Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, May 24, 2012

AFYA KWANZA: JINSI YA KUZUIA CHOO KIGUMU (CONSTIPATION)


Na Beatrice Githiri-HLH
Afya ya tumbo na choo ni sehemu muhimu katika maisha yetu. Wengine wanaona ni aibu kujadili hii mada hata wanapofika hospitalini. Hii ni sehemu muhimu na nyeti katka afya pia.madhara ya kuwa na choo kigumu nina imani tunayafahamu maana kila mmoja wetu lazima aliwahi kupata. Hili tatizo kwa wengine ni sugu na wangependa kufahamu namna ya kuepukana na hili tatizo. Nitaeleza baadhi ya njia za kuzuia choo kuwa kigumu na ni matumaini yangu wengi mtafaidika na mada hii.

  • Kula milo yote bila kuepuka mlo wowote
Kula milo iliokamilika(protini, wanga na vitamini) kwa muda maalum bila kuepuka mlo Fulani: kwa mfano kuacha chakula cha mchana au asubuhi. Milo iliopangiliwa husaidia kutupa mfumo wa choo uliowa kawaida.

  • Kula vyakula vyenye vinyunyuzi vingi (high fibre diet)
Vyakula visivyokobolewa kwa mfano dona, matunda na mboga mboga hutusaidia katika kulainisha choo na pia kuzuia uwezekano wa kupata kansa ya utumbo. Hivyo ni muhimu kufanya vinyunyuzi kuwa sehemu ya milo yako ya kila wakati na kila siku.

  • Kunywa maji mengi
Bila maji afya zetu ni mbovu, na vivyo hivyo bila kunywa maji ya kutosha husababisha choo chetu kuwa kigumu. Tunashauriwa knywa zaidi ya glasi nane 8 za maji kila siku.vitu kama maziwa, supu na juisini sehemu ya kutuongezea maji mwilini. Hakikisha maji yako ni safi na salama kabla ya kunywa.

  • Ongeza mazoezi ya viungo
Mazoezi ni moja yapo ya sehemu ya kutulainishia choo na hivyo yunashauriwa kufanya mazoezi ya viungo angalau mara 3 kwa wiki na zaidi kwa muda usiopungua dakika 30. Kutembea, kuendesha baiskeli, kuruka kamba au kuogelea ni aina yamazoezi.

  • Jibu haja yako
Wengi wanamazoea ya kubana haja kubwa wanapoipata na kufikiri wanaweza kuahirisha zoezi hilo hadi wakati mwingine.kujibana husababisha choo chetu kukauka. Mara pengne mazingira hayaruhusu hivyo inabidi tuzuie haja lakini kutotii nako kuna madhara yake.

  • Kubaliana na mfumo wako wa kupata choo
Kwa wengine ni kawaidakupata choo mara nyingi kwa siku na wengine hupata hata ara 3 tu kwa wiki. Uyeyushaji wa chakula na mfumo wa choo w kila mtu ni tofauti. Endapo unapata choo cha kawaida na laini hata kama sio kila siku usiogope.

  • Usizoee mdawa ya kulainisha choo au kuharisha
Baadhi ya madawa haya husumbua au(irritate) utumbo pia yanaweza kufanya hali ya kukaukiwa na choo kuwa mbaya zaidi. Endapo unahitaji hizi dawa ni vyema kupata ushauri wa daktari kabla ya kuzitumia.


Endapo choo chako kitaendelea kuwa kigumu na cha shida licha ya kufuuata ushauri huu wa makala ya afya kwanza ni vyema kumwona daktari kwa msaada na tiba zaidi. Wakati mwingine hii hali inaweza kuwa dalili ya ugonjwa mwingine.
Makala hii ipo kwa ajili ya kuboresha afya zetu pia tusiwe wachoyo kuwaelimisha ndugu na jamaa zetu ambao hawawezi kusoma makala yetu ya AFYA KWANZA

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda