Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, May 17, 2012

Inaendelea Sasa Hivi: Warsha ya wawezeshaji jamii juu ya mabadiliko ya hali ya Hewa

Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni Haydom, 4CCP kinaendesha warsha ya siku mbili kuanzia leo hadi kesho inayofanyika katika Ukumbi wa mikutano (pavilion) ya 4CCP iliyopo katika Kituo cha utamaduni Haydom.

Mgeni rasmi Mh. Diwani wa kata ya Haydom, Nasaeli Sulle akifungua Warsha

Warsha hiyo ni warsha ya kwanza mwaka huu ambapo wawezeshaji jamii takribani 100 kutoka makundi manne ya lugha (wabantu, Wanailotoki, Wakushi na Wahadzabe) wamehudhuria na kupata mafunzo mbalimbali kuhusu Athari za mabadiliko ya hali ya hewa na Haki Ardhi.
Warsha hii imehudhuriwa na Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Manyara ndugu Edward O. Mollel, Ndugu Deogratius Mathiya (Afisa ardhi-Mbulu), Mullingwa C. M. Sabbi (Afisa ardhi-Iramba), Fausta Awet (afisa utamaduni wilaya ya Mbulu), James Sulumo (Afisa utamaduni-Hanang), Charles M. Kingu (Afisa utamaduni wilaya ya Iramba)
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hii, mheshimiwa diwani wa kata ya Haydom ndugu Nasaeli Sulle aliwataka wawezeshaji hao kuyafanyia kazi mafunzo watakayopata ili kujenga jamii bora na ushirikiano baina ya makundi hayo.

Wawezeshaji katika warsha hii ni ndungu M. Mgelwa, afisa misitu wa tarafa za Haydom na Dongobesh akisaidiana na Bw.Frank Shoo (afisa misitu kata ya Haydom) kutoa mafunzo kuhusu athari za mabadiliko ya Hali ya hewa. Aidha Deo Mathiya na maafisa ardhi watatoa mafunzo kuhusu Haki Ardhi na ndugu Mollel pamoja na maafisa utamaduni watatoa mafunzo kuhusu shughuli za uboreshaji wa kazi za utamaduni.
Katika warsha hii wawezeshaji hawa hupata wasaa wa kukaa katika vikundi vyao na kujadilina na kuwasilisha namna mafunzo wanayoyapata yataleta mabadiliko katika jamii nzima.
Katika hatua nyingine, wawezeshaji hawa watafanya hafla fupi baadaye jioni kwa ajili ya kumuaga mama Kari ambaye anarudi kwao Norway tarehe 23 Mei mwaka huu. Mama Kari amechangia kwa sehemu kubwa kufanukisha shughuli za 4CCP tangu kuanzishwa kwake ikiwa ni pamoja na kugharimikia ujenzi wa jengo la ofisi ya 4CCP katika kituo hiki.
Ohayoda itazidi kukuletea matukio yaneyoendelea katika warsha hii

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda