Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, May 11, 2012

January Makamba na Somo kwa Wabunge wetu

Kati ya mambo yaliyonigusa sana jana jioni wakati naangalia kipindi cha Original Komedi ni jinsi Masanja Mkandamizaji alivyobuni na kufanya ``fundrising`` kwa ajili ya msanii mwenzake Sajuki anayehitaji kwenda kufanyiwa matibabu nchini India kupitia wabunge mbalimbali.


January Makamba
Kati ya wabunge wote walioshiriki, Januay Makamba ambaye ni mbunge wa Bumbuli wilayani Lushoto siyo kwa kuhusiana na harambee aliyokuwa anaiendesha Masanja, La hasha bali kwa jinsi alivyokuwa mbunifu kwa ajili ya jimbo lake la Bumbuli. January alimkaribisha Masanja katika ofisi za Bumbuli Development Corporation yaani Shirika la Maendeleo Bumbuli zilizopo kwenye jengo la NSSF Water Front jijini Dar es Salaam na kwa fahari kabisa (of course anastahili kujisikia fahari) alimpitisha Masanja katika vitengo mbalimbali vya ofisi hiyo.
Kumbuka hiyo siyo Ofisi ya Mbunge bali ni Ofisi ya Shirika la Maendeleo Bumbuli, mradi alioubuni kwa ajili ya maendeleo ya jimbo lake akitumia fedha za mkopo wa ``Shangingi`` wanazopewa wabunge.
January alieleza kuwa ``Tulipopewa ule mkopo sikununua gari kwa kuwa tayari nilikuwa nalo hivyo niliamua kufungua ofisi hii na kuajiri vijana ambao kazi yao kubwa ni kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ajili ya wanaBumbuli``
January Makamba ambay hivi karibuni aliteuliwa kuwa naibu waziri wa Sayansi na Teknolojia, ni mtoto wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na kisha kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Luteni Mstaafu Yusuf Makamba, ni somo tosha kwa wabunge wetu ambao hufikiri kujinufaisha wenyewe pasipo kuweka maslahi ya waliowachagua mbele.
January alinifanya nitafakari kwa kina, kumbe inawezekana kwa wabunge wetu hata kama wanaishi mijini (Arusha na Dar es Salaam) lakini hukohuko walipo wakafanya kitu kwa ajili ya wananchi majimboni mwao. Ni kweli kuwa wasomi wengi kama si wote wapo mijini lakini swali ni je, wabunge wetu wamefanya jitihada gani kuwaunganisha huko walipo na kubuni miradi ya maendeleo huku nyumbani? Nadhani  ni wakati muafaka kujifunza kutoka kwa January ambaye anawakilisha vijana wapenda mabadiliko katika jamii, japo muda mwingi yupo Dar es Salaam na tena hivi sasa ni Naibu Waziri lakini bado ana ``connection`` na jimbo lake, kwani anadai kuwa hajafunga ndoa na serikali bali wananchi wa Bumbuli ambao ndio waliompa dhamana ya kuwaongoza na kwao anawajibika. Je ni mara ngapi wabunge wetu toka Matheo Qaresi, Philip Marmo, Frederick Sumaye na Mary Nagu wamechukulia kuteuliwa kwao kuwa mawziri kama sababu ``excuse`` ya kusahau waliowapeleka bungeni na kujichimbia mijini?
Mary Michael Nagu, Mbunge wa Hanang

January ameandika kitabu chake kiitwacho ``Bumbuli, Jana, Leo na Kesho`` pia anatovuti yake ya http://www.januarymakamba.com/ ameipigia sana debe Bumbuli na amebeba taswira ya kiongozi makini na mwenye mawazo ya kisasa zaidi (modernist) tofauti kabisa hata na baba yake achilia mbali chama chake ambacho wengi huamini ni chama cha wazee na wasiopenda mabadiliko.
Hapo nikakumbuka miaka ya mwanzo ya 2000 kulikuwa na kitu inaitwa DODEA (Dongobesh Division Development Association), sijui malengo na nia ya waanzilishi hasa ni nini, ila naamini ilikuwa na lengo la kusaidia kuleta maendelea kwenye Tarafa ya Dongobesh, lakini kilichotokea hapo kati hakijulikani na DODEA ikafa kifo cha kimya kama mtu aliyelala chumbani huku jiko la mkaa likiwaka!
Ni hayo tu kwa leo, naamini wabunge wetu hata kama hawatapata fursa ya kusoma makala hii naamini wapambe wao wataisoma na kuwafikishia ujumbe!
Ijumaa Karim

OMBI: Tafadhali usiache kupiga kura ya maoni kuhusu swali letu wiki hii lililopo upande wa juu kulia mwa blogu hii linalosema ``Ni idara ipi ya serikali inaongoza kwa rushwa?``

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda