Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, May 11, 2012

Afya Kwanza: Ujue Ugonjwa wa Kisukari


Na Beatrice Githiri, Kitengo cha Kisukari-HLH 
Napenda kuwakaribisha wapenzi wasomaji wa Ohayoda katika sehemu ya kwanza ya makala hii ya AFYA KWANZA itakayokuwa inakujia kila siku ya Ijumaa. Lakini kabla ya yote napenda kutoa shukrani za dhati kwa Ohayoda kwa kutupa  nafasi ya kuzungumzia na kutafakari afya zetu. Ni matumaini yangu kwamba utafurahia kusoma na kuyatekeleza ili kuimarisha afya yako na hatimaye kukuza kipato cha familia na taifa letu kwa ujumla.Mara nyingi tunajisahau kuchunguza afya zetu na hivyo tunajisababishia matatizo na madhara mengi na kuongeza gharama za maisha pia.

Leo makala yetu itahusu ugonjwa wa kisukari ambao umekuwa ukiathiri watu wengi katika miaka ya karibuni, wakubwa kwa wadogo na wake kwa waume.

UGONJWA WA KISUKARI
Ugonjwa wa kisukari ni mlolongo wa matatizo mwilini,ya mda mrefu na mfupi kutokana na upungufu au kutoweza kutumika vizuri kwa kichocheo kinachoitwa insulin. Insulin hutengenezwa na chembechembe zilizopo ndani ya kiungo cha kongosho. Miili yetu inahitaji insulin ili kuweza kutumia sukari tuliyonayo mwilini. Sukari inatokana na chakula ambacho tunakula kila siku na hutumika kwa kutupa nguvu mwilini. Kwa kawaida sukari ikizidi, ya ziada inahifadhiwa katika ini kama mafuta. Mafuta haya hubadilishwa kuwa sukari na kutumika wakati tukiwa na njaa kwa mda mrefu. Endapo kuna matatizo ya kutengeneza au kutumika kwa insulin, sukari mwilini huongezeka haraka na inamaanisha ugonjwa wa kisukari upon a dalili kuanza kuonekana.

Viashiria vya ugonjwa wa kisukari (risk factors) 
 • Unene uliozidi na kiribatumbo
 • Ulaji mbaya wa chakula
 • Baadhi ya madawa
 • Msongo wa mawazo
 • Historia ya ugonjwa wa kisukari kwenye familia
 • Tezi ya shingo (husababisha mwili kukua na kuongezeka haraka)
 • Kutofanya mazoezi
 • Umri zaidi ya miaka arobaini (kadri tunavyozeeka na kongosho letu linapungua uwezo wa kutoa insulin hivyo kusababisha kisukari)
 • Magonjwa yanayoharibu kongosho
 • Akina mama wanaojifungua watoto wenye kilo zaidi ya arobaini (Mara nyingi hawa akina mama huwa na ugonjwa wa kisukari ila hawagunduliki hadi mtoto anapozaliwa na kuonekana mkubwa)
 • Akina mama wenye historia ya kisukari wakati wa ujauzito
 • Utumiaji uliozidia pombe na uvutaji sigara
Dalili za ugonjwa wa kisukari
 •     Kiu ya mara kwa mara
 •     Kupungua uzito licha ya kula vizuri
 •     Njaa kali na ya mara kwa mara
 •     Jasho jingi
 •      Uchovu usioeleweka hata bila kufanya kazi
 •     Kizunguzungu
 •      Macho kupungua uwezo wa kuona
 •      Kidonda kisichopona haraka
Tiba ya ugonjwa wa kisukari
 • Tiba bila dawa- ukigundulika unatakiwa kula chakula utakachoshauriwa na kufanya mazoezi ili ili kushusha sukari yako iwe ya kawaida.
 • Tiba kwa vidonge-wengine hawawezi kutumia chakula tu kwa kushusha sukari hivyo wanapewa dawa za vidonge ili kushusha sukari yao pamoja na chakula.
 • Tiba kwa kutumia sindano ya insulin-wanopata kisukari kabla ya miaka 35 lazima watumie insulin ili kuishi. Pia wagonjwa wa umri zaidi ya miaka 35 inawezekane sukari yao isishuke kwa vidonge hivyo namna ya tiba yao inabaki kuwa sindano tu.
Madhara ya ugonjwa wa kisukari
Endapo ugonjwa wa kisukari utapuuzwa au kutotibiwa inavyostahili madhara mengi yanaweza kujitokeza na yanatokana na kiwango cha sukari kuwa  juu mwilini.
 • Magonjwa ya moyo
 • Kiharusi
 • Kupungua nguvu za kiume
 • Figo kushindwa kufanya kazi
 • upofu
Ni matumaini yangu wewe msomaji umenufaika na hili somo na pia utanufaishaisha familia na jamii iliokuzunguka.
Kama hujapata huu ugonjwa ni muhimu kuepuka unene uliozidi kwa kula lishe nzuri na  ya kiasi, epuka pombe, msongo wa mawazo, pombe na uvutaji wa sigara na la muhimu zaidi ni mazoezi ya viungo .
Tunashauriwa kupima kama tuna ugonjwa wa kisukari kila mwaka, hivyo basi nenda mapema ili kuepuka madhara.
Hospitali ya Haydom ina kitengo cha kisukari na tunawashauri wote walio na umri zaidi ya miaka 35 waje kwa Kupima na ushauri. Kipimo ni shilingi ni elfu na mia tano tu(1500)!

OMBI: Usiache kupigia swali letu la wiki hii upande wa juu kulia mwa blogu hii, ambalo linauliza ni idara ipi ya serikali inaongoza kwa rushwa katika mikoa ya Manyara, Singida na Arusha?

1 comment:

 1. Kisukari kinatibika wapendwa kwa kutumia virutubisha na kutumia viini lishe mbalimbali mfano hii kifaa kinapatikana dar es salaam na ukihitaji unaweza kutumiwa pia  Nano Cup-black

  Nano energy cup adopts nano composite material and energetic biochemical ceramic which is an abstract from lavae. It‘s formed after high temperature from special tombar thite material. On contact with water, it becomes smaller molecule energy-water that not only strengthens physiological function, purity, penetrability, expandability and emulsifying ability of water, but also contains negative potential and anti-oxidation material, so that it removes acidic materials and free radical from human body.

  Functions:

  1. Accelerate metabolism and enhance immunity

  2. Accelerate activation of ferment

  3. Reduce harmful effects of cigarette and alcohol

  4. Reduce blood fat and gout

  5. Accelerate liver vermiculation and reduce astriction

  6. Reduce acidity of human body

  7. Purify blood, alleviate hardening of artery and stroke

  8. Reduce high blood pressure and diabetes

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda