Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, May 17, 2012

Fahamu Historia ya Simu za mkononi

Na Alexander Stephen,
Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano-HLH

Ni mawazo ya Samwel Morse, mawazo na ndoto zake zimekuwa ni nguzo kwenye mawasiliano.
Utakubaliana na mimi kwamba Teknolojia inayo bamba kuliko zote kwenye upande wa mawasiliano ya kielekroniki ni teknolojia ya  simu za mkononi, pamoja na huduma nyingine zinazo itegemea.
Kwahivyo utashangaa ni vipi tumetoka kwa Samwel Morse hadi hapa tulipo leo na tunapokwenda kesho.
Samwel Morse Iliwekeza kwenye TellegraphHistoria yoyote ya simu za mkononi inaanzia kwa Samwil Morse, Alianza kwa tellegraph ya usumaku, mwaka 1832 na kuitengeneza kwaajili ya mazoezi na majaribio mwaka 1835.
Mnamo Oktoba 18 mwaka 1842, Morse alitandaza waya kati ya Kisiwa cha Gavana na Bustani yake iliyopo New York umbali wa karibu maili 2 hivi. Sehemu ya waya huo ilipita chini ya maji, kwa kuwa alitaka kuonesha kuwa hata chini ya maji waya unaweza kusafirisha ishara (signals) , lakini kwa bahati mbaya kabla hajakamilisha zoezi lake meli ilipita    na kukata nyaya zake, na huo ukawa kama ni mwisho wa jaribio hilo.
Baada ya hapo kukatokea wazo la kutuma ujumbe na uwezekano wa kufanya hivyo ulianza kuonekana. Sasa ikajulikana kuwa maji yanaweza kuchukua umeme na kupeleka ujumbe, hivyo njia nyingine zikaanza kufikiriwa.
     
Mwaka 1843, mtaalamu na mchambuzi wa kemia Michael Faraday aliendesha utafiti wa kutaka kufahamu  kama "space" uwazi ungeweza kusafirisha umeme, kwakutumia kanuni ambazo tayari ziliwekwa kwaajili ya kuanzisha tellegraph.
Mwaka 1864 James Clerk Maxwellalitoa makala yake "Dynamic Theory of Electromagnetic Fields"
ambayo ili hitimisha kuwa mwanga, umeme, na usumaku vyote vina mahusiano vyote vinafanya kazi bega kwa bega, na "ellectromagnetic Phenomena" zinasafiri kwa mawimbi "waves".
Halafu mnamo mwaka 1865, Dr. Mahlon Loonis wa Virginia, daktari wa meno, ina semekana alkuwa wakwanza kutumia wireless kwa mawasiliano kwenye anga. Kati ya mwaka 1866 na 1873 alifanikiwa kutumia tellegraph kwa umbali wa maili 18 kutoka Cohoction hadi Beorse Deer    Mountains huko Virginia.
Alianzisha njia ya kusafirissha na kupokea ujumbe kwa kutumia anga (Earth's Atmosphere ) kama Conductor. Miaka 30 iliyofuata, wawekezaji na wataalamu walitengeneza tellegraph iliyo unganishwa kwa waya (wire line tellegraphy)
Majaribio yaliendelea kwa mfumo wa kujaribu na kukosea (Trial and error) pasipo kufanikiwa

Kuzaliwa kwa simu ya Mkononi
Akatokea jamaa mwingine kwa majina aliitwa Martin Cooper maarufu kama baba wa simu za mkononi aliajiriwa na kampuni ya Motorola mwaka 1954, Bw. Cooper alifanya shughuli ya kubuni bidhaa rahisi (developing portable products) ikiwa ni pamoja na redio ndogo ya mkononi ya polisi kwaajili ya idara ya Polisi ya Chicago ya mwaka 1967, na tena akaongoza utafiti wa simu za mkononi wa Motorola
Mnamo Aprili 3 mwaka 1973 Martin Cooper alipiga simu kwa kutumia simu ya mkononi kwa mara ya kwanza mbele ya umati, ikiwa kama maonesho ya ugunduzi wa simu ya mkoni.

Hii ndio simu ya kwanza na vipimo vyake
First  Cell Phone (1973):      Motorola Dyna-Tac
Size: 9 x 5 x 1.75 inches
Weight: 2.5 pounds
Display: None
Number of Circuit Boards: 30
Talk time: 35 minutes
Recharge Time: 10 hours
Features: Talk, listen, dial
   hii ni simu ya mwaka huu 2012
1 comment:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda