Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, May 9, 2012

Milioni 26 kusaidia maendeleo ya Wahadzabe Kipamba-Iramba

Katibu tawala wa wilaya ya Iramba,Yahaya Naniyo,akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada kwa shule ya awali ya Kipamba na wakazi wa kitongoji hicho ambao ni Wahadzabe. Msaada huo ulitolewa na Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Singida (Singpress).
Mkazi wa kitongoji cha Kipamba kata ya Mwangeza wilaya ya Iramba,ambaye hakuweza kujulikana jina lake mara moja,akiomba alipwe fedha za kumpiga picha.
Mkazi wa kitongoji cha Kipamba kata ya Mwangeza ambaye amekataa kutaja jina lake,akiwa kwenye nyumba yake ya kuishi na familia yake. (Picha na Nathaniel Limu).
imeandikwa na Nathaniel Limu (http://dewjiblog.com)
Halmashauriya wilaya ya Iramba mkoani Singida, inatarajia kutumia zaidi ya shilingi milioni 26 kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii ya watu wa kabila la Wahadzabe wa kitongoji cha Kipamba kata ya Mwageza.
Hayo yalisemwa juzi na Katibu tawala wa wilaya ya Iramba, Yahaya Naniya, wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi zawadi kwa shule ya awali ya Kipamba pamoja na wakazi wake.
Alisema kati ya fedha hizo, baadhi zitatumika katika hatua za matumizi bora ya ardhi.  Lengo ni kuhakikisha kunakuwa na matumizi bora ya ardhi, hifadhi ya mazingira na kuzuia migogoro ya matumizi ya raslimali hiyo.
“Wananchi wote wa jamii ya kihadzabe watapatiwa elimu ya hifadhi ya mazingira, jumla ya vikundi sita vya ufugaji nyuki, vitaundwa na kupewa mizinga bora 120 ya ufugaji nyuki” 
Kuhusu sekta ya elimu, Naniyo alisema serikali imeshaboresha mazingira katika shule za msingi na ambayo asilimia kubwa ya wanafunzi, ni wahadzabe.
Msaada huo katika SINGPRESS, ulikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani

Habari hii na Picha ni kwa mujibu wa www.dewjiblog.com  

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda