Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, May 4, 2012

Miss Haydom Kufanyika Siku ya Jumamosi 6/05/2012

Hatimaye lile shindano lililokuwa linasubiriwa kwa hamu na wakazi wa haydom na vitongoji vyake la MISS HAYDOM, litafanyika kwa mara ya kwanza kabisa katika mji wa Haydom Jumamosi tarehe 05 May 2012 kwenye ukumbi wa CCM
Aidha wananchi wengi wamepokea kwa hisia tofauti haya mashindano ambayo ni mageni kwa wakazi wa Haydom hasa baada ya kutangazwa kufanyika.
"Hii kitu ni mbaya sana, inachochea momonyoko wa maadili, tumeshuhudia tabia chafu za warembo hawa mijini" alisema mdau moja ambaye hakutaka jina lake liandikwe.
Katika hatua nyingine, Mama Kari, Mjane wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Tiba wa HLH alimjia juu afisa utumishi wa hospitali baada ya kutangaza kuhamasisha kuhusu haya mashindano kwenye sala ya asubuhi inayofanyika kila siku asubuhi ikiwajumuisha wafanyakazi wote zaidi ya 500 wa hospitali hiyo teule ya rufaa ya mkoa.
Katika king`ang`anyiro hicho, wadau wengi wamedai kuwa mshindi atatoka kitongoji cha gangay!
Ohayoda itakuwa mstari wa mbele kukuletea yatakayojiri siku ya jumamosi kutoka ukumbi wa CCM ambapo kiingilio ni shilingi 10,000/=.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda