Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, May 29, 2012

Je Wairaqw ni Wambulu? Fahamu Historia yao na asili ya jina Mbulu...sehemu ya Pili


Kaka samahani je wewe ndiye coordinator wa Ohayoda blog? Kama ndivyo hebu tafadhali ufanye utafiti wa kabila la kiirak *IRAQW* na je hili jina la Wambulu origin yake ni wapi? Je hawa kama c Wabantu wametokea wapi? Maana naona kuna upotoshaji mwingi na tafiti za watu mbalimbali. I w'll appreciate that kaka-Joachim John

Je jina Wambulu lilianza wapi? Kutokana na eneo lote walilokuwa wanaishi la Mbulu, Karatu, Babati na Hanang kuwa katika wilaya moja wakati huo yaani wilaya ya Mbulu ndipo wakawa wanaitwa Wambulu kwa kuwa wanatoka katika wailaya ya Mbulu na wote wanapatikana katika wilaya hiyo tu! Lakini kwa kuwa wilaya hizo zimegawanyika sasa hivi kuwaita wambulu haina mantiki na pia kuna makabila mengine yaliyopo Mbulu pia
Lakini Je, nini maana ya Jina Mbulu? Hakuna jibu sahihi ya jina Mbulu asili yake na kuna majibu mengi, Ohayoda itayachambua yote ili kukupa mwanga na ukweli halisi
Twende kazi....
Kanisa katoliki Mbulu

1. German: Neu-Trier
Mbulu ni neno la Kijerumani (Neu-Trier) lenye maana ya Majaribio mapya (new trial). Wajerumani walifika Mbulu katika karne ya 19 na kuweka ngome yao (boma) hapo ambapo inasemekana kuwa Mbulu ilianzishwa siku moja na Nairobi. Kutokana na hali ya hewa ya mahali hapo kuwa nzuri na kuzungukwa na milima pande zote, wajerumani walipapenda mahali hapo kwa sababu ya kiulinzi pia japo hali ya hewa nzuri ndiyo iliyowavutia zaidi. Hivyo basi wakaweka mpango wa majaribio wa kupafanya Mbulu kuwa kama Berlin hasa ukizingatia utawala wa kijerumani ulikuwa wa moja kwa moja (direct rule) na waliweka makazi ya kudumu na walichukulia makoloni yao kama sehemu ya Ujerumani, ndiyo maana hata miundombinu waliyoyaweka ni ya muda mrefu!
Japo hili laweza kuwa sahihi lakini hakuna ushahidi wowote kuwa Mbulu ni neno la kijerumani


2. Imboru
Inadaiwa kuwa jina Mbulu linatokana na neno Imboru ambalo Wairaqw hulitumia wanapopataja Mbulu. Inasemekana kuwa ``waswahili na wakoloni`` walilitohoa jina Imboru na kutokana na matatizo ya ``r`` na L jina hilo lilibadilika hadi kuwa Mbulu na Wajerumani kushindwa kutamka Imboru.
Lakini utafiti mdogo wa matamshi unaonesha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa neo Imboru kugeuzwa kutoka Mbulu na kufanywa lionekane la Kiiraqw zaidi yaani Imboru. Mfano mzuri ni kuwa Wairaqw lazima wongeze irabu (aeiou) katika maneno yanayoanzia na M au N kisha kufuatiwa na konsonati. Mfano neno ``Ngano`` wairaqw hutamka ``angano`` na ``mjomba`` hutamkwa ``majomba``, ``ngamia`` hutamkwa ``angamia`` n.k
Pia majina ya maeneo mengi sana yamebadilishwa baada ya ``kuIraqwishwa`` mfano Haydom kutoka ``Heidom``, Garoch kutoka ``Garawja`` n.k
Lakini kwa upande mwingine, inasemekana neno Imboru linatokana na Imbori, moja ya majina ya Kiiraqw lakini huyu Imbori alikwa nani mpaka mahali hapo paitwe kwa jina lake? Tutaiangazia katika makala nyingine lakini hii inatupa uhalisia zaidi kuwa Imbori inatupeleka karibu zaidi na ukweli kuwa Mbulu limetokna na neno Imbori. Inasemekana Imbori alikuwa binti aliyepata mimba kabla hajaolewa (doroway) ambapo alifukuzwa kwao na kuozwa kwa ``Homo`` na kisha kwenda kuishi naye huko mbulu wakati huo bado wairaqw wanaishi Irqwar Daaw hawajafika Mbulu. Baada ya kuolewa ndugu zake walikuwa wakimtembelea wakisema ``Aya Imborir kawaan`` na hadi hapo baadaye pakabaki hivyo. 
3. Mbulu-Mtu anayeongea lugha isiyoeleweka
Kamusi ya kiwahili sanifu (sijainukuu rasmi) inaelezea neno Mbulu kama mtu anayeongea lugha isiyoeleweka.Kutokana na Kiiraqw kuwa tofauti kabisa na lugha za kibantu, kuna wanaoamini kuwa Mbulu imetokana na ``waswahili`` kuwaita Wairaqw kwa kuwa wanaongea lugha isiyoeleweka kwao.
hata na hivyo hija hii inakosa mshiko kutokana na ukweli kuwa kuna makabila mengine yasiyo ya kibantu na wanaongea lugha isiyoeleweka na pia ni ukweli usiofichika kuwa hakukuwa na mwingiliano (interaction) baina ya wairaqw na jamii za kibantu kabla ya wajerumani kwani wamekuwa na uhusiano au mwingiliano na Wadatoga zaidi na kwa upande wa mashariki wamepakana na wamasai ambao si wabantu na wanyiramba kwa magharibi.
Hoja hii inakosa mshiko kwani kwa jinsi kiswahili kinavyokua kimekuwa kikiingiza maneno mapya kwa kutohoa zaidi kuliko kuyaunda, hivyo kuweka uwezekano mkubwa sana kwa Kiswahili kulikuta neno Mbulu tayari likiwa linatumika na tayari wairaqw wakiwa wanaitwa Wambulu na hivyo kulipa maana ya mtu anayeongea lugha isiyoeleweka.


Huo ni uchambuzi wangu kuhusu asili ya neno Mbulu...kama kuna mtu anamaana tofauti na hizi nilizoeleza anakaribishwa kuujulisha umma au wadau na kisha kwa pamoja tujadili kupata jibu sahihi zaidi. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda