Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, May 8, 2012

Gongali: Kijiji cha kwanza Tanzania kuchagua kiongozi wa upinzani

Wananchi wa Gongali wakishiriki katika ujenzi wa
Shule ya Msingi iliyofadhiliwa na Primary Schools For Afrika

Wilaya ya Mbulu mwaka 1960 na kisha wilaya ya Karatu miaka 35 baadaye ziliandika historia ya pekee nchini pale ambapo wananchi walitekeleza haki yao ya msingi kidemokrasia kuwachagua viongozi wanaowapenda wenyewe na si kushinikizwa na viongozi wa kitaifa.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1960 TANU ikiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere, pamoja na kukubalika nchi nzima pengine kwa ushawishi wake lakini alifanya kosa moja ambalo liliigharimu TANU kwani katika uchaguzi huo TANU ilishinda viti 70 kati ya 71 ikikosa kiti kimoja kilichochukuliwa na binafsi Sarwatt baada ya TANU kumsimamisha Dodo ambaye watu walikuwa hawamkubali. Japo TANU ilishinda uchaguzi huo, Nyerere alijifunza somo na kuamua kufutilia mbali mgombea binafsi.
Miaka 34 baadaye, kijiji cha Gongali kilichopo Karatu kikaandika historia nyingine nchini, historia ambayo haitajwi sana pengine kwa kufunikwa na yaliyotokea mwaka 1995 baada ya CCM kufanya kosa kama ilivyofanya TANU miaka 35 kabla kwa kumwengua mgombea ambaye watu wanampenda na kumsimamisha mgombea wao yaani ``mtu wa System``. Katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 1994, Kijiji cha Gongali (ambako ndiko nyumbani kwa Dr. Slaa) kilimchagua Mwenyekiti wa Kijiji kwa kupitia Chama cha demkrasia na Maendelea, CHADEMA, japo wakati huo Dr. Slaa hakuwa amejiunga naa upinzani.
Pengine watu wengi wanadhani kuwa Dr. Slaa ndiye chanzo cha Karatu kuwa ngome ya upinzani nchini lakini Gongali ilianzisha safari, na wazee wa Gongali ndio waliomshawishi Dr. Slaa arudi nyumbani kugombea na kumpiga chini Patrick Qorro aliyekuwa mbunge lakini asiyejali maslahi ya wananchi.
Pengine kama si Gongali Dr. Slaa asingerudi kwenye siasa na upepo mkubwa wa mabadiliko ya kisiasa nchini yasingetokea, kwani katika uchaguzi wa mwaka 1995 CHADEMA haikuwa na nguvu kisiasa kulingana na vyama vingine lakini kwa kuwa kilikuwa na nguvu Gongali na kumshawishi Dr. Slaa agombee kupitia CHADEMA, CHADEMA kikapata mtu makini ambaye nchi nzima inamheshimu kwa kuibua hoja nzito na zenye msingi kwa maslahi ya Taifa.
Mbulu iliandika historia ya demokrasia nchini mwaka 1960, historia iliyoifanya TANU chini ya Nyerere kufuta mgombea binafsi, na Karatu ambayo wakazi wake walihamia kutoka Mbulu ikaikumbusha CCM makosa yao kwa kutokujifunza kutoka kwa TANU lakini Gongali iliandika historia ya kuwa mwanzo wa mabadiliko nchini na pengine historia ya kuanguka CCM ilianza kuandikwa na wananchi wa Gongali. CCM bado haijajifunza kitu kutokana na historia kama ilivyodhirishwa katika uchaguzi mkuu uliopita jimbo la Mbulu wakatoa ``photocopy`` ya makosa yaliyofanyika 1960 na 1995, kisha ikapeleka makosa hayo kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru.
Kama CCM itakufa kama wengi wanavyotarajia, Gongali itaingia kwenye historia kama mwanzo wa safari ya mabadiliko nchi.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanganyika, Mungu Ibariki Gongali!

2 comments:

  1. This is EXCELLENT. Please keep it up! For more information visit www.gongalimodel.org

    ReplyDelete
  2. Naombeni muazishe historia ya Askofu Hhando vizazi vipya vijue jinsi inavyowapasa kuwa..., naamini mnaweza

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda