Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, May 9, 2012

Elewa maana ya Mrengo wa kulia na mrengo wa kushoto katika siasa
Na Mussa Billegeya
Moja katika ya maneno ambayo hutumika zaidi katika vyombo vya habari na siasa kwa ujumla katika dunia ya leo ni "Mrengo wa Kulia (Right Wing)" na "Mrengo wa Kushoto (Left Wing)". Leo nimeona ni vizuri kuangazia asili ya maneno hayo, matumizi yake ya mwanzo na maana yake halisi katika siasa za sasa
Mnamo mwaka 1789, baada ya Vuguvugu la mapinduzi nchini Ufaransa, kwa mara ya kwanza liliundwa bunge la kitaifa ambalo lilikuwa na pande kuu mbili - Upande Mmoja ni wale Waliotaka Mabadiliko, Mamlaka na uhuru zaidi kwa wanachi - yaani kupunguza mamlaka ya Mfalme juu ya masuala ya Utawala wa Nchi na kuyapeleka zaidi kwa Wananchi. Na upande wa pili ulikuwa ni wale waliokuwa upande wa Mfalme - waliokuwa wanatetea na kulinda maslahi ya Mfalme na tabaka tawala katika Ufaransa ya wakati huo!
Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Bungeni, makundi haya mawili yalikuwa yanakaa pande mbili tofauti (walikuwa hawachanganyikani). Waliokuwa wanataka Mabadiliko (wapingaji wa tabaka tawala) waliketi upande wa Kushoto wa Spika na waliokuwa hawataki mbadiliko, (Mahafidhina), walikuwa wanaketi upande wa kulia wa Spika - Utaratibu huu unaendelea mpaka leo katika mabunge yote duniani - Hadi Dodoma, Tanzania!

Kwa hiyo, wale waliokuwa wanatetea na kulinda tabaka Tawala waliitwa Mrengo wa Kulia (Right Wing, Conservatives) na wale waliokuwa wanataka mabadiliko waliitwa wa Mrengo wa Kushoto (Leftists / Left Wing, Liberals).
Hata hivyo, katika matumizi ya kawaida SIKU HIZI, Left Wing na Right Wing huwa sio istilahi zinazohusu zaidi nani anatetea Tabaka tawala na nani analipinga, bali zaidi Ni nani anatetea Maslahi ya Taifa/Utaifa zaidi na nani anataka Uhuru na Mabadiliko zaidi - hususan wanaotaka Muunganiko na Muingiliano zaidi wa Jamii na Mataifa mbalimbali na wageni!... Ndio maana katika nchi zilizoendelea, moja ya hoja za msingi ambazo hutofautisha mirengo ya vyama na watu ni suala la uhamiaji - wenye mrengo wa kulia hupinga kabisa masuala ya kuruhusu wahamiaji kutoka nje kuingia - na hususan kupewa haki kama raia wazawa, wakati wa mrengo wa kushoto huwa wazi na suala zima la wa hamiaji - wote kwa sababu tofauti.
Kwa hiyo,katika siasa za sasa, suala la kuwa mrengo wa kushoto au wa kulia halifungamani sana na kuwa madarakani au kuwa upinzani - bali linahusu zaidi aidiolojia ambayo mtu husika au chama inaisimamia. Kwa maana hiyo, Kuwa madarakani au kwenye Tabaka tawala hakumfanyi mtu akawa ni Right wing, anaweza akawa madarakani huku akiwa ni mrengo wa Kushoto (Liberal) ki-aidiolojia, na bungeni ataketi Mkono wa Kulia wa Spika, lakini akiwa ni Left wing Kisiasa / kiaidiolojia! Jambo la Msingi katika kutambua Mlengo wa Siasa katika dunia ya sasa huwa ni msimamo wa mtu kuhusu Taifa na Utaifa.
          
Wafuasi wa CHADEMA wakipambana na FFU                  
Wanaoweka taifa na utaifa wao mbele ndio huitwa Mahafidhina, Mrengo wa Kulia, na wale wanaoweka mbele "uhuru zaidi" kama kukaribisha na kutetea uwekezaji wa nje, mafungamano ya kimataifa n.k. huitwa Mrengo wa Kushoto.

Kwa mfano, marekani kwa sasa inatawalia na Mwanasiasa wa Mrengo wa Kushoto / Left wing / Liberal (Obama / Democrats). Hiki ni chama kinachoamini katika uhuru zaidi wa watu, kiko wazi zaidi katika muingiliano na ushirikiano na mataifa na watu wa mataifa mbalimbali zaidi na wageni kuliko chama cha upinzani ambacho ndicho cha kihafidhina - Republican! Rais aliyeshinda Ufaransa wiki hii ni wa Mrengo wa Kushoto-Kati (F. Hollande / Center-Left) kwa kumshinda Mhafidhina-kati (Center-Right) Sarkozy.

Kwa maana hiyo tunaongeza dhana nyingine hapo ya muhimu kuielewa, Center-Right na Center-Left. Hizi ni pande ambazo haziko ki-viile katika hiyo mirengo, tunaweza kusema ni mirengo  yenye aina fulani ya Uvuguvugu, ambapo husimamia masuala makuu ya upande wake (Kulia au Kushoto), wakati huo ikikubaliana na baadhi ya yale yaliyo upande mwingine...

tujadili pamoja, Je, wewe unadhani kwa Tanzania, ni vyama gani viko mlengo wa kulia na vipi viko mlengo wa kushoto? weka maoni yako hapo chini kwenye comments!


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda