Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Sunday, May 27, 2012

Ikiwa Leo Ni Siku Ya Kuombea Nchi Za Kiislam Duniani, Zanzibar Kanisa la Lachomwa Moto Usiku Wa Kuamkia LeoHali ya Amani katika Visiwa Vya Zanzibar hasa kwa Jamii ya Wakristo inazidi kuwa tete baada ya Usiku wa Kuamkia leo, Kanisa la TAG Visiwani Zanzibar linaloongozwa na Pastor Kaganga Visiwani humo kulipuliwa kwa kitu kinachosadikika kuwa ni bomu na kuteketeza sehemu kubwa ya madhabahuni mwa kanisa hilo na sehemu za Milango ya Kanisa hilo.
Kanisa hilo lililokuwa na uwezo wa kuchukua Waumini zaidi ya 1000 limechomwa moto ikiwa ni mara ya pili baada ya mara ya kwanza kitu kinachosadikika kuwa ni bomu kutupwa ndani ya kanisa hilo mwanzoni mwa mwaka huu na bomu hilo kushindwa kulipuka wakati wa Ibada.
Baada ya Uchunguzi wa Polisi katika tukio la kwanza Polisi walisema bomu hilo lilokuwa na uwezo wa kuteketeza kila kitu kilichomo ndani ya Kanisa hilo lakini ajabu halikuweza kulipuka wakati lilikuwa tayari kwa kulipuka.
Kumekuwa na hali ya Sinto fahamu kwa Wakristo wengi wanaoabudu katika Makanisa Visiwani Zanzibar na kasi ya Serikali katika Kushughulikia masuala haya imekuwa si ya kuridhisha.
Ndugu zetu wa Zanzibar wanahitaji maombi katika kusimama kwao katika ardhi hiyo inayosadikiwa watu zaidi ya 95% ni dini ya Kiislam
Picha za Tukio Zitafuata hivi punde.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda