Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, May 1, 2012

MAMA KARI ATEMBELEA NA KUWAAGA WALIMU NA WANAFUNZI WA MAMA KARI

Mjane wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Tiba wa Hospitali ya Kilutheri ya Haydom marehemu Dr. Evjen Olsen, Mama Kari, siku ya jumatano tarehe 25 Aprili alitembelea shule iliyopewa heshima ya kutumiwa jina lake, Mama Kari Sekondary School, iliyopo kwenye kijiji cha Endaharghadatk, kata ya Haydom kwa ajili ya kuwaaga wanajumuiya ya shule hiyo kabla hajarudi kupumzika nyumbani kwao Norwaya baada ya kuishi Haydom kwa zaidi ya Miaka 50.

 "Ni heshima kubwa sana nimepewa" Akiongea huku akitokwa na machozi, "ntawakumbuka daima na Mama Kari itadumu. Umri wangu umeenda sana, siwezi kuahidi kuwa nitarudi lakini tulishike neno hili, tuonane mbinguni"
Aidha Mama Kari kama ilivyokuwa ada yake katika miaka 50 aliyoishi Haydom toka aingie Tanzania siku moja baada ya Uhuru yaani Tarehe 9 Desemba 1961, hakuacha kuhubiri injili hata katika umri mkubwa alionao wa zaidi ya miaka 85. Aliwaachia neno kutoka Zaburi 37:5 "Umkabidhi Bwana njia zako, naye atafanya" alimalizia Mama Kari

Awali wakimkaribisha Mama Kari, Diwani wa Kata ya Haydom, Mh. Nasaeli Sulle na Afisa Mtendaji kata ya Haydom, Mh. Isaay waliwataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili kulienzi jina la Mama Kari na kumhakikishia kuwa jina la Mama Kari.
Mama Kari alitoa zawadi ya Kamusi za Kiingereza (Dictionary) 20 na nguo za michezo kwa ajili ya wanafunzi.

Mama Kari ataondoka nchini tarehe 23 May kurudi kwao Norway baada ya kukaa Tanzania kwa zaidi ya miaka 50, huduma yake kimwili na kiroho haitasahauliwa kamwe na matu wa Haydom na maeneo ya jirani.No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda