Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, May 15, 2012

Datoga Bible Translation wamuaga Mama Kari

Ohayoda itakuwa inakuletea matukio mbalimbali yanayojiri katika hafla mbalimbali za kumuaga mjane wa marehemu Dr. Olsen anayejiandaa kurudi kwao Norway baada ya kuishi Haydom toka tarehe 10-12-1961 siku moja baada ya uhuru wa Tanganyila

Leo tunakuletea hafla iliyofanywa tarehe 12-05-2012 katika Hoteli ya IM mjini Haydom iliyoandaliwa na Timu ya kutafsiri Biblia kwa ligha ya Kidatoga.Hafla hiyo pia ilikuwa mahusui kwa ajili ya kumshukuru Mama Kari pamoja na mwanae Knut na familia yake kwa mchango wao wa hali na mali kufnikisha kuwa mradi wa kutafsiri Biblia kwa Kidatoga unaanza na kufanikiwa.
Katika hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Mbulu (KKKT) mchungaji Nzanganzelu, pia ilihudhuriwa na wachungaji mbalimbali akiwepo Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Haydom Mchungaji Zakaria Dalei, mchungaji mstaafu Yotham Girgis pamoja na timu nzima ya mradi wa tafsiri wa Biblia kwa kidatoga.
Akisoma risala fupi iliyoandaliwa, katibu wa mradi huo Dr. Isaack Malleyeck alisema kuwa mradi huo utaukumbuka daima mchango wa Mama Kari na Knut toka mradi huo umeanza mwaka 1989. Aliongeza kuwa mpaka sasa wamekwisha kumaliza kutafsiri Agano jipya kwa lugha ya kidatoga na bila msaada wa Mama kari na Knut pengine wasingeweza kufikia hapo.
Naye Mama Kari alikuwa na neno moja tu la ``Asanteni sana`` kwa timu hiyo kufanikisha kutafsiri Biblia kidatoga kwani anakumbuka alienda Yaeda chini na kukuta wadatoga wengi hasa kina mama hawaendi kanisani kwa kuwa hawaelewi lugha ya kiswahili au kiiraqw, ila sasa anafurahi injili itawafikia wote.
Naye Knut alisema anamshukuru Mungu kwa kupata fursa ya kuchangia katika mradi huu na kuwasihi waendelee na moyo ili kazi hiyo isonge mbele
Knut, Dr. Malleyeck, Mzee Festo na Petro Gasheka

Karibuni wageni

Namwona Mzee Yakobo upande wa kulia

Meza KuuDr. Isaack malleyeck

Mzee Festo


Si maonesho ya mavazi bali hivi ndivyo ``Mama Neema`` alivyolipuka

Mchungaji Yotham Girgis alipowasili


Mama Kari akifuta machozi

Risala ikisomwa

Msaidizi wa Askofu, mchungaji Nzanganzelu akimpa zawadi mama Kari

Mama Kari na Mama Happy katika vazi la kiasili la kidatoga

Shukrani kwa mama Kari

Knut naye akipewa zawadi

Knut akipokea zawadi ya mkuki na fimbo

Cheti cha Knut

Msosi kedekede

mate yalikuwa yananitoka 

Hii ndo IM Hotel, hoteli maarufu kabisa haydom na ndipo shughuli ya kuaga mama Kari ilipofanyika

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda