Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Saturday, May 5, 2012

Miss Haydom 2012: Leo hapatoshi ukumbi wa CCM Haydom

Hatimaye lile shindano la kumsaka kisura wa Haydom 2012 atakayewakilisha Haydom katika shindano la kumsaka mrembo wa wilaya ya Mbulu 2012 tarehe 18/105/2012 litafanyika leo jioni katika ukumbi wa CCM Haydom
Akizungumza na Ohayoda, Promota wa shindano hilo ambaye ni meneja masoko wa kampuni ya FMR Entertainment ya Mbulu , Babuu Adam alisema kuwa wakazi wa Haydom na vitongoji vyake wajiandae kupata burudani kali kutoka kwa warembo ambao wamekuwa wakijifua chini ya usimamizi wa Mrisha Ramadhani ambaye alikuwa Miss Manyara No2 mwaka 2011 na pia Miss Kanda ya Kaskazini No. 3 mwaka 2011.
Aidha Babuu aliendelea kutuhabarisha kuwa maadalizi yanaendelea vizuri, kila kitu kipo tayari kwa ajili ya kutoa burudani kwa watakaokwepo.
Lucy Stephano King`ang`anyiro cha leo kitajumuasha warembo 7 kutoka Haydom na Vitongoji vyake ambao ni pamoja na Lucy Stephano, Margreth Pius, Linah Emmanuel, Agnes Michael na Monica ambapo mshindi ataibuka na zawadi ambayo haijatajwa bado.

Katika hatua nyingine waandaaji yaani FMR Entertainment wameeleza kuwa wamekumbana na changamoto nyingi katika kuandaa shindano hilo kwani ni geni kwa watu wengi na linafanyika kwa mara ya kwanza Haydom na wilaya ya Mbulu kwa ujumla na kupata upinzani mkali kutoka kwa jamii ambao wanalichukulia kama uhuni na hivyo kutokuwaruhusu watoto wao kushiriki na huku washiriki wengi kujitoa baada ya kujiandikisha kushiriki kwa hofu ya kutoeleweka kwa jamii.
Akiendelea kufungua kwa Ohayoda, Babuu alisema kuwa malengo ya mashindano hayo zaidi ya kupata mrembo wa Haydom ni pamoja na kuinua vipaji vya wasichana ambao hawapati fursa ya kushiriki katika mashindano ya kikanda na kitaifa, kuitangaza haydom ikiwa ni pamoja na rasilimali ilizonazo, vivutio na kuvutia uwekezaji Haydom. Mengine ni pamoja kutoa elimu ya mambo mbalimbali kwa jamii, kutoa burudani na kuwaleta pamoja wakazi wa Haydom ma kujadiliana mambo mbalimbali.

Aidha shindano hili litaambatana na shoo kali kutoka kwa FMR Dancers wakiongozwa na Nickson Severini na Rajabu Athumani huku mziki mnee ukishushwa na DJ Tall na MC Top TZ akisherehesha shughuli nzima.
Warembo wanapambwa na KIWI BEAUTY SALOON chini ya Baby Juma na Teddy Jacob akiwa mlezi wa warembo hao.
Miss Manyara No.2 mwaka 2011 akiwa na Agnes Michael

Miss Manyara No 2 mwaka 2011Cecy 

Linah

Baby akiwa saluni kumwanda Margreth

FMR dancers

KIWI Salon-Haydom

2 comments:

 1. Ohayoda one of my favorite blogspot.. thank you so much for wonderful site. I love every bit of it
  :) keep up great job..

  I will love to go in KIWI SALON one day... .. Tchaooo

  ReplyDelete
 2. Thank you Afrodenzi, keep visiting it and you can participate to make it even much more better.
  Karibu sana Haydom

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda