Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, April 30, 2012

Haydom2015

Karibuni ndugu wanaHaydom na maeneo ya jirani kwenye hili jamvi jipya kwa ajili ya kupeana habari, kuelimishana na kuhamasishana kuhusu maswala mbalimbali yanayojiri huku kwetu hususani tunapoelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambao tunatarajia ulete mabadiliko mengi sana kwa wananchi wa Haydom na Tanzania kwa ujumla.

Kwa nini HAYDOM2015?
Jibu lake ni rahisi sana kama 1+1=2....Haydom lazima iwe jimbo kamili la Uchaguzi ifikapo 2015. Haydom inakila sababu ya kuwa jimbo, vigezo vyote vya kijiografia, idadi ya watu na huduma za jamii zinatosheleza kama yalivyo majimbo mengine nchini. Na kulifanikisha hilo ndio maana tunaanza kuwakumbusha hao wakuu wa kaya huko juu wanaofanya maamuzi wajue mapema kuwa bila jimbo 2015 hakitaeleweka.
Ndugu zangu wana Haydom hasa wasomi (wengi wetu tukiwa mijini), toka uhuru tumekuwa chini sana bila kuwa na sauti wala wa kutusikiliza, tumewaachie wengine watuamulie mambo yetu na tumeonekana wanyonge kiasi cha kutosha. Embu fikiria umbali toka Haydom hadi Mbulu ni takriban KM 85, zaidi ya umbali toka Arusha hadi Moshi yaani makao makuu ya mikoa miwili ambayo kati ya hiyo mikoa kuna majimbo zaidi ya manne, NDIYO, MAJIMBO MANNE! ya Arusha Mjini, Arumeru Mashariki, Hai na Moshi Mjini! sisi bado tu tupo kwenye jimbo moja!
 Pamoja na uwepo wa moja ya Hospitali kubwa sana nchini ambayo hivi karibuni imeteuliwa kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, yenye zaidi ya wafanyakazi 500, ikiwa ndiyo kitovu kikuu cha biashara cha wilaya ya Mbulu, Haydom inagusa maelfu ya maisha ya watu siyo tu mkoani manyara bali hata katika mikoa ya Singida, Arusha na Shinyanga. Lakini ni aibu isiyoelezeka kuwa, miaka 50 baada ya Uhuru kuwa Haydom hamna Benki, hamna mahakama, hamna huduma nyingi muhimu za kijamii ambazo unapozihitaji inabidi usafiri zaidi ya KM 85 kuzipata...MIAKA 50 baada ya Uhuru! Imefika mahali wakubwa hao waelewe kuwa TUMECHOKA!
Inauma sana unapoteza kitambulisho au nyaraka zozote za muhimu inakubidi utumie gharama zaidi ya Shilingi 15,000/= na usumbufu wa kuamka saa 10 usiku kwenda kulipia Shilingi 500 upate ``Police Loss Report``!
Inauma sana wafanyakazi pamoja na mshahara mdogo walionao hasa walimu, wauguzi na madaktari wanatumia zaidi ya Shilingi 20,000 kwenda kuchukua mshahara wakati nyongeza ya mshahara ni Shilingi 12,000
Inauma sana TRA wanakusanya kodi zetu tena wakati mwingine isivyo kihalali lakini bado tunabarabara mbovu, masika matope na madimbwi kiangazi vumbi zaidi ya poda!
Inauma sana hatumwoni mbunge wetu, yawezekana pengine kwa kuwa hajui kero zetu au ni kwa kuwa jimbo ni kubwa sana na amezidiwa na majukumu ya ``  Kamati ya Bunge``
Inauma sana, tena sana na inasikitisha....HAKUNA MAHAKAMA! Hili pengine ndilo linaloumiza zaidi kwani najiuliza ni watu wangapi wamepoteza haki zao kwa kukosa huduma za kimahakama?
Orodha ni ndefu mno, inazidi kunitia uchungu kuendelea kwani maumivu yake twayajua sisi! IMETOSHA

Kwa pamoja tunaweza, 2015 si mbali na tunaweza kufanya mabadiliko tukawa sehemu ya historia bila kujali itikadi zetu za kisiasa au kidini, HAYDOM2015 INAWEZEKANA NA INAANZA LEO!
Tafakari Chukua HatuaNo comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda