Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, May 29, 2012

Je Wairaqw ni Wambulu? Fahamu Historia yao na asili ya jina Mbulu...sehemu ya Tatu

Kutoka Imbori hadi Imboru na kisha Mbulu

Katika sehemu hii ya mwisho, nimepata bahati ya kuongea na Mzee Modesti Gilyo na Mzee Lohay Bariye ambao walinisimulia kuhusu binti aliyeitwa Imbori. Haya ni maelezo yao ikiwa ni sehemu ya majibu ya sintofahamu iliyojitokeza katika sehemu ya pili ya makala haya. Twende kazi...

Wakati Wairaqw wakiwa bado wanakaa ``Irqwar Da/aw`` yaani bado hata hawajaanza kuhamia maeneo ya Mbulu, kuna binti alikuwa anaitwa Imbori alipata mimba yaani Doroway. Doroway ilikuwa inaleta unajisi ``meeta`` kwenye familia husika na katu binti hakuruhusiwa kuzaa nyumbani na hawezi kuolewa na Mwiraqw yeyote, hivyo ilibidi Imbori afukuzwe kwao salama yake ni aolewe na mtu wa kabila lingine yaani ``homo`` ambao mara nyingi ni wadatoga au wambugwe. Lakini kulikuwa na taratibu za kufuata na ilikuwa hivyo pia kwa Imbori.
Alipobainika anamimba, Imbori alinyolewa nywele na kupakwa majivu kichwani ikiwa ni utambulisho kuwa ana``doroway`` alipfungashiwa chakula ambacho mara nyingi huwa viazi au mahindi ya kuchoma (haya yalikwepo muda wote kutokana na hali ya hewa ya Irqwar Da/aw) na kuongozwa na kaka yake aliyekuwa anatembea mbele yake ili amkabidhi kwa ``homo`` yeyote atakayejitokeza kama anataka mke au chakula kikiisha afie hukohuko porini au aliwe na wanyama. Wakafika sehemu inayoitwa Mantla ambapo ni njia panda moja inaelekea Murray na nyingine Kainam na kwa kuwa Nade Be/a ambaye ni mganga maarufu kutoka Manda do Bayo alikuwa anakaa Murray hawakuthubutu kupitia njia hiyo maarufu kama ``tlo/u /awaak`` ambayo pia ilikuwa njia ya wamasai waliokuwa tishio kwa wairaqw hivyo wakapita njia ya Kainam hadi Aya Ma/ami ambako alifanikiwa kumpata ``homo`` aliyemwoa akaondoka naye hadi Mbulu.
Alipokwisha kuolewa ile ``meeta`` ikaisha na ndipo ndugu zake (pengine hata yeye mwenyewe baadaye) kumfuatilia kwa njia aliyofuatana na huyo mume wake na kufanikiwa kumpata na hatimaye kumtembelea mara kwa mara.
Katika kumtembelea huko, walikuwa wakisema tunaenda kwa Imbori ``do imboru kawaan``na hatimaye pakawa maarufu kama kwa Imboru na hatimaye Imboru. Wajerumani walipofika wakashindwa kutamka Imboru wakawa wanasema Mbulu na ndipo hatimaye jina Mbulu likawa ``official``

Shukrani za pekee kwa Mzee Modesti Gilyo na Lohay Bariye, wasomaji wote wa Ohayoda hasa Joachim John ambaye aliomba nifanyie kazi hii mada, Marco Sanka, Fakihi Fadhili, Yotham Yuda, Chronik Afrik ``Tumaini Koppa``, Emmanuel Elibariki wa HSN, Ofisi nzima ya 4CCP ikiongozwa na Mama Happy, Janeth John na Mzee Yakobo Awe.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda