Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, May 2, 2012

Haydom Cultural Festivals Kufanyika September

Kwa mara ya kwanza katika mkoa Manyara, Haydom Four Corners Cultural Program-4CCP itafanya maonesho makubwa ya Kiutamaduni yatakayofanyika katika viwanja vya 4CCP-Haydom. Maonesho hayo yanatarajia kufanyika mwezi September 2012 na yatakuwa ya siku tatu ambayo yatawajumuisha wadau mbalimbali wa sekta ya utamaduni, taasisi, mashirika, makampuni mbalimbali na watu binafsi toka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.
Pamoja na mambo mengine, maonesho hayo yataambatana na maonesho ya ngoma za asili kutoka makundi manne ya lugha ya Afrika yanayopatikana kwenye eneo la Haydom (Wabantu, Wanailoti, Wakoisani na Wakushi) wanaowakilishwa na Makabila ya Wanyiramba/wanyisanzu, Wadatoga, Wahadzabe na Wairaqw.


Akiongea na Ohayoda, Amani Paul Gaseri ambaye ndiye mratibu wa maonesho hayo alisema kuwa maonesho haya yatatoa fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Manyara hususan Haydom na maeneo ya jirani kushiriki katka kusherehekea hazina kubwa ya utamaduni walionao, kujua umuhimu wa urithi wa utamaduni ambao unaelekea kupotea na kuutunza kwa ajili ya vizazi vijavyo.
"Ni fursa pekee kwa wananchi wa Mkoa wa Manyara kusherekea urithi wao na ikiwa ni pamoja na kujifunza kutoka makabila mengine ambayo ni tofauti na yao" Alisema Amani.

Pia kutakuwa na mashindano ya ngoma za asili ktoka makabila yote manne ambapo washindi watapata zawadi mbalimbali ambazo zitatajwa hapo baadaye.

Katika kutambua mchango mkubwa unaotolewa na mkoa wa Manyara katika kutoa wanariadha wanaoongoza kuliletea taifa letu sifa kubwa, kutakuwa pia na mashindano ya mbio ndefu yaani marathon ili kuwapa fursa wananchi wa huku kushiriki na kuibua vipaji katika sekta hii ya riadha, mchezo ambao ulililetea sifa kubwa nchi yetu kupitia wanariadha wanaotoka mkoa wa Manyara kama Filbert Bayi, Zebedayo Bayo, Francis Naali, Gidamis Shahanga, John Yuda, Steven Axwari na wengineo wengi.

"Tunaomba wadau mbalimbali watuunge mkono kuyafanikisha haya maonesho. Tunaomba mashirika, taasisi, makampuni na hata watu binafsi kushiriki katka haya maonesho na kusherehekea urithi huu na kuwa sehemu ya jamii ya mikoa ya Manyara na Singida katika kuuenzi utamaduni wetu.

Haydom ni sehemu pekee katika bara la Afrika ambapo makundi manne makuu ya Lugha zinazozungumzwa Afrika yanapatikana sehemu moja. Pamoja na tofauti kubwa zilizopo baina ya haya makundi (makabila) hususani kwenye matumizi ya Ardhi lakini makabila haya yanaishi kwa pamoja kwa amani na kuheshimiana. Haydom Cultural festival inatarajia kuyaleta makundi yote manne pamoja na kusherekea urithi wao kwa faida ya vizazi vijavyo.

Ngoma 

Vifaa vya asili vya kupepeta nafaka

kipepeteo

Majembe ya asili ya Wairaqw

Ilgendi

Kugema damu


1 comment:

  1. man natamani kuwa hapo...
    i'm gonna miss this :(

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda