Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, May 21, 2012

Mbulu Cathedal: Kanisa la pili kwa ukubwa Afrika Mashariki

Kuna mambo mengi sana ya kujivunia kutoka huku kwetu, ukiacha wanamichezo walioiletea sifa kubwa nchi yetu katika anga za kimataifa wametoka huku kwetu, nami asiyemjua Filbert Bayi? Zebedayo Bayo na Francis Naali?
Kwa upande wa siasa nako, toka uhuru tumekuwa chachu ya demokrasia ya kweli kwa kutokukubali kuendeshwa na kuamuliwa mambo na viongozi wetu, kifupi tumekuwa nuru kwa nchi nzima kutambua kuwa kiongozi ni mtumishi wa wananchi na wananchi ndiyo wanamamlaka ya kumchagua kiongozi wampendaye na si kuamuliwa na viongozi. Kama unabisha nenda kamwulize yaliyomkuta Nyerere mwaka 1960 alipowalazimisha wananchi wamchague kiongozi wa TANU ambaye si chaguo lao, siyo kwamba walikuwa na ugomvi na TANU la hasha, bali hawakutaka kulazimishiwa kiongozi. Nenda kaulize Karatu watakupa ``Mkanda mzima`` kuna jamaa anaitwa Patrick Qorro hawezi kusahau kamwe.
Hayo ni ya kwenye siasa na michezo, leo tukumbushane jambo moja ambalo yumkini hata sisi wenyewe hatulitambui kuwa ni la kujivunia. Jengo la Kanisa Katoliki Mbulu ndilo la pili kwa ukubwa AFRIKA MASHARIKI! Ngoja niandike kwa kiingereza inaweza kuwa na uzito ``Mbulu Cathedral is the Second Largest Cathedral in East Africa! Unashangaa? Ndo ujue hivyo sasa!


1 comment:

  1. Nimekuelwa; je kanisa la kwanza kwa ukubwa ni lipi Africa Mashariki?

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda