Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, May 18, 2012

Miss Mbulu 2012: Leo ndio leo, ndani ya Community Center-Mbulu

Ukumbi wa Cummunity Center-Mbulu
Leo ndio leo asiye na mwana aeleke jiwe kama si kokoto...lile shindano la kumsaka mlimbende wa wilaya ya Mbulu litafanyika leo usiku katika ukumbi wa Community Centre, Mbulu Mjini.
Shindano hilo linalodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redds, limeandaliwa na FMR Entertainment ya Mbulu chini ya promota Babuu ambao pia ndio walioandaa shindano la kumsaka miss Haydom wiki mbili zilizopita.

Akizungumza kwa simu kutoka Mbulu, promota Babuu amelieleza Ohayoda kuwa maandalizi yote yamekamilika na warembo wote tisa wapo tayari kutoa burudani kali na ushindani utakuwa mkubwa sana baina yao.
"Napenda kuwaambia wananchi wa Mbulu kuwa watarajie burudani kali sana kutoka kwa hawa warembo, pia kutakuwa na mziki kutoka kwa Wannee, K-Man wa Mbuli, Kikundi cha sarakasi cha Tumaini Group chini ya Flatei pamoja na FMR dancers wakiongozwa na Nickson" alisema Babuu

Aidha alizidi kueleza kuwa mshindi wa shindano la leo, licha kupata fursa ya kuwakilisha wilaya katika mashindano ya mkoa, ataibuka na kitita cha TSH 300,000/=, mshindi wa pili atapata 200,000/= huku mshindi wa tatu akipata 100,000/= na atakayeibuka mshindi mwenye kipaji "miss talent" atapata shilingi 80,000 huku mhindi wa nne na watano watapata 50,000/= na washiriki waliobaka watapata kifuta jasho cha 30,000/=.
Miss Haydom 2012, Agnes Michael
Je ataibuka kidedea tena leo?

Katika mashindano hayo ya leo yanayojumuisha warembo 9 kati ya hao 4 wanatokea Haydom akiwepo Miss Haydom 2012 Agnes Michael.
Warembo hao walipiga kambi katika Loji ya Sanu Park iliyopo Mbulu na yanafanyika kwa mara ya Kwanza. Ohayoda itakujuza yatakayojiri katika shindano hilo leo usiku.
Miss Haydom 2012 Agnes Michael (kulia) akiwa anapata msosi na washiriki wengine


Sitaki maswali jamani


Warembo Mazoezini

Wakipata msosi, hapa ni kwenye kambi yao, Sanu Park Lodge

1 comment:

  1. acheni kutuambisha, ni wapi tena huku na sisi tunaelekea?
    kuna fassions za kuiga si hizi

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda