Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Sunday, May 13, 2012

Akonaay afunguka: Haydom kuwa jimbo kamili 2015

  • Awajia juu watendaji, asema koromeo zao zipo wazi
  • Afunguka kwa Ohayoda; 2015 Haydom jimbo kamili
  • Rose Kamili naye aunguruma
  • Gari la ``mheshimiwa`` lagoma kuwaka
Akonaay akisisitiza jambo

Hatimaye kile kilio cha wananchi wengi wa Haydom na maeneo ya Dongobeshe, maretadu, Maghang, Muslur, Labay na hata Qamatananat ya kutaka jimbo la Mbulu ligawanywe kimesikilizwa na wahusika kwani katika uchaguzi mkuu ujao, hayatakuwa sehemu ya jimbo la Mbulu tena.
Hayo yalithibitishwa na mbunge wa Mbulu mh Mustapha Akonaay alipokuwa akiongea na wananchi katika kata za Maghang, Getarer na Haydom ambapo pia alipata fursa ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa kata hizo.
Katika ziara hiyo, mbunge huyo aliambatana na Rose Kamili ambaye ni mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA, pamoja na uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu ukiongozwa na mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, diwani wa kata husika pamoja na afisa watendaji wa kata na vijiji ambao kwa hakika walisulubishwa na wananchi mbele ya hao wawakilishi hao.
Akijibu hoja za wananchi kuhusu suala la lini mahakama itakuwa tayari kufunguliwa Akonaay alisema kuwa tayari suala hilo limekwishapitishwa na vyombo husika kilichobaki ni utekelezaji, jibu lililowapa wananchi hisia kuwa limetolewa kisiasa zaidi kwani awali alidai kuwa Haydom haikuwa na kigezo cha kuwa na watu 30,000 lakini baadaye akabadili majibu.
Kama ilivyotarajiwa suala la maji na ardhi lilikuwa mbele kabisa ya kero za ``wapiga kura`` hao waliokuwa na jazba na hasira hasa dhidi ya watendaji wa halmashauri. Kuhusu maji mbunge huyo alieleza kuwa kwa mwaka huu miradi ya maji imepelekwa katika vijiji vya Masieda na Harsha huku ule ule mradi wa maji wa Haydom wenye thamani ya shilingi milioni 800 kutoka Benk ya Dunia bado fedha zake hazijapatikana, na kuwasihi wananchi hao kuwa na subira.
``Kuhusu kero za ardhi, msiende kwa watendaji nendeni mahakamani, ndipo haki inapopatikana`` alieleza mbunge huyo ambaye aliingia bungeni mwaka 2010 baada ya kumbwaga aliyejiita ``mbunge wa maisha`` wa mbulu Philip Marmo.
Katika mkutano huo, Akonaay aliahidi kuwabana watendaji wa halmashauri ambao aliwaita ``koromeo zao zipo wazi``, kwani ni asilimia 10 tu ya kiasi cha fedha zinazoteloewa kwa ajili ya shughuli za maendeleo kinawafikia wananchi huku zingine wakizimeza. Aliongeza kuwa viongozi hao wamekuwa si waaminifu hasa katika vocha zinazotolewa kwa wananchi baada ya mwananchi moja kupinga mbele ya mkutano huo taarifa ya kupelekwa vocha 50 kijiji cha Ng`wandakw.
``wanawaibia wananchi, na hili suala la vocha minaona halina maana kabisa lingefutwa kabisa`` alisema Akonaay ``watendaji wameona vidole vya mikono havitoshi wameamua kuweka hadi vya miguu`` huku akishangiliwa na umati uliokwepo hapo.
Suala la afya nalo liliibuka ambapo wananchi walidai kuwa mzigo wa huduma za afya kwa Haydom na maeneo ya jirani umeachiwa hospitalia ya Kilutheri ya Haydom (HLH) na wakaitaka serikali iipatie hospitali hiyo ruzuku zaidi ili wapate huduma ka bei nafuu zaidi sawa na wananchi wa sehemu zingine
``Kama hakuna zahanati ya serikali hapa Haydom basi serikali ipeleke hizo fedha HLH ili zipunguze gharama  nasi tupate huduma kwa bei nafuu kama Watanzania wengine`` alisema moja wa wananchi wliofurika katika viwaja vya CCM.
Akizungumzia suala hilo mbunge huyo alisema kuwa atafanya mkutano na Uongozi wa HLH baada ya mkutano huo na watajadili mambo mbalimbali hasa ya kuboresha huduma za afya mojawapo likiwa namna ya kuongeza ruzuku. Ohayoda litakuletea baadaye yaliyojiri katika mkutano huo.
Mkutano huo ulitiwa nakshi zaidi na uwepo wa mwanasiasa machachari Rose Kamili ambaye hakuficha hasira zake dhidi ya watendaji na wakubwa wa halmashauri. Alimhakikishia Akonaay kuwa watasidiana kuhakikisha kero za wananchi zinapata utatuzi muafaka kwa kuwabana viongozi wanaofuja mali za umma.
Rose aliendelea kufunguka kuwa asilimia 20 ya kodi inayokusanywa katika eneo husika inapaswa kurudi kusaidia shughuli za maendeleo katika eneo husika jambo ambalo halifanyiki.

Wakati huo huo, ohayoda iliweza kufanya mahojiano na mbunge huyo baada ya mkutano huo kujua hatma ya jimbo la Mbulu kugawanywa, Akonaay alisema kuwa suala hilo lilikwisha kupitishwa kabla hata ya uchaguzi uliopita ila mbunge aliyemtangulia alifanya hujuma kwa kulichelewesha
``yule bwana wa CCM aliyenitangulia alidhani kuwa jimbo linkigawanywa asingeweza kushinda hivyo alifanya hujuma huchelewesha japo lilikwishakupitishwa badala yake akawalaghai wananchi kwa kuongeza idadi ya kata pasipo na msingi wowote na kuiongezea halmashauri mzigo mkubwa wa gharama zisizo na msingi.Mbulu mjini kuna kata kibao, Maghang kutoa kata tatu ni haiingii akilini`` alifunguka
``Kama unampango wa kugombea usiwe na mashaka Haydom litakuwa jimbo kamili 2015`` alisema huku akimtania mwandishi wa Ohayoda bila kutaja jina kamili la jimbo na wala makao yake makuu.
Itakumbukwa kuwa katika moja ya makala za kwanza kabisa toka kuanzishwa kwa Ohayoda iliyoitwa HAYDOM2015, tulieleza kero mbalimbali zinazowakabiliwananchi wa Haydom na maeneo ya jirani  vikiwemo barabara na mahakama ambavyo viliibuka katika mkutano wa jana. Ohayoda inaamini kuwa huu ni muda wa utekelezaji wa ahadi mbalimbali wanazotoa hao wanasiasa kwani ``ndoa yao na wananchi`` itakapofika mwisho mwaka 2015 hapatatosha.
Gari la mheshimiwa likipigwa ``busti`` baada ya kugoma kuwaka

Katika hatua nyingine gari la mheshimiwa Akonaay liligoma kuwaka baada ya kumaliza kikao na uongozi wa Hospitali baada ``makosa ya fundi`` kuweka betri tofauti na betri halali ya gari na hivyo kuchelewesha msafara wake uliokuwa umeambatana na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari kwa muda wa takribani nusu saa kabla hajapigwa ``busti`` na kisha kuondoka.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda