeo ya kidato cha nne.
Tital amepita katika makanisa mbalimbali akiomba kuwa kama kuna mtu anamfahamu mama yake amjulishe, leo asubuhi alifika katika sala ya asubuhi inayofanyika katika ukumbi wa Sala wa HLH inayowakutanisha wafanyakazi wote wa HLH

Kijana huyu ambaye hazungumzi lugha ya Kiswahili na kiingereza chake kikiwa ``hakijanyooka``, aliieleza Ohayoda kuwa kwa sasa anaishi na bibi yake baada ya baba yake kuoa mke mwingine ambaye alimtesa. Ohayoda ilipomwuliza ameweza vipi kuja huku alisema kuwa alipewa hela na mfadhili wake wa kimarekani alikuwa anamsomesha.
Aidha kijana huyu ambaye ni Mmasai wa Masai Mara alieleza kuwa anatoka eneo la Baringo karibu na mpaka wa Somalia, lakini Ohayoda ilibaini kuwa Baringo ipo karibu na Naivasha kama kilometa 100 tu kutoka Nairobi, mbali kabisa na mpaka huo anaoueleza. Ohayoda ilimwomba aoneshe Baringo ipo wapi kwenye ramani ya Kenya ``alijikanyaga na kudai kuwa kwao ni mpakani na Somalia na pia ni kama kilometa 200 kutoka Masai Mara.
Aliendelea kueleza kuwa anandugu wengine amabo ni Jackson anayefanya kazi nchini Marekani, Magdeleta aliyepo Urusi na mdogo wake anayesoma Los Angeles Marekani.
Anasema kuwa amejua kuwa mama yake ni mwenyeji wa maeneo ya haydom kutoka kwa majirani zao huko Kenya na alikuja huku mwaka jana kumtafuta mama yake na kisha akarudi kwao kufanya mtihani wa kidato cha nne (KCSE) lakini alipoulizwa alikuwa anasoma shule gani alijibu kuwa alisoma shule inaitwa ``Central School`` majibu ambayo hayakuiridhisha Ohayoda.
Aidha Ohayoda ilitaka kujua kama amefuata taratibu zote za uhamiaji alijibu kuwa amezifuata lakini alipoombwa kuonesha pasi yake ya kusafiria alijisachi kisha kudai ameiacha alipofikia.
Ohayoda ilipomtafuta mwenyeji wake ambaye ni mratibu elimu kata ya Haydom, alisema kuwa alikuja kwa mara ya kwanza mwaka jana Oktoba na aliletwa na kijana moja ambaye hawakuwa wanaelewana lugha na kuwa amerejea tena nchini kama siku tano zilizopita.
MEK huyo alizidi kufunguka kuwa kijana huyo hajafuata taratibu zozote za uhamiaji na amekwisha kutoa taarifa kwa afisa mtendaji wa kata ya Haydom.

Pengine ni kweli kuwa kijana huyu anamtafuta mzazi wake japo maelezo yake yanatia mashaka mengi, lakini ni vyema kwa wananchi kutoa taarifa katika vyombo husika anapotokea mtu yeyote hasa asiyefahamika na zaidi ya yote akiwa si Mtanzania kwani wengine huwa si watu wema ni matapeli. Kinga bora kuliko tiba!

Taarifa zilizofikia ohayoda hivi punde zinadai kuwa kuna tetesi za kuwepo kwa mtu anayeitwa ``Hhando Gara`` maeneo ya Murkuchida ambako inasemekana pia binti yao aliolewa nchini Kenya siku nyingi na hawajui aliko kwa sasa. Kijana huyo yupo kwenye mchakato wa kwenda huko kwa sasa.

Tital anaomba kama kuna mtu yeyote mwenye taarifa na mama yake huyo amjulishe kupitia namba za simu  0689528609

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda