Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, May 8, 2012

Ijue Historia ya Kisiasa Mbulu, Karatu, Babati na Hanang..1

Katika sehemu hii ya kwanza ya makala hii tutapitia mabadiliko ya kisiasa hasa katika majimbo ya uchaguzi katika wilaya za Mbulu na Karatu toka mwaka 1960.
Kanisa Katoliki Mbulu, Moja ya Makanisa Makubwa zaidi Afrika Mashariki

1960-Chief Sarwatt anashinda kiti pekee cha ubunge kama mgombea binafsi akimshinda Chief Amir Dodo aliyesimamishwa na TANU
1965-Katiba inafanyiwa mabadiliko na kuwekwa kwa kipengele kinachomzuia mgombea binafsi, Chief Sarwatt anaingia TANU
1965-Katika uchaguzi mkuu, jimbo linagawanywa na kuwa na jimbo la Mbulu na Babati. Chief Sarwatt anashinda tena Mbulu huku Dodo akiwa mbunge wa kwanza wa Babati
1967-Sarwatt anateuliwa na rais kuwa kwenda kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na nafasi yake kushikwa na Damian Ge/ay
1970-Jimbo la Mbulu linanagawanywa na kuwa Mbulu na Karatu, Damian Ge/ay anakuwa mbunge wa Mbulu na Patrick Qorro anakuwa Mbunge wa kwanza wa karatu
1975-Jimbo la karatu linavunjwa na kuwa jimbo moja tena la Mbulu ambapo Patrick Qorro anamshinda Damian Ge/ay
1980-Salutian Deeng`w anamshinda Patrick Qorro na kuwa Mbunge wa Mbulu
1985-Jimbo la Mbulu lagawanywa tena, ambapo Philip Marmo anashinda uchaguzi jimbo la Mbulu na Patrick Qorro anaingia bungeni kwa mara ya tatu tofauti akiwakilisha Karatu
1990-Marmo na Qorro wanatetea viti vyao bila upinzani
1994-Katika uchaguzi wa serikali za mitaa, Kijiji cha Gongali chamchagua mwenyekiti kutoka CHADEMA na kuwa kiongozi wa kwanza kabisa kutoka upinzani toka kuanza tena vyama vingi nchini
1995-Katika kura za maoni CCM jimbo la Karatu, Dr. Wilbrod Sla/a amshinda patrick Qorro lakini NEC yatengua matokeo na kumsimamisha Qorro. Wazee wamsihi Sla/a kujiunga na CHADEMA
Dr.Slaa akiwa na aliyekuwa mkewe Rose kamili ambaye sasa ni
Mbunge wa viti maalum CHADEMA-Hanang

1995-Katika Uchaguzi Mkuu, Dr. Wilbrod Sla/a ashinda uchaguzi na kuwa mbunge wa Karatu kupitia CHADEMA akimshinda Qorro wakati Mbulu Marmo akimshinda kwa taabu ``binamu yake`` Safari Sangka Mislay wa NCCR-Mageuzi
1996/1997-Karatu yawa wilaya kamili na kujitenga na Mbulu
2000-2010-Marmo na Sla/a watetea viti vyao
2010-Katika kura za maoni, CCm warudia kosa lilelile kwa kumpitisha mgombea asiyependwa na watu kwa kumsimamisha tena Marmo na kumwengua Lorry
Akona/ay, Mbunge wa Mbulu-CHADEMA

2010-Dr.Sla/a asimamishwa na chama chake kugombea urais, Mchungaji Israeli Yohane Natse huku Mustapha Akona/ay wa CHADEMA akimshinda Marmo

Je itakuwaje mwaka 2015? Inaaminika kuwa CHADEMA wakishalichukua jimbo hawaliachii kamwe na hawafanyi makosa kama ya CCM. Na Je upepo utakuwaje kama Haydom ikifanikiwa kuwa jimbo? Tusubiri tuone

Ungana nami katika makala nyingine ambayo nitaendelea na wilaya za Babati na Hanang, ambazo pia zilikuwa sehemu ya wilaya ya Mbulu.

1 comment:

  1. Asante kwa historia hii fupi ya Kisiasa .Tuna mambo mengi ya Kujifunza (Mbulu-Karatu).

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda