Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, May 7, 2012

Halmashauri ya Wilaya ya Babati yashitakiwa

Ziwa Babati

Wakazi wawili wa wilaya ya Babati mkoani Manyara wameiburuza Halmashauri ya Wilaya ya Babati katika mahakama ya ardhi ya wilaya ya Babati wakiidai fidia ya zaidi ya Shilingi milioni 75 baada ya halmashauri hiyo kuyachuka mashamba yao yanayofikia takriban ekari nne mwaka 2004 pasipo kuwalipa fidia na kuyagawa kwa watu wengine.
Wakazi hao Bw. Bruno Ngumuo na Iddi Ngumuo walidai mahakamani hapo kuwa wamekuwa wakipewa ahadi za kulipwa fedha hizo kwa miaka saba sasa lakini zimekuwa ahadi hewa. Kesi hiyo imetajwa kusikilizwa tena tarehe 24 mwezi huu.

Kesi hiyo ni moja kati ya kesi nyingi zinazokumba halmashauri nyingi mkoani Manyara hasa za Mbulu na Babati na ile ya wilaya ya Karatu mkoani Arusha ambapo kumekuwa na malalamiko mengi ya wananchi kunyang`anywa ardhi zao pasipo kulipwa fidia.
Moja ya maeneo ambayo yameathirika kwa kiasi kikubwa na unyanyasaji huo wa hizi Halmashauri ni Haydom, ambapo mwaka juzi wananchi wapatao 35 waliiburuza Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu katika mahakama ya ardhi ya mkoa wakidai kulipwa fidia baada ya ardhi yao kuchukuliwa na kugawiwa watu wengine katika programu ya mpango mji wa Haydom iliyotekelezwa toka mwaka 1993 hadi 1997.
Aidha jambo la kushangaza ni kuwa, badala ya kulipa fidia husika, halmashauri iliamua kuwanyang`anya watu iliyowapa ardhi kihalali na imekuwa ikipokea ada za kila mwaka za umiliki wa hiyo ardhi na kuwarudishia walalamikaji hao pasipo hata kuahakiki kama walalamikaji wote wanastahili au la jambo amabalo limezua mgogoro mkubwa sana na wakazi wengi wameathiriwa na uamuzi huo mbovu wa Halmashauri hiyo ambayo imelaumiwa kwa kuwa chanzo cha migogoro hiyo.
Ohayoda imebaini kuwa wananchi wengi wamepoteza imani na hizi halmashauri hasa idara za ardhi ambazo badala ya kuratibu na kuboresha programu endelevu za matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya maendeleo, idara hizo zimekuwa chanzo cha migogoro isiyoisha katika maeneo mbalimbali. Ohayoda inauliza, kwa hali hii je tutafika?

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda