Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, May 31, 2012

AFYA KWANZA: KUTIBU MAUMIVU YA MGONGO UKIWA NYUMBANI


Na Beatrice Githiri-HLH
Leo Afya kwanza inazungumzia jinsi ya kupunguza au kutibu maumivu ya mgongo. Mara nyingi haya matatizo yanatokana na kunyanyua vitu vizito, kukaa au kuinama vibaya na pia kulala vibaya. Haya maumivu huisha ndani ya iki 2 au 3.
Ni vyema kumwona daktari haraka ikiwa maumivu yako ya mgongo yametokana na kuanguka, kugongwa na kitu Fulani pia kama hayo maumivu yanasababisha ganzi au ulegevu wa mguu mmoja au yote miwili au unapata matatizo katika kibofu au mfumo wa haja kubwa.

  1. weka barafu kisha kanda kutumia kitu cha joto katika sehemu ya maumivu mgongoni
weka barafu mara 4 kwa kutwa katika sehemuya maumivu kwa mda usiozidi kakika 20. tia barafu ndani ya mfuko wanailoni, kasha zungushia kitambaa au taulo ili kuepusha barafu kugusa ngozi yakomoja kw moja.
Baada ya maumivu kupungua ndani ya siku 2, jaribu kuweka kitu cha moto kama vile chupa yenye maji ya moto, hot appliances kama hot water bottles au kuogea maji ya moto. Hakikisha unazungushia kitambaa kwenye chombo cha moto utakachokitumia. Usizidishe dakika 20katika kuweka chombo cha moto,pia epuka kusinzia ukiwa na chombo cha moto ili kuepua hatari ya kuungua.

  1. tumia dawa za kutuliza maumivu
tumia dawa za kutuliza maumivu na kupunguza inflammation katika sehemu yamaumivu mgongoni kwa mfano asprin au ibuprofen. Dawa za kuchua pia zinaweza kutuliza haya maumivu ya mgongo. Ni vyema kufuata dose ilioshauriwa na kama unatumia madawa mengine pata ushauri wa daktari kwanza.

  1. pumzikana pia pata mazoezi laini
Pumzika kitandani vya kutosha ila usizidishe kulala sana kitandani. Kulala mda mrefunazaidiya siku 2, hufanya kuona kuchukua mda mrefu zaidi.
Mazoezi ya kiasi na kujinyoosha husaidia misuli kuwa na nguvu na kuwa laini (flexible), hivyo kufupisha mda wa maumivu.

NB: Epuka kubeba, kunyanyanyua au kusukuma vitu vizito au vigumu. Kufanya hivyo kutafanya maumivu ya mgongo kuongezeka na kusababisha madhara zaidi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda