Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, May 31, 2012

Fahamu kuhusu Mkonga wa mawasiliano wa Taifa


Na Alexander Stephen-HLH
Tanzania ipo kwenye mchakato wa kusambaza mkonga wa taifa wa mawasiliano, mkonga huu unatakiwa usambazwe nchi nzima katika kila wilaya, hii ina maanisha kuwa Tanzania itakuwa imeunganishwa pamoja, toka hapo tunaungana na nchi zote za Afrika Mashariki, pamoja na Afrika ya Kusini, halafu tunaungana na dunia nzima.
Wanantumia ‘Fiber optic cables’ kusambaza mawasiliano hayo,
Kwa kifupi ni kwamba mkonga ni neno la kiswahili lililoongezwa kwenye kamusi miaka ya karibuni kumaanisha optics fiber kwa lugha ya kigeni. Kwa faida ya wengine, Fiber optics ni aina ya waya (cable) kama hizi tulizozizoea za kupitisha umeme au simu ambazo kwa kawaida huwa zinatengenezwa na madini ya shaba (copper) ila sasa mkonga (fiber optics) unatengenezwa na aina ya material kama inayotumika kutengeneza kioo (glass), kwa hiyo ni cable ambayo ni kioo na hutumika kusafirisha mawimbi (signal) ambayo yamegeuzwa kuwa mwanga (light). Hiyo cable ambayo ni kioo ni nyembamba sana, unene wake ni kama unene wa unywele wa mwanadamu na ndio maana inaitwa fiber (fibre) na kwa sababu mawimbi yanayosafirishwa ni mwanga (light/ optic) ndio maana inaitwa fiber optic. Kumbuka kwa kuwa fiber ni nyembamba sana na delicate huwa inawekewa ulinzi (protection) mkubwa sana kuizunguka (insulation) ndio maana unaiona imekuwa ni cable nene.
Kuna aina kuu mbili ya kusafirisha mawimbi ya mawasiliano. Moja ni kwa kupitia hewani (wireless network) na nyingine ni kwa kupitia kwenye waya (cable or wired network) ambayo kwenye hiyo njia ya kwanza kuna technolojia nyingi sana kama microwave antennas ambayo ndiyo makampuni ya simu km Vodacom, Tigo, Zain network yao kubwa inatumia hii technolojia, pia ipo sattelite communication ambayo vituo vingi vya redio na Tv vinatumia, pia kuna technolojia ya wifi na nyingine nyingi sana.

Kwenye hiyo technolojia ya pili inategemea zaidi ni aina gani ya cable unaitumia, inaweza kuwa shaba (copper) kama kwenye simu za landline za TTCL au inaweza kuwa mkonga (optic fiber) kama ambayo sasa serikali imeamua itumie kwenye hiyo network ya taifa ya mawasiliano ambao wanauta sasa Mkonga wa Taifa ambayo kwa mujibu wa malengo yao ni kuunganisha wilaya zote za nchi hii (sasa sijui itawezekana maana umeme tu ni tatizo na hata ikiwezekana bila umeme sijui zitatumika kufanya nini !!)

Huo mkonga wa Taifa kuna sehemu umepita ardhini na pia kuna sehemu nyingine umepita kwenye gridi ya taifa ya umeme. Kama ukipita sehemu yenye nguzo za umeme za gridi ya taifa kutokea ubungo kwenda mikoani utaona cable mbili juu kabisa hizo ndio mkonga wa taifa (achana na cable tatu za chini ambazo ni za umeme). Mkonga wa taifa umeunganishwa na fiber ya TTCL baadhi ya sehemu na pia unaunganishwa na fiber ya makampuni mengine inayopita baharini kuelekea nchi zingine. Kitu cha kunote ni kwamba, mkonga uliopita baharini sio mkonga wa taifa, ule unamilikiwa na makampuni binafsi.

Maelezo ni mengi, ila nadhani kwa haya mafupi umepata angalau hints.
Usisahau: kasi ya wireless network maximum ni 150 mbps  wakati ya fober optic ni 10Gbps

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda