- Washiriki kutoka Haydom wafanyiwa hujuma saluni na kwenye vyumba vya kuvalia
- Miss Haydom aingia jukwaani akilia machozi
- Lucy Stephano na Paschalina Emmanuel kuwakilisha Mbulu Miss Manyara
Hayawi hayawi hatimaye yakawa, jana ikawa jana na hatimaye kitendawili cha nani kuibuka kidedea yaani atakayevikwa umalkia wa wilaya ya Mbulu kikateguliwa jana usiku katika ukumbu wa Kituo cha Jamii (Community Centre) kwa wawakilishi kutoka Haydom kuibuka kidedea kwa kushika nafasi za juu kabisa.
Lucy Stephano ambaye ni Miss Haydom No.2 hakuamini masikio yake pale alipotangazwa mshindi na kujinyakulia zawadi zenye thamani ya shilingi laki tatu (300,000/=) huku Paschalina (Linah) Emmanuel ambaye alikuwa Miss Haydom No. 3 akiibuka mshindi wa pili na kuweka kibindonizawadi zenye thamani ya shilingi laki mbili (200,000/=) na pia aliibuka kuwa Miss Talent Mbulu 2012 na kushinda fedha taslimy shilingi 80,000/= na mshindi wa tatu katika king`ang`anyiro hicho ambacho washiriki kutoka Haydom walilalamika sana kufanyiwa hujuma na wawakilishi kutoka Mbulu alikuwa Modesta Robert aliyejishindia shilingi 50,000/= na zawadi nyingine.
Katika hali ya kushangaza, Miss Haydom alikataa kupanda jukwaani dakika za mwisho huku akilia machozi katika kile kilichodaiwa na washiriki kutoka Haydom (5 kati ya 9 walitoka Haydom) kuwa kufanyiwa hujuma ikiwa ni pamoja na nguo zao kukanyagwakanyagwa, kusemwa vibaya na hata walipokuwa saluni washiriki kutika Mbulu ndio waliopewa kipaumbele hali iliyopelekea Agnes Michael ambaye ni Miss Haydom kutokutaka kushiriki hadi alipobembelezwa na hata alipokubali alipanda jukwaani akiwa na uso wa huzuni na hakutoa tabasamu lolote na kushika nafasi ya 7 huku dada yake Juliana Michael ambaye hakushiriki Miss Haydom lakini alishika nafasi ya nne.
Kwa matokeo hayo, Lucy Stephano na Paschalina "Linah" wataiwakilisha wilaya ya Mbulu katika king`ang`anyiro cha kumsaka malkia wa Mkoa wa Manyara tarahe 25 mwezi huu kitakachofanyika Babati.
Ohayoda inawapongeza Lucy na Linah na kuwatakia mafanikio mema mbele ya safari yao
 |
Lucy Stephano akiwa kapozi kabla ya mashindano |
 |
Wadau wa Miss Haydom Mr. & Mrs R. Kawala wakipata msosi kabla ya shindano |
 |
Miss Haydom akiwa mwenye huzuni kabla ya shindano |
 |
Meza ya majaji |
 |
Shoo ikaanza |
 |
Burudani ikashika mkondo wake |
 |
Kati ya watu ninaowakubali sana ni Tumaini Group, walifunika ile Mbayaaaaaaaaa |
 |
Hapo vipiiii |
 |
Hapo jee? |
 |
Na hapa jee? |
 |
Miss Haydom yaani hakwepo kabisa jukwaani |
 |
Lucy Stephano mwenyewe, mwingine copy |
 |
Walimbwende wote tisa |
 |
Miss Talent, Linah wa Kutoka Haydom akipanda jukwaani kupewa taji |
 |
"Lina" miss talent na first runner up (mshindi wa pili) wa Miss Mbulu |
 |
Second Runner up (mshindi wa tatu) wa Miss Mbulu Modesta Robert kutoka Mbulu akipewa zawadi |
 |
Lucy Stephano mmmmm Need I say More? Funika woooote! |
 |
Lucy Stephano katikati akiwa na Linah kulia na Modesta kushoto |
 |
Agnes Michael akipokea zawadi ya kushinda Miss Haydom 2012 |
 |
Washiriki katika picha ya pamoja na Lucy |
 |
Majaji wakiwa na washiriki |
 |
Mgeni rasmi Isaac Masesa |
 |
Swahiba wangu sanaaa Mary Margwe alikuwa ndani ya nyumba |
 |
Mashostiiii |
 |
Ikafika mambo ya "umbali sifuri" hawa ni Bwana na Bibi Robin Inch Kawala |
 |
Burudani ikashika hatamu |
Picha zote kwa hisani R.I.K
love it ... Nimehuzunishwa kusoma story ya Lucy .. She is so beautiful... yaani kwa kweli alitakiwa kuwa miss Manyara.. Kila lakheri kwa miss Mbulu wa sasa .. tuwakilishe vema uendapo..
ReplyDeleteLucy kama unasoma Ohayoda ningependa tu kukwambia si kila mtu dunia hii anakutakia mema, ndivyo binadamu walivyo(na jinsi ulivyo mzuri) utajenga maadui kuliko marafiki. ila hayo ndo maisha usilete watu kama hao wakuharibie maisha yako.. you never know labda hata ungekuwa Miss Tanzania. kama ungeshiriki.. Jinsi ya kukomoa watu kama hao (maadui zako) ni wewe kufanya vema kuliko wao.. nakutakia kila lakheri na unachofanya maishani.. Keep your head up girl , your bloody beautiful..
my apology...
DeleteThe previous message was for Agness ( Miss Haydom & not Lucy)..
miss mbulu wa sasa ni beauty by nature
ReplyDelete