Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Saturday, May 12, 2012

Bweni la Wanafunzi Sanu Technical lateketea kwa moto

Bweni la wavulana la Sanu Technical Secondary School inayomilikiwa na kanisa Katoliki Jimbo la Mbulu limeteketea kwa moto na kusababisha hasara ya inayokadiriwa kufikia shilingi za kitanzania milioni 40.


Bweni lililoungua moto
 Akizungumza na Ohayoda kwa njia ya simu, Mkuu wa Shule hiyo Bw. Maximilian Pius alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa tatu usiku wakati wanafunzi wapo madarasani kwa ajili ya masomo ya usiku.
``Nilikuwa nyumbani kwangu niliposikia sauti ya filimbi inayoashiria hatari kutoka kwa wanafunzi, kwani wanafunzi wetu huwa na filimbi za kuashiria hatari, ndipo nilipotoka na kuelekea eneo la tukio na kukuta walinzi wakijitahidi kufanya jitihada za kuzima moto huku wanafunzi waliokuwa wanaishi kwenye bweni hilo wakitaka kuingia kuokoa mali zao lakini niliona ule moto unazidi kuwa mkubwa na wangeweza kupata madhara hivyo niliwaamuru walinzi wawazuie wanafunzi kuingia kwenye bweni lililokuwa linaungua`` Alisema Mkuu huyo wa Shule.
Alisema kuwa bweni hilo lililokuwa na wanafunzi 49 pamoja na stoo ndogo ya chakula iliyokuwa karibu na bweni hilo viliteketea kabisa na hakuna chochote kilichoweza kuokolewa.
``Mlinzi wetu alikuwa amelipa bweni mgongo hivyo hakuweza kuona upesi moto, alistuliwa na mlinzi wa jirani na ndipo walipojitahidi kuingia na kuanza kuuzima kwa maji lakini bila mafanikio`` aliongeza bwana Pius
Ohayoda ilitaka kujua kama kulikuwa na kifaa cha zima moto (fire extinguisher) hapo bwenini alijibu kuwa kweli kifaa hicho kipo ila ni kile kidogo na kwa kuwa moto ulianzia kwenye mojawapo ya vitanda na kuanza kushika magodoro, kifaa kile kisingeweza kuuzima.
``Moto ulianzia kwenye mojawapo ya vitanda na siyo hitilafu ya umeme, kuna uwezekano kuwa mojawapo ya mambo mawili yakawa ndio chanzo cha moto huo. Moja, wanafunzi wetu si malaika, inawezekana moja alikuwa anavuta sigara akawa hajaizima vizuri na kile kipisi akakificha kitandani na kusababisha moto au kuna uwezekano mkubwa sana ikawa ni hujuma kutoka kwa moja wa wanafunzi ambaye siku ya tukio alionekana bwenini mchana wakati wenzake wakiwa madarasani na hata usiku huo alikuwa amejificha kwenye vyoo vilivyokuwa jirani na bweni hilo takribani mita 25``
Aidha aliendelea kueleza kuwa mwanafunzi huyo alipohojiwa alidai kuwa alikuwa anajisikia kuumwa hivyo aliona ni bora ajifiche chooni jambo linalozua maswali mengi kwani kama alikuwa anaumwa kuna taratibu zinazofahamika na zinazofuatwa na wanafunzi wote wanapougua, na kwa hali ya baridi kali iliyokwepo kuna uwezekano mkubwa sana akawa amefanya hujuma.
``Bado tunaendelea na upelelezi kupitia serikali ya wanafunzi kujua chanzo haswa, ila madhara ni makubwa sana, pengine kungekuwa na gari la zima moto hapa Mbulu madhara yasingekuwa makubwa sana`` aliongeza Pius akiwa bado katika hali ya mshituko.
Aidha Ohayoda ilifanya uchunguzi na kubaini kuwa magari ya zima moto yapo Babati tu katika mkoa mzima wa Manyara na hivyo kutokuweza kusaidi hasa pale majanga ya moto yanapotokea katika maeneo mengine mbali na Babati. Ohayoda inatoa wito kwa wahusika kuliangazia macho swala hili ili kuweza kupunguza majanga yanayotokana na moto hasa katika shule za bweni ambako kuna historia ya kuungua. Ikumbukwe kuwa mwana 1994 wanafunzi wapatao 45 wa shule ya sekondari ya wasichana ya Shauritanga iliyopo Mkoani Kilimanjaro ambayo nayo inamilikiwa na Kanisa katoliki, waliteketea kwa moto na matukio mengine pia yameripotiwa kwenye shule kadha wa kadha za bweni hapa nchini. Ni wakati muafaka kwa serikali kuangalia hili swala.

OMBI: Tafadhali usiache kupiga kura ya maoni kuhusu swali letu wiki hii lililopo upande wa juu kulia mwa blogu hii linalosema ``Ni idara ipi ya serikali inaongoza kwa rushwa?``

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda