Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, May 28, 2012

Geso Bajuta-Serikali walipeni mawakala kwa wakati


Na Joseph Lyimo,Hanang’
SERIKALI imeshauriwa iche kulimbikiza madeni ya mawakala wa pembejeo za
kilimo, ili kuepuka kuzorotesha shughuli za kilimo.

Imeelezwa kuwa ulimbikizaji wa  madeni hayo, unaweza kuwafanya  mawakala kushindwa kuwahudumia
wakulima ipasavyo.
Rai hiyo ilitolewa juzi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bajuta International, Gesso Bajuta,  alipokuwa akizungumza katia maonyesho ya kilimo ya wilayani Hanang’.

Bajuta alisema wakati umefika kwa Serikali kuwalipa  mawakala madeni yao, ili waweze kutoa huduma zao kikamilifu.

Alisema kufanya hivyo, kuliwezesha taifa kufikia azma ya kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo.

“Mawakala hawa wanafanya kazi hiyo kwa niaba ya Serikali, kwa hiyo ni vizuri wakalipwa fedha zao kwa wakati, ili waweze kuendelea kutoa huduma zao kwa ufanisi,” alisema Bajuta.

Bajuta pia aliishauri Serikali itafute  njia mbadala ya kuongeza ajira kwa maofisa ugani ili kuondoa tatizo la upungufu wa  wataalamu hao kote nchini.

Alisema hatua hiyo itawezesha  wakulima hasa wa maeneo ya vijijini, kuhudumiwa ipasavyo.

“Nchi yetu ina ardhi nzuri na  yenye rutuba ya kutosha na hali ya hewa nayo nzuri inayofaa kwa uzalishaji lakini, tatizo letu ni pungufu wa maofisa ugani ambao ni washauri wa wakulima kuhusu kilimo bora,” alisema.

Chanzo, Mwananchi 28/05/2012

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda