Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, May 11, 2012

Aliyeiba sahani na kuacha ``laptop ya Apple`` afungwa miaka 6 jela

Mahakama ya wilaya ya Mbulu jana tarehe 10 Mei imemhukumu kifungo cha miaka 6 jela Lulu Bayo mkazi wa Haydom kwa kosa la uwizi wa mali zenye thamani ya shilingi za Kitanzania zaidi ya 1,037,500 mali ya Nina Thomson Bakke raia wa Norway, mwanafunzi anayefanya mafunzo kwa vitendo katika Hospitali ya Kilutheri ya Haydom. Katika kesi hiyo, mahakama hiyo imemwachia huru mtuhumiwa mwingine ndugu Elias Hhando baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kumtia hatina mshitakiwa.
Awali katika kesi hiyo, mwendesha mashitaka wa polisi aliieleza mahakama kuwa mnamo tarehe 17 mwezi Machi mwaka huu majira kati ya saa moja hadi saa tano usiku wakati mlalamikaji ametoka kwenye nyumba anayoishi ndani ya hospitali, mshtakiwa alivunja mlango na kuiba vitu mbalimbali vikiwemo taulo, begi la kamera, mouse ya kompyuta, koti la mvua, jozi mbili za viatu vya kufanyia mazoezi, begi la nguo, mkanda wa kiunoni, begi la kubebea laptop,  kopo moja la Blueband, kalamu, cutlery box, vyombo vya plastiki, visu, cutleries (vilia vya mezani), maji ya kilimanjaro na sahani ambazo zote zina thamani ya shilingi milioni moja.

Akitoa ushahidi mahakamani hapo, Mkurugenzi wa Tiba wa Hospitali ya Kilutheri ya Haydom aliiomba mahakama impe adhabu kali mshitakiwa ili iwe fundisho kwa wezi wengine kwani kumekuwepo kwa matukio ya wizi ndani ya hospitali katika siku za karibuni.

Ukistaajabu ya Musa utaona ya firauni: Katika hali ya kushangaza, mshitakiwa alipovunja na kuiba vitu vilivyotajwa hapo juu, alikuta kompyuta ya mapajani yaani laptop aina ya Apple ambayo thamani yake ni zaidi ya shilingi milioni mbili za kitanzania ikiwa katika begi, lakini mshitakiwa aliitoa na kuchukua begi na kulitumia kubebea sahani za plastiki. Kitendo hicho kiliwaacha hoi watu wengi huku wengine wakidai kuwa aliamua kuiacha kwa sababu kama angefanikiwa kuondoka nayo, asingeweza kuiuza hapa haydom bila kukamatwa na wengine wakidai kuwa alikuwa hajui ilikuwa ni kitu gani.

OMBI: Tafadhali usiache kupiga kura ya maoni kuhusu swali letu wiki hii lililopo upande wa juu kulia mwa blogu hii linalosema ``Ni idara ipi ya serikali inaongoza kwa rushwa?``

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda