Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, April 30, 2012

SEMINA YA MALEZI, MAKUZI NA MAWASILIANO YA MTOTO YAFANYIKA HAYDOM

``Nondo`` za semina

Semina hii ilifanyika katika ukumbi wa Ofisi za jimbo la Kanisa la Kiinjili kilutheri Tanzania (KKKT), Haydom kuanzia tarehe 23 hadi tarehe 27 Aprili 2012, iliandaliwa kwa ushirikiano baina ya Hospitali ya Sorlandet Sykenhus HF ya Christiansand-Norway, Jumuiya ya Haydom kupitia Haydom Lutheran Hospital na Kikundi Cha Wanawake Kupambana na UKIMWI Kilimanjaro-KIWAKUKI chini ya mpango wa Kimataifa wa Maendeleo Ya Mtoto yaani International Child Development Program (ICDP)
Akizungumzia mara baada ya kumalizika kwa semina, Mratibu wa Semina hiyo, Martha Masawe ambaye pia ni Afisa Tawala wa HLH, alisema kuwa imekuwa na mafanikio makubwa tofauti na matarajio ya awali kwani washiriki siyo tu walitoa ushirikiano kwa wakufunzi bali pia walibadilika mtazamo wao juu ya malezi na makuzi ya watoto. Aidha alizidi kuongeza kuwa anaamini semina hiyo itainufaisha jamii kwani kupitia mafunzo hayo washiriki wataenda kuihamasisha jamii juu ya kuwalea watoto katika njia ipasayo na kujenga jamii bora

Mama Verynice Monyo, akitoa darasa
Nao wakufunzi katika semina hiyo, Verynice Monyo na Egla H. Matechi kutoka KIWAKUKI walieleza kuwa walifurahishwa na ushirikiano walioupata hasa kutoka kwa washiriki na kuwa washiriki walikuwa wanajituma kujifunza na wao kama wakufunzi wamejifunza pia kupitia kwa washiriki hao, na zaidi walishangazwa na upendo waliooneshwa na washiriki kwa kuwapa zawadi.
Semina hiyo iliyowashirikisha washiriki 13 kutoka vijiji zaidi ya 6 vya kata ya Haydom, ilifunguliwa na Mkurugenzi wa Tiba wa HLH Dr. Olaf Espegren kisha kuzinduliwa na Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Haydom Mch. Zakaria Dalei na kufungwa na Martha Masawe kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tiba wa HLH siku ya Ijumaa tarehe 27 Aprili 2012


Mkurugenzi wa Tiba wa HLH Dr. Olaf Espegren akizungumza na Washiriki wa Semina ya ICDP baada ya kufungua Semina


Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wakufunzi na Dr. Olaf Espegren

Mkurugenzi wa Tiba wa HLH Dr. Olaf Espegren wakati wa ufunguzi


Mchungaji Zakaria Dalei akisoma neno la Mungu wakati wa ufunguzi


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda