Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Sunday, May 13, 2012

HLH: Serikali boresheni miundombinu tuwahudumie wananchi vizuri


  • Waomba barabara na uwanja wa ndege ziboreshwe
  • Waitaka serikali ilete wataalamu bingwa na kusaidia kulipa mishahara
  • Sera iangaliwe upya ili halmashauri zingine nazo zitoe ruzuku kwa HLH
Mustapha Akonaay (Mb) kushoto akiwa katika mazungumzo na Dr. Olav Espegren (katikati)
na Emmanuel Mighay (kulia)

Uongozi wa Hospitali ya Kilutheri ya Haydom umeiomba serikali kuboresha miondombinu mbalimbali hasa ya barabara ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi wanaopata hudum kutoka kwenye hospitali hiyo.
Akizungumza na Ohayoda baada ya kikao na mbunge wa Mbulu mh. Mustapha Akonaay (CHADEMA) ambacho hakuna mwandishi wa habari aliyeruhusiwa kuwepo, Emmanuel Mighay ambaye ni Muuguzi Mkuu wa HLH alisema kuwa uongozi wa Hospitali umekuwa ukibeba mzigo mzito kuwahudumia wananchi hivyo kuiomba serikali iongeze msaada zaidi kwani ruzuku inayotolewa kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ni ndogo mno kulingana na uhalisia.
``Sera ya serikali imeweka mbele sana mipaka ya kiutawala, lakini HLH ipo katika mipaka ya wilaya 3 za Iramba, Hanang na Mbulu na pia inahudumia wananchi kutoka Singida, Shinyanga, Arusha, Babati na Karatu lakini tunapata ruzuku ndogo kutoka wilaya ya Mbulu tu, tumemwomba mheshimiwa alifikishe kwa wahusika ili hizo halmashauri nyingine nao wachangie hasa wilaya za Iramba na Hanang``
``Pia tumemwomba mheshimiwa aboreshe miundombinu ya barabara ili kurahisisha kuleta wagonjwa hapa hospitalini na pia kupunguza uchakavu wa magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) kutokana na ubovu wa barabara``
``Kwa kuwa Hospitali yetu ni hospitli ya rufaa kwa sasa, lakini haina wataalamu bingwa, tumemwomba mheshimiwa aishawishi serikali ituletee wataalamu bingwa na pia kutusaidia kulipa mishahara. Vile vile tumeomba uwanja wetu wa ndege uboreshwe ili hata wagonjwa wnaotoka hapa kwenda kwenye hospitali za rufaa kama KCMC waweze kupata usafiri mzuri wa anga`` Alisema Emmanuel Mighay

Hospitali ya Kilutheri ya Haydom mbali na kuhudumia wagonjwa wengi kutoka sehemu mbalimbali wanaofika hospitalini hapo, inaendesha vituo vya afya vya Kansay kilichopo Karatu, Balangdalalu na Gendabi vilivyopo wilaya ya Hanang. Pia inaprogramu za kliniki za mara kwa mara (Outreach program) kwa kutumia ndege katika maeneo ya Endanyawish na Harbanghet vilivyoko wilaya ya Mbulu, Matala na Buger zilizopo Karatu na Kliniki mpya imefunguliwa Hanang. Pia kuna kliniki (outreach) za kila siku katika katika vijiji mbalimbali vya wilaya za Mbulu, Hanang na Iramba.
Awali katika mkutano na wananchi wa kata ya Haydom, Mheshimiwa Akonaay aliwaahidi wananchi wa Haydom waliokuwa wakitaka Hospitali ya haydom ipewe msaada zaidi na serikali ili kupunguza mzigo unaobebwa na hospitali hiyo na kuwapa gharama kubwa wananchi. Pia mbunge huyo aliwaambia wananchi kuwa ujenzi wa barabara ya mji wa Haydom ni kutokana na juhudi zake na si fedha za mfuko wa jimbo na kuongeza kuwa amepata fedha kwa ajili ya kutengeneza barabara ya Haydom-Dongobesh kupitia Maretadu.
Je yaliyozungumzwa yatafanyiwa utekelezaji au ni siasa za kila mara? Tusubiri tuone!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda